Mathayo 9 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mathayo 9 (Swahili) Matthew 9 (English)

Akapanda chomboni, akavuka, akafika mjini kwao. Mathayo 9:1

He entered into a boat, and crossed over, and came into his own city.

Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako. Mathayo 9:2

Behold, they brought to him a man who was paralyzed, lying on a bed. Jesus, seeing their faith, said to the paralytic, "Son, cheer up! Your sins are forgiven you."

Na tazama, baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru. Mathayo 9:3

Behold, some of the scribes said to themselves, "This man blasphemes."

Naye Yesu, hali akijua mawazo yao, akasema, Mbona mnawaza maovu mioyoni mwenu? Mathayo 9:4

Jesus, knowing their thoughts, said, "Why do you think evil in your hearts?

Kwa maana rahisi ni lipi, ni kusema, Umesamehewa dhambi zako, au ni kusema, Ondoka, uende? Mathayo 9:5

For which is easier, to say, 'Your sins are forgiven;' or to say, 'Get up, and walk?'

Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (amwambia yule mwenye kupooza) Ondoka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwako. Mathayo 9:6

But that you may know that the Son of Man has authority on earth to forgive sins..." (then he said to the paralytic), "Get up, and take up your mat, and go up to your house."

Akaondoka, akaenda zake nyumbani kwake. Mathayo 9:7

He arose and departed to his house.

Makutano walipomwona, walishikwa na hofu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu amri ya namna hii. Mathayo 9:8

But when the multitudes saw it, they marveled and glorified God, who had given such authority to men.

Naye Yesu alipokuwa akipita kutoka huko aliona mtu ameketi forodhani, aitwaye Mathayo, akamwambia, Nifuate. Akaondoka, akamfuata. Mathayo 9:9

As Jesus passed by from there, he saw a man called Matthew sitting at the tax collection office. He said to him, "Follow me." He got up and followed him.

Ikawa alipoketi nyumbani ale chakula, tazama, watoza ushuru wengi na wenye dhambi walikuja wakaketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake. Mathayo 9:10

It happened as he sat in the house, behold, many tax collectors and sinners came and sat down with Jesus and his disciples.

Mafarisayo walipoona, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? Mathayo 9:11

When the Pharisees saw it, they said to his disciples, "Why does your teacher eat with tax collectors and sinners?"

Naye aliposikia, aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi. Mathayo 9:12

When Jesus heard it, he said to them, "Those who are healthy have no need for a physician, but those who are sick do.

Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi. Mathayo 9:13

But you go and learn what this means: 'I desire mercy, and not sacrifice,' for I came not to call the righteous, but sinners to repentance."

Wakati ule wanafunzi wake Yohana wakamwendea, wakasema, Kwa nini sisi na Mafarisayo twafunga, bali wanafunzi wako hawafungi? Mathayo 9:14

Then John's disciples came to him, saying, "Why do we and the Pharisees fast often, but your disciples don't fast?"

Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kuomboleza, muda bwana arusi akiwapo pamoja nao? Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi; ndipo watakapofunga. Mathayo 9:15

Jesus said to them, "Can the friends of the bridegroom mourn, as long as the bridegroom is with them? But the days will come when the bridegroom will be taken away from them, and then they will fast.

Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; maana kile kilichotiwa huondoa kipande cha lile vazi, na pale palipotatuka huzidi. Mathayo 9:16

No one puts a piece of unshrunk cloth on an old garment; for the patch would tear away from the garment, and a worse hole is made.

Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu; na kama wakitia, vile viriba hupasuka, divai ikamwagika, na viriba vikaharibika; bali hutia divai mpya katika viriba vipya, vikahifadhika vyote. Mathayo 9:17

Neither do people put new wine into old wineskins, or else the skins would burst, and the wine be spilled, and the skins ruined. No, they put new wine into fresh wineskins, and both are preserved."

Alipokuwa akiwaambia hayo, tazama, akaja jumbe mmoja, akamsujudia, akisema, Binti yangu sasa hivi amekufa; lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, naye ataishi. Mathayo 9:18

While he told these things to them, behold, a ruler came and worshiped him, saying, "My daughter has just died, but come and lay your hand on her, and she will live."

Akaondoka Yesu, akamfuata, pamoja na wanafunzi wake. Mathayo 9:19

Jesus got up and followed him, as did his disciples.

Na tazama, mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuja kwa nyuma, akaugusa upindo wa vazi lake. Mathayo 9:20

Behold, a woman who had an issue of blood for twelve years came behind him, and touched the tassels of his garment;

Kwa maana alisema moyoni mwake, Nikigusa tu upindo wa vazi lake nitapona. Mathayo 9:21

for she said within herself, "If I just touch his garment, I will be made well."

Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu; imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile. Mathayo 9:22

But Jesus, turning around and seeing her, said, "Daughter, cheer up! Your faith has made you well." And the woman was made well from that hour.

Yesu alipofika nyumbani kwa yule jumbe, aliona wapiga filimbi, na makutano wakifanya maombolezo, Mathayo 9:23

When Jesus came into the ruler's house, and saw the flute players, and the crowd in noisy disorder,

akawaambia, Ondokeni; kwa maana kijana hakufa, amelala tu. Wakamcheka sana. Mathayo 9:24

he said to them, "Make room, because the girl isn't dead, but sleeping." They were ridiculing him.

Lakini makutano walipoondoshwa, aliingia, akamshika mkono; yule kijana akasimama. Mathayo 9:25

But when the crowd was put out, he entered in, took her by the hand, and the girl arose.

Zikaenea habari hizi katika nchi ile yote. Mathayo 9:26

The report of this went out into all that land.

Yesu alipokuwa akipita kutoka huko, vipofu wawili wakamfuata wakipaza sauti, wakisema, Uturehemu, Mwana wa Daudi. Mathayo 9:27

As Jesus passed by from there, two blind men followed him, calling out and saying, "Have mercy on us, son of David!"

Naye alipofika nyumbani, wale vipofu walimwendea; Yesu akawaambia, Mnaamini kwamba naweza kufanya hili? Wakamwambia, Naam, Bwana. Mathayo 9:28

When he had come into the house, the blind men came to him. Jesus said to them, "Do you believe that I am able to do this?" They told him, "Yes, Lord."

Ndipo alipowagusa macho, akasema, Kwa kadiri ya imani yenu mpate. Mathayo 9:29

Then he touched their eyes, saying, "According to your faith be it done to you."

Macho yao yakafumbuka. Naye Yesu akawaagiza kwa nguvu, akisema, Angalieni hata mtu mmoja asijue. Mathayo 9:30

Their eyes were opened. Jesus strictly charged them, saying, "See that no one knows about this."

Lakini wakatoka, wakaeneza habari zake katika nchi ile yote. Mathayo 9:31

But they went out and spread abroad his fame in all that land.

Hata hao walipokuwa wakitoka, tazama, walimletea mtu bubu mwenye pepo. Mathayo 9:32

As they went out, behold, a mute man who was demon possessed was brought to him.

Na pepo alipotolewa, yule bubu alinena, makutano wakastajabu, wakasema, Haijaonekana hivi katika Israeli wakati wo wote. Mathayo 9:33

When the demon was cast out, the mute man spoke. The multitudes marveled, saying, "Nothing like this has ever been seen in Israel!"

Lakini Mafarisayo wakasema, Kwa nguvu za mkuu wa pepo atoa pepo. Mathayo 9:34

But the Pharisees said, "By the prince of the demons, he casts out demons."

Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Mathayo 9:35

Jesus went about all the cities and the villages, teaching in their synagogues, and preaching the Gospel of the Kingdom, and healing every disease and every sickness among the people.

Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji. Mathayo 9:36

But when he saw the multitudes, he was moved with compassion for them, because they were harassed{TR reads "weary" instead of "harassed"} and scattered, like sheep without a shepherd.

Ndipo alipowaambia wanafunzi wake, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Mathayo 9:37

Then he said to his disciples, "The harvest indeed is plentiful, but the laborers are few.

Basi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake. Mathayo 9:38

Pray therefore that the Lord of the harvest will send out laborers into his harvest."