Mathayo 7 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mathayo 7 (Swahili) Matthew 7 (English)

Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. Mathayo 7:1

"Don't judge, so that you won't be judged.

Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa. Mathayo 7:2

For with whatever judgment you judge, you will be judged; and with whatever measure you measure, it will be measured to you.

Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? Mathayo 7:3

Why do you see the speck that is in your brother's eye, but don't consider the beam that is in your own eye?

Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? Mathayo 7:4

Or how will you tell your brother, 'Let me remove the speck from your eye;' and behold, the beam is in your own eye?

Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako. Mathayo 7:5

You hypocrite! First remove the beam out of your own eye, and then you can see clearly to remove the speck out of your brother's eye.

Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua. Mathayo 7:6

"Don't give that which is holy to the dogs, neither throw your pearls before the pigs, lest perhaps they trample them under their feet, and turn and tear you to pieces.

Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; Mathayo 7:7

"Ask, and it will be given you. Seek, and you will find. Knock, and it will be opened for you.

kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. Mathayo 7:8

For everyone who asks receives. He who seeks finds. To him who knocks it will be opened.

Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? Mathayo 7:9

Or who is there among you, who, if his son asks him for bread, will give him a stone?

Au akiomba samaki, atampa nyoka? Mathayo 7:10

Or if he asks for a fish, who will give him a serpent?

Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao? Mathayo 7:11

If you then, being evil, know how to give good gifts to your children, how much more will your Father who is in heaven give good things to those who ask him!

Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii. Mathayo 7:12

Therefore whatever you desire for men to do to you, you shall also do to them; for this is the law and the prophets.

Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Mathayo 7:13

"Enter in by the narrow gate; for wide is the gate and broad is the way that leads to destruction, and many are those who enter in by it.

Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache. Mathayo 7:14

How{TR reads "Because" instead of "How"} narrow is the gate, and restricted is the way that leads to life! Few are those who find it.

Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. Mathayo 7:15

"Beware of false prophets, who come to you in sheep's clothing, but inwardly are ravening wolves.

Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? Mathayo 7:16

By their fruits you will know them. Do you gather grapes from thorns, or figs from thistles?

Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mathayo 7:17

Even so, every good tree produces good fruit; but the corrupt tree produces evil fruit.

Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Mathayo 7:18

A good tree can't produce evil fruit, neither can a corrupt tree produce good fruit.

Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. Mathayo 7:19

Every tree that doesn't grow good fruit is cut down, and thrown into the fire.

Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua. Mathayo 7:20

Therefore, by their fruits you will know them.

Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Mathayo 7:21

Not everyone who says to me, 'Lord, Lord,' will enter into the Kingdom of Heaven; but he who does the will of my Father who is in heaven.

Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Mathayo 7:22

Many will tell me in that day, 'Lord, Lord, didn't we prophesy in your name, in your name cast out demons, and in your name do many mighty works?'

Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. Mathayo 7:23

Then I will tell them, 'I never knew you. Depart from me, you who work iniquity.'

Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; Mathayo 7:24

"Everyone therefore who hears these words of mine, and does them, I will liken him to a wise man, who built his house on a rock.

mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. Mathayo 7:25

The rain came down, the floods came, and the winds blew, and beat on that house; and it didn't fall, for it was founded on the rock.

Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; Mathayo 7:26

Everyone who hears these words of mine, and doesn't do them will be like a foolish man, who built his house on the sand.

mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa. Mathayo 7:27

The rain came down, the floods came, and the winds blew, and beat on that house; and it fell--and great was its fall."

Ikawa, Yesu alipoyamaliza maneno hayo, makutano walishangaa mno kwa mafundisho yake; Mathayo 7:28

It happened, when Jesus had finished saying these things, that the multitudes were astonished at his teaching,

kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi wao. Mathayo 7:29

for he taught them with authority, and not like the scribes.