Mathayo 13 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mathayo 13 (Swahili) Matthew 13 (English)

Siku ile Yesu akatoka nyumbani, akaketi kando ya bahari. Mathayo 13:1

On that day Jesus went out of the house, and sat by the seaside.

Wakamkusanyikia makutano mengi, hata akapanda chomboni, akaketi; na ule mkutano wote wakasimama pwani. Mathayo 13:2

Great multitudes gathered to him, so that he entered into a boat, and sat, and all the multitude stood on the beach.

Akawaambia mambo mengi kwa mifano, akisema, Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda. Mathayo 13:3

He spoke to them many things in parables, saying, "Behold, a farmer went out to sow.

Hata alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila; Mathayo 13:4

As he sowed, some seeds fell by the roadside, and the birds came and devoured them.

nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara zikaota, kwa udongo kukosa kina; Mathayo 13:5

Others fell on rocky ground, where they didn't have much soil, and immediately they sprang up, because they had no depth of earth.

na jua lilipozuka ziliungua; na kwa kuwa hazina mizizi zikanyauka. Mathayo 13:6

When the sun had risen, they were scorched. Because they had no root, they withered away.

Nyingine zikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea, ikazisonga; Mathayo 13:7

Others fell among thorns. The thorns grew up and choked them:

nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini. Mathayo 13:8

and others fell on good soil, and yielded fruit: some one hundred times as much, some sixty, and some thirty.

Mwenye masikio na asikie. Mathayo 13:9

He who has ears to hear, let him hear."

Wakaja wanafunzi, wakamwambia, Kwa nini wasema nao kwa mifano? Mathayo 13:10

The disciples came, and said to him, "Why do you speak to them in parables?"

Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa. Mathayo 13:11

He answered them, "To you it is given to know the mysteries of the Kingdom of Heaven, but it is not given to them.

Kwa maana ye yote mwenye kitu atapewa, naye atazidishiwa tele; lakini ye yote asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa. Mathayo 13:12

For whoever has, to him will be given, and he will have abundance, but whoever doesn't have, from him will be taken away even that which he has.

Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa. Mathayo 13:13

Therefore I speak to them in parables, because seeing they don't see, and hearing, they don't hear, neither do they understand.

Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona. Mathayo 13:14

In them the prophecy of Isaiah is fulfilled, which says, 'By hearing you will hear, And will in no way understand; Seeing you will see, And will in no way perceive:

Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya. Mathayo 13:15

For this people's heart has grown callous, Their ears are dull of hearing, They have closed their eyes; Or else perhaps they might perceive with their eyes, Hear with their ears, Understand with their heart, And should turn again; And I would heal them.'

Lakini, heri macho yenu, kwa kuwa yanaona; na masikio yenu, kwa kuwa yanasikia. Mathayo 13:16

"But blessed are your eyes, for they see; and your ears, for they hear.

Kwa maana, amin, nawaambia, Manabii wengi na wenye haki walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi, wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi, wasiyasikie. Mathayo 13:17

For most assuredly I tell you that many prophets and righteous men desired to see the things which you see, and didn't see them; and to hear the things which you hear, and didn't hear them.

Basi ninyi sikilizeni mfano wa mpanzi. Mathayo 13:18

"Hear, then, the parable of the farmer.

Kila mtu alisikiapo neno la ufalme asielewe nalo, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia. Mathayo 13:19

When anyone hears the word of the Kingdom, and doesn't understand it, the evil one comes, and snatches away that which has been sown in his heart. This is what was sown by the roadside.

Naye aliyepandwa penye miamba, huyo ndiye alisikiaye lile neno, akalipokea mara kwa furaha; Mathayo 13:20

What was sown on the rocky places, this is he who hears the word, and immediately with joy receives it;

lakini hana mizizi ndani yake, bali hudumu kwa muda; ikitukia dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara huchukizwa. Mathayo 13:21

yet he has no root in himself, but endures for a while. When oppression or persecution arises because of the word, immediately he stumbles.

Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai. Mathayo 13:22

What was sown among the thorns, this is he who hears the word, but the cares of this age and the deceitfulness of riches choke the word, and he becomes unfruitful.

Naye aliyepandwa penye udongo mzuri, huyo ndiye alisikiaye lile neno, na kuelewa nalo; yeye ndiye azaaye matunda, huyu mia, na huyu sitini, na huyu thelathini. Mathayo 13:23

What was sown on the good ground, this is he who hears the word, and understands it, who most assuredly bears fruit, and brings forth, some one hundred times as much, some sixty, and some thirty."

Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake; Mathayo 13:24

He set another parable before them, saying, "The Kingdom of Heaven is like a man who sowed good seed in his field,

lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake. Mathayo 13:25

but while people slept, his enemy came and sowed darnel{darnel is a weed grass (probably bearded darnel or lolium temulentum) that looks very much like wheat until it is mature, when the difference becomes very apparent.} also among the wheat, and went away.

Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu. Mathayo 13:26

But when the blade sprang up and brought forth fruit, then the darnel appeared also.

Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu? Mathayo 13:27

The servants of the householder came and said to him, 'Sir, didn't you sow good seed in your field? Where did this darnel come from?'

Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye? Mathayo 13:28

"He said to them, 'An enemy has done this.' "The servants asked him, 'Do you want us to go and gather them up?'

Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing'oa ngano pamoja nayo. Mathayo 13:29

"But he said, 'No, lest perhaps while you gather up the darnel, you root up the wheat with them.

Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu. Mathayo 13:30

Let both grow together until the harvest, and in the harvest time I will tell the reapers, "First, gather up the darnel, and bind them in bundles to burn them; but gather the wheat into my barn."'"

Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya haradali, aliyoitwaa mtu akaipanda katika shamba lake; Mathayo 13:31

He set another parable before them, saying, "The Kingdom of Heaven is like a grain of mustard seed, which a man took, and sowed in his field;

nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hata nyuni wa angani huja na kukaa katika matawi yake. Mathayo 13:32

which indeed is smaller than all seeds. But when it is grown, it is greater than the herbs, and becomes a tree, so that the birds of the air come and lodge in its branches."

Akawaambia mfano mwingine; Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyoitwaa mwanamke, akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachachwa wote pia. Mathayo 13:33

He spoke another parable to them. "The Kingdom of Heaven is like yeast, which a woman took, and hid in three measures{Literally, satas. 3 satas = about 0.5 bushel or 22 litres} of meal, until it was all leavened."

Hayo yote Yesu aliwaambia makutano kwa mifano; wala pasipo mfano hakuwaambia neno; Mathayo 13:34

Jesus spoke all these things in parables to the multitudes; and without a parable, he didn't speak to them,

ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema, Nitafumbua kinywa changu kwa mifano, Nitayatamka yaliyositirika tangu awali. Mathayo 13:35

that it might be fulfilled which was spoken through the prophet, saying, "I will open my mouth in parables; I will utter things hidden from the foundation of the world."

Kisha Yesu akawaaga makutano, akaingia nyumbani; wanafunzi wake wakamwendea, wakasema, Tufafanulie mfano wa magugu ya kondeni. Mathayo 13:36

Then Jesus sent the multitudes away, and went into the house. His disciples came to him, saying, "Explain to us the parable of the darnel of the field."

Akajibu, akasema, Azipandaye zile mbegu njema ni Mwana wa Adamu; Mathayo 13:37

He answered them, "He who sows the good seed is the Son of Man,

lile konde ni ulimwengu; zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu; Mathayo 13:38

the field is the world; and the good seed, these are the children of the Kingdom; and the darnel are the children of the evil one.

yule adui aliyeyapanda ni Ibilisi; mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika. Mathayo 13:39

The enemy who sowed them is the devil. The harvest is the end of the age, and the reapers are angels.

Basi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia. Mathayo 13:40

As therefore the darnel is gathered up and burned with fire; so will it be at the end of this age.

Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi, Mathayo 13:41

The Son of Man will send out his angels, and they will gather out of his Kingdom all things that cause stumbling, and those who do iniquity,

na kuwatupa katika tanuru ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. Mathayo 13:42

and will cast them into the furnace of fire. There will be weeping and the gnashing of teeth.

Ndipo wenye haki watakapong'aa kama jua katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio, na asikie. Mathayo 13:43

Then the righteous will shine forth like the sun in the Kingdom of their Father. He who has ears to hear, let him hear.

Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile. Mathayo 13:44

"Again, the Kingdom of Heaven is like a treasure hidden in the field, which a man found, and hid. In his joy, he goes and sells all that he has, and buys that field.

Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri; Mathayo 13:45

"Again, the Kingdom of Heaven is like a man who is a merchant seeking fine pearls,

naye alipoona lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda akauza alivyo navyo vyote, akainunua. Mathayo 13:46

who having found one pearl of great price, he went and sold all that he had, and bought it.

Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya samaki wa kila namna; Mathayo 13:47

"Again, the Kingdom of Heaven is like a dragnet, that was cast into the sea, and gathered some fish of every kind,

hata lilipojaa, walilivuta pwani; wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wabaya wakawatupa. Mathayo 13:48

which, when it was filled, they drew up on the beach. They sat down, and gathered the good into containers, but the bad they threw away.

Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki, Mathayo 13:49

So will it be in the end of the world. The angels will come forth, and separate the wicked from among the righteous,

na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. Mathayo 13:50

and will cast them into the furnace of fire. There will be the weeping and the gnashing of teeth."

Yesu aliwauliza, Mmeyafahamu hayo yote? Wakamwambia, Naam. Mathayo 13:51

Jesus said to them, "Have you understood all these things?" They answered him, "Yes, Lord."

Akawaambia, Kwa sababu hiyo, kila mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni amefanana na mtu mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale. Mathayo 13:52

He said to them, "Therefore, every scribe who has been made a disciple in the Kingdom of Heaven is like a man who is a householder, who brings out of his treasure new and old things."

Ikawa Yesu alipoimaliza mifano hiyo, alitoka akaenda zake. Mathayo 13:53

It happened that when Jesus had finished these parables, he departed from there.

Na alipofika nchi yake, akawafundisha katika sinagogi lao, hata wakashangaa, wakasema, Huyu amepata wapi hekima hii na miujiza hii? Mathayo 13:54

Coming into his own country, he taught them in their synagogue, so that they were astonished, and said, "Where did this man get this wisdom, and these mighty works?

Huyu si mwana wa seremala? Mamaye si yeye aitwaye Mariamu? Na nduguze si Yakobo, na Yusufu, na Simoni, na Yuda? Mathayo 13:55

Isn't this the carpenter's son? Isn't his mother called Mary, and his brothers, James, Joses, Simon, and Judas?

Na maumbu yake wote hawapo hapa petu? Basi huyu amepata wapi haya yote? Mathayo 13:56

Aren't all of his sisters with us? Where then did this man get all of these things?"

Wakachukizwa naye. Yesu akawaambia, Nabii hakosi kupata heshima, isipokuwa katika nchi yake, na nyumbani mwake mwenyewe. Mathayo 13:57

They were offended by him. But Jesus said to them, "A prophet is not without honor, except in his own country, and in his own house."

Wala hakufanya miujiza mingi huko, kwa sababu ya kutokuamini kwao. Mathayo 13:58

He didn't do many mighty works there because of their unbelief.