Mathayo 16 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mathayo 16 (Swahili) Matthew 16 (English)

Wakamjia Mafarisayo na Masadukayo, wakamjaribu, wakamwomba awaonyeshe ishara itokayo mbinguni. Mathayo 16:1

The Pharisees and Sadducees came, and testing him, asked him to show them a sign from heaven.

Akajibu, akawaambia, [Kukiwa jioni, mwasema, Kutakuwa na kianga; kwa maana mbingu ni nyekundu. Mathayo 16:2

But he answered them, "When it is evening, you say, 'It will be fair weather, for the sky is red.'

Na asubuhi, mwasema, Leo kutakuwa na dhoruba; kwa maana mbingu ni nyekundu, tena kumetanda. Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa mbingu; lakini, je! Ishara za zamani hizi hamwezi kuzitambua?] Mathayo 16:3

In the morning, 'It will be foul weather today, for the sky is red and threatening.' Hypocrites! You know how to discern the appearance of the sky, but you can't discern the signs of the times!

Kizazi kibaya na cha zinaa chataka ishara; wala hakitapewa ishara, isipokuwa ishara ya Yona. Akawaacha, akaenda zake. Mathayo 16:4

An evil and adulterous generation seeks after a sign, and there will be no sign given to it, except the sign of the prophet Jonah." He left them, and departed.

Nao wanafunzi wakaenda hata ng'ambo, wakasahau kuchukua mikate. Mathayo 16:5

The disciples came to the other side and had forgotten to take bread.

Yesu akawaambia, Angalieni, jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo. Mathayo 16:6

Jesus said to them, "Take heed and beware of the yeast of the Pharisees and Sadducees."

Wakabishana wao kwa wao, wakisema, Ni kwa sababu hatukuchukua mikate. Mathayo 16:7

They reasoned among themselves, saying, "We brought no bread."

Naye Yesu akafahamu, akawaambia, Mbona mnabishana ninyi kwa ninyi, enyi wa imani chache, kwa sababu hamna mikate? Mathayo 16:8

Jesus, perceiving it, said, "Why do you reason among yourselves, you of little faith, 'because you have brought no bread?'

Hamjafahamu bado, wala hamkumbuki ile mikate mitano kwa wale elfu tano, na vikapu vingapi mlivyoviokota? Mathayo 16:9

Don't you yet perceive, neither remember the five loaves for the five thousand, and how many baskets you took up?

Wala ile mikate saba kwa watu elfu nne, na makanda mangapi mliyoyaokota? Mathayo 16:10

Nor the seven loaves for the four thousand, and how many baskets you took up?

Imekuwaje hamkufahamu ya kuwa si kwa sababu ya mkate naliwaambia? Ila jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo. Mathayo 16:11

How is it that you don't perceive that I didn't speak to you concerning bread? But beware of the yeast of the Pharisees and Sadducees."

Ndipo walipofahamu ya kuwa hakuwaambia kujilinda na chachu ya mkate, bali na mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo. Mathayo 16:12

Then they understood that he didn't tell them to beware of the yeast of bread, but of the teaching of the Pharisees and Sadducees.

Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani? Mathayo 16:13

Now when Jesus came into the parts of Caesarea Philippi, he asked his disciples, saying, "Who do men say that I, the Son of Man, am?"

Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. Mathayo 16:14

They said, "Some say John the Baptizer, some, Elijah, and others, Jeremiah, or one of the prophets."

Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? Mathayo 16:15

He said to them, "But who do you say that I am?"

Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Mathayo 16:16

Simon Peter answered, "You are the Christ, the Son of the living God."

Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. Mathayo 16:17

Jesus answered him, "Blessed are you, Simon Bar Jonah, for flesh and blood has not revealed this to you, but my Father who is in heaven.

Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Mathayo 16:18

I also tell you that you are Peter,{Peter's name, Petros in Greek, is the word for a specific rock or stone.} and on this rock{Greek, petra, a rock mass or bedrock.} I will build my assembly, and the gates of Hades will not prevail against it.

Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni. Mathayo 16:19

I will give to you the keys of the Kingdom of Heaven, and whatever you bind on earth will be bound in heaven; and whatever you release on earth will be released in heaven."

Ndipo alipowakataza sana wanafunzi wake wasimwambie mtu ye yote ya kwamba yeye ndiye Kristo. Mathayo 16:20

Then he charged the disciples that they should tell no one that he is Jesus the Christ.

Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka. Mathayo 16:21

From that time, Jesus began to show his disciples that he must go to Jerusalem and suffer many things from the elders, chief priests, and scribes, and be killed, and the third day be raised up.

Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata. Mathayo 16:22

Peter took him aside, and began to rebuke him, saying, "Far be it from you, Lord! This will never be done to you."

Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu. Mathayo 16:23

But he turned, and said to Peter, "Get behind me, Satan! You are a stumbling-block to me, for you are not setting your mind on the things of God, but on the things of men."

Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Mathayo 16:24

Then Jesus said to his disciples, "If anyone desires to come after me, let him deny himself, and take up his cross, and follow me.

Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. Mathayo 16:25

For whoever desires to save his life will lose it, and whoever will lose his life for my sake will find it.

Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? Mathayo 16:26

For what will it profit a man, if he gains the whole world, and forfeits his life? Or what will a man give in exchange for his life?

Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. Mathayo 16:27

For the Son of Man will come in the glory of his Father with his angels, and then he will render to everyone according to his deeds.

Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake. Mathayo 16:28

Most assuredly I tell you, there are some standing here who will in no way taste of death, until they see the Son of Man coming in his Kingdom."