Mathayo 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mathayo 1 (Swahili) Matthew 1 (English)

Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu. Mathayo 1:1

The book of the generation of Jesus Christ{Christ (Greek) and Messiah (Hebrew) both mean "Anointed One"}, the son of David, the son of Abraham.

Ibrahimu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake; Mathayo 1:2

Abraham became the father of Isaac. Isaac became the father of Jacob. Jacob became the father of Judah and his brothers.

Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari; Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu; Mathayo 1:3

Judah became the father of Perez and Zerah by Tamar. Perez became the father of Hezron. Hezron became the father of Ram.

Aramu akamzaa Aminadabu; Aminadabu akamzaa Nashoni; Nashoni akamzaa Salmoni; Mathayo 1:4

Ram became the father of Amminadab. Amminadab became the father of Nahshon. Nahshon became the father of Salmon.

Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu; Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu; Obedi akamzaa Yese; Mathayo 1:5

Salmon became the father of Boaz by Rahab. Boaz became the father of Obed by Ruth. Obed became the father of Jesse.

Yese akamzaa mfalme Daudi. Mathayo 1:6

Jesse became the father of David the king. David became the father of Solomon by her who had been the wife of Uriah.

Sulemani akamzaa Rehoboamu; Rehoboamu akamzaa Abiya; Abiya akamzaa Asa; Mathayo 1:7

Solomon became the father of Rehoboam. Rehoboam became the father of Abijah. Abijah became the father of Asa.

Asa akamzaa Yehoshafati; Yehoshafati akamzaa Yoramu; Yoramu akamzaa Uzia; Mathayo 1:8

Asa became the father of Jehoshaphat. Jehoshaphat became the father of Joram. Joram became the father of Uzziah.

Uzia akamzaa Yothamu; Yothamu akamzaa Ahazi; Ahazi akamzaa Hezekia; Mathayo 1:9

Uzziah became the father of Jotham. Jotham became the father of Ahaz. Ahaz became the father of Hezekiah.

Hezekia akamzaa Manase; Manase akamzaa Amoni; Amoni akamzaa Yosia; Mathayo 1:10

Hezekiah became the father of Manasseh. Manasseh became the father of Amon. Amon became the father of Josiah.

Yosia akamzaa Yekonia na ndugu zake, wakati wa ule uhamisho wa Babeli. Mathayo 1:11

Josiah became the father of Jechoniah and his brothers, at the time of the exile to Babylon.

Na baada ya ule uhamisho wa Babeli, Yekonia akamzaa Shealtieli; Shealtieli akamzaa Zerubabeli; Mathayo 1:12

After the exile to Babylon, Jechoniah became the father of Shealtiel. Shealtiel became the father of Zerubbabel.

Zerubabeli akamzaa Abihudi; Abihudi akamzaa Eliakimu; Eliakimu akamzaa Azori; Mathayo 1:13

Zerubbabel became the father of Abiud. Abiud became the father of Eliakim. Eliakim became the father of Azor.

Azori akamzaa Sadoki; Sadoki akamzaa Akimu; Akimu akamzaa Eliudi; Mathayo 1:14

Azor became the father of Sadoc. Sadoc became the father of Achim. Achim became the father of Eliud.

Eliudi akamzaa Eleazari; Eleazari akamzaa Matani; Matani akamzaa Yakobo; Mathayo 1:15

Eliud became the father of Eleazar. Eleazar became the father of Matthan. Matthan became the father of Jacob.

Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo. Mathayo 1:16

Jacob became the father of Joseph, the husband of Mary, from whom was born Jesus{"Jesus" is a Greek variant of the Jewish name "Yehoshua," which means "Yah saves." "Jesus" is also the masculine form of "Yeshu'ah," which means "Salvation."}, who is called Christ.

Basi vizazi vyote tangu Ibrahimu hata Daudi ni vizazi kumi na vinne; na tangu Daudi hata ule uhamisho wa Babeli ni vizazi kumi na vinne; na tangu ule uhamisho wa Babeli hata Kristo ni vizazi kumi na vinne. Mathayo 1:17

So all the generations from Abraham to David are fourteen generations; from David to the exile to Babylon fourteen generations; and from the carrying away to Babylon to the Christ, fourteen generations.

Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Mathayo 1:18

Now the birth of Jesus Christ was like this; for after his mother, Mary, was engaged to Joseph, before they came together, she was found pregnant by the Holy Spirit.

Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri. Mathayo 1:19

Joseph, her husband, being a righteous man, and not willing to make her a public example, intended to put her away secretly.

Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Mathayo 1:20

But when he thought about these things, behold, an angel of the Lord appeared to him in a dream, saying, "Joseph, son of David, don't be afraid to take to yourself Mary, your wife, for that which is conceived in her is of the Holy Spirit.

Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao. Mathayo 1:21

She shall bring forth a son. You shall call his name Jesus, for it is he who shall save his people from their sins."

Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema, Mathayo 1:22

Now all this has happened, that it might be fulfilled which was spoken by the Lord through the prophet, saying,

Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi. Mathayo 1:23

"Behold, the virgin shall be with child, And shall bring forth a son. They shall call his name Immanuel;" Which is, being interpreted, "God with us."

Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe; Mathayo 1:24

Joseph arose from his sleep, and did as the angel of the Lord commanded him, and took his wife to himself;

asimjue kamwe hata alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake YESU. Mathayo 1:25

and didn't know her sexually until she had brought forth her firstborn son. He named him Jesus.