Mathayo 6 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mathayo 6 (Swahili) Matthew 6 (English)

Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni. Mathayo 6:1

"Be careful that you don't do your charitable giving before men, to be seen by them, or else you have no reward from your Father who is in heaven.

Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu. Mathayo 6:2

Therefore when you do merciful deeds, don't sound a trumpet before yourself, as the hypocrites do in the synagogues and in the streets, that they may get glory from men. Most assuredly I tell you, they have received their reward.

Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; Mathayo 6:3

But when you do merciful deeds, don't let your left hand know what your right hand does,

sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. Mathayo 6:4

so that your merciful deeds may be in secret, then your Father who sees in secret will reward you openly.

Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. Mathayo 6:5

"When you pray, you shall not be as the hypocrites, for they love to stand and pray in the synagogues and in the corners of the streets, that they may be seen by men. Most assuredly, I tell you, they have received their reward.

Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. Mathayo 6:6

But you, when you pray, enter into your inner chamber, and having shut your door, pray to your Father who is in secret, and your Father who sees in secret will reward you openly.

Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. Mathayo 6:7

In praying, don't use vain repetitions, as the Gentiles do; for they think that they will be heard for their much speaking.

Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. Mathayo 6:8

Therefore don't be like them, for your Father knows what things you need, before you ask him.

Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, Mathayo 6:9

Pray like this: 'Our Father in heaven, may your name be kept holy.

Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Mathayo 6:10

Let your Kingdom come. Let your will be done, as in heaven, so on earth.

Utupe leo riziki yetu. Mathayo 6:11

Give us today our daily bread.

Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Mathayo 6:12

Forgive us our debts, as we also forgive our debtors.

Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.] Mathayo 6:13

Bring us not into temptation, but deliver us from the evil one. For yours is the Kingdom, the power, and the glory forever. Amen.'

Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Mathayo 6:14

"For if you forgive men their trespasses, your heavenly Father will also forgive you.

Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu. Mathayo 6:15

But if you don't forgive men their trespasses, neither will your Father forgive your trespasses.

Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. Mathayo 6:16

"Moreover when you fast, don't be like the hypocrites, with sad faces. For they disfigure their faces, that they may be seen by men to be fasting. Most assuredly I tell you, they have received their reward.

Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; Mathayo 6:17

But you, when you fast, anoint your head, and wash your face;

ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. Mathayo 6:18

so that you are not seen by men to be fasting, but by your Father who is in secret, and your Father, who sees in secret, will reward you.

Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; Mathayo 6:19

"Don't lay up treasures for yourselves on the earth, where moth and rust consume, and where thieves break through and steal;

bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; Mathayo 6:20

but lay up for yourselves treasures in heaven, where neither moth nor rust consume, and where thieves don't break through and steal;

kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako. Mathayo 6:21

for where your treasure is, there your heart will be also.

Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru. Mathayo 6:22

"The lamp of the body is the eye. If therefore your eye is sound, your whole body will be full of light.

Lakini jicho lako likiwa bovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Basi ile nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza; si giza hilo! Mathayo 6:23

But if your eye is evil, your whole body will be full of darkness. If therefore the light that is in you is darkness, how great is the darkness!

Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali. Mathayo 6:24

"No one can serve two masters, for either he will hate the one and love the other; or else he will be devoted to one and despise the other. You can't serve both God and Mammon.

Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? Mathayo 6:25

Therefore, I tell you, don't be anxious for your life: what you will eat, or what you will drink; nor yet for your body, what you will wear. Isn't life more than food, and the body more than clothing?

Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao? Mathayo 6:26

See the birds of the sky, that they don't sow, neither do they reap, nor gather into barns. Your heavenly Father feeds them. Aren't you of much more value than they?

Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja? Mathayo 6:27

"Which of you, by being anxious, can add one cubit to the measure of his life?

Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti Mathayo 6:28

Why are you anxious about clothing? Consider the lilies of the field, how they grow. They don't toil, neither do they spin,

nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo. Mathayo 6:29

yet I tell you that even Solomon in all his glory was not dressed like one of these.

Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba? Mathayo 6:30

But if God so clothes the grass of the field, which today exists, and tomorrow is thrown into the oven, won't he much more clothe you, you of little faith?

Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? Mathayo 6:31

"Therefore don't be anxious, saying, 'What will we eat?', 'What will we drink?' or, 'With what will we be clothed?'

Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Mathayo 6:32

For the Gentiles seek after all these things, for your heavenly Father knows that you need all these things.

Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. Mathayo 6:33

But seek first God's Kingdom, and his righteousness; and all these things will be given to you as well.

Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake. Mathayo 6:34

Therefore don't be anxious for tomorrow, for tomorrow will be anxious for itself. Each day's own evil is sufficient.