Mathayo 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mathayo 5 (Swahili) Matthew 5 (English)

Naye alipowaona makutano, alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake walimjia; Mathayo 5:1

Seeing the multitudes, he went up onto the mountain. When he had sat down, his disciples came to him.

akafumbua kinywa chake, akawafundisha, akisema, Mathayo 5:2

He opened his mouth and taught them, saying,

Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. Mathayo 5:3

"Blessed are the poor in spirit, For theirs is the Kingdom of Heaven.

Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika. Mathayo 5:4

Blessed are those who mourn, For they shall be comforted.

Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi. Mathayo 5:5

Blessed are the gentle, For they shall inherit the earth.

Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa. Mathayo 5:6

Blessed are those who hunger and thirst after righteousness, For they shall be filled.

Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema. Mathayo 5:7

Blessed are the merciful, For they shall obtain mercy.

Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu. Mathayo 5:8

Blessed are the pure in heart, For they shall see God.

Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu. Mathayo 5:9

Blessed are the peacemakers, For they shall be called children of God.

Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. Mathayo 5:10

Blessed are those who have been persecuted for righteousness' sake, For theirs is the Kingdom of Heaven.

Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. Mathayo 5:11

"Blessed are you when people reproach you, persecute you, and say all kinds of evil against you falsely, for my sake.

Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu. Mathayo 5:12

Rejoice, and be exceedingly glad, for great is your reward in heaven. For that is how they persecuted the prophets who were before you.

Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu. Mathayo 5:13

"You are the salt of the earth, but if the salt has lost its flavor, with what will it be salted? It is then good for nothing, but to be cast out and trodden under the feet of men.

Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. Mathayo 5:14

You are the light of the world. A city located on a hill can't be hidden.

Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Mathayo 5:15

Neither do you light a lamp, and put it under a measuring basket, but on a stand; and it shines to all who are in the house.

Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni. Mathayo 5:16

Even so, let your light shine before men; that they may see your good works, and glorify your Father who is in heaven.

Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Mathayo 5:17

"Don't think that I came to destroy the law or the prophets. I didn't come to destroy, but to fulfill.

Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie. Mathayo 5:18

For most assuredly, I tell you, until heaven and earth pass away, not even one smallest letter{literally, iota} or one tiny pen stroke{or, serif} shall in any way pass away from the law, until all things are accomplished.

Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. Mathayo 5:19

Whoever, therefore, shall break one of these least commandments, and teach others to do so, shall be called least in the Kingdom of Heaven; but whoever shall do and teach them shall be called great in the Kingdom of Heaven.

Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. Mathayo 5:20

For I tell you that unless your righteousness exceeds that of the scribes and Pharisees, there is no way you will enter into the Kingdom of Heaven.

Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu. Mathayo 5:21

"You have heard that it was said to the ancient ones, 'You shall not murder;' and 'Whoever shall murder shall be in danger of the judgment.'

Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto. Mathayo 5:22

But I tell you, that everyone who is angry with his brother without a cause shall be in danger of the judgment; and whoever shall say to his brother, 'Raca{"Raca" is an Aramaic insult, related to the word for "empty" and conveying the idea of empty-headedness.}!' shall be in danger of the council; and whoever shall say, 'You fool!' shall be in danger of the fire of Gehenna{Gehenna is another name for Hell that brings to mind an image of a burning garbage dump with dead bodies in it.}.

Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, Mathayo 5:23

"If therefore you are offering your gift at the altar, and there remember that your brother has anything against you,

iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako. Mathayo 5:24

leave your gift there before the altar, and go your way. First be reconciled to your brother, and then come and offer your gift.

Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani. Mathayo 5:25

Agree with your adversary quickly, while you are with him in the way; lest perhaps the prosecutor deliver you to the judge, and the judge deliver you to the officer, and you be cast into prison.

Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho. Mathayo 5:26

Most assuredly I tell you, you shall by no means get out of there, until you have paid the last penny.{Literally, kodrantes. A kodrantes was a small copper coin worth about 2 lepta (widow's mites)--not enough to buy very much of anything.}

Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; Mathayo 5:27

"You have heard that it was said, {TR adds "to the ancients,"} 'You shall not commit adultery;'

lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. Mathayo 5:28

but I tell you that everyone who gazes at a woman to lust after her has committed adultery with her already in his heart.

Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. Mathayo 5:29

If your right eye causes you to stumble, pluck it out and throw it away from you. For it is more profitable for you that one of your members should perish, than for your whole body to be cast into Gehenna.

Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. Mathayo 5:30

If your right hand causes you to stumble, cut it off, and throw it away from you: for it is profitable for you that one of your members should perish, and not your whole body be thrown into Gehenna.

Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka; Mathayo 5:31

"It was also said, 'Whoever shall put away his wife, let him give her a writing of divorce,'

lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini. Mathayo 5:32

but I tell you that whoever puts away his wife, except for the cause of sexual immorality, makes her an adulteress; and whoever marries her when she is put away commits adultery.

Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako; Mathayo 5:33

"Again you have heard that it was said to them of old time, 'You shall not make false vows, but shall perform to the Lord your vows,'

lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu; Mathayo 5:34

but I tell you, don't swear at all: neither by heaven, for it is the throne of God;

wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu. Mathayo 5:35

nor by the earth, for it is the footstool of his feet; nor by Jerusalem, for it is the city of the great King.

Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. Mathayo 5:36

Neither shall you swear by your head, for you can't make one hair white or black.

Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu. Mathayo 5:37

But let your 'Yes' be 'Yes' and your 'No' be 'no.' Whatever is more than these is of the evil one.

Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino; Mathayo 5:38

"You have heard that it was said, 'An eye for an eye, and a tooth for a tooth.'

Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili. Mathayo 5:39

But I tell you, don't resist him who is evil; but whoever strikes you on your right cheek, turn to him the other also.

Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia. Mathayo 5:40

If anyone sues you to take away your coat, let him have your cloak also.

Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili. Mathayo 5:41

Whoever compels you to go one mile, go with him two.

Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo. Mathayo 5:42

Give to him who asks you, and don't turn away him who desires to borrow from you.

Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; Mathayo 5:43

"You have heard that it was said, 'You shall love your neighbor, and hate your enemy.'

lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, Mathayo 5:44

But I tell you, love your enemies, bless those who curse you, do good to those who hate you, and pray for those who mistreat you and persecute you,

ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. Mathayo 5:45

that you may be children of your Father who is in heaven. For he makes his sun to rise on the evil and the good, and sends rain on the just and the unjust.

Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo? Mathayo 5:46

For if you love those who love you, what reward do you have? Don't even the tax collectors do the same?

Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo? Mathayo 5:47

If you only greet your friends, what more do you do than others? Don't even the tax collectors do the same?

Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu. Mathayo 5:48

Therefore you shall be perfect, just as your Father in heaven is perfect.