Mathayo 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mathayo 3 (Swahili) Matthew 3 (English)

Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema, Mathayo 3:1

In those days, John the Baptizer came, preaching in the wilderness of Judea, saying,

Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. Mathayo 3:2

"Repent, for the Kingdom of Heaven is at hand!"

Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake. Mathayo 3:3

For this is he who was spoken of by Isaiah the prophet, saying, "The voice of one crying in the wilderness, Make ready the way of the Lord, Make his paths straight."

Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu. Mathayo 3:4

Now John himself wore clothing made of camel's hair, with a leather belt around his waist. His food was locusts and wild honey.

Ndipo walipomwendea Yerusalemu, na Uyahudi wote, na nchi zote za kandokando ya Yordani; Mathayo 3:5

Then people from Jerusalem, all of Judea, and all the region around the Jordan went out to him.

naye akawabatiza katika mto wa Yordani, huku wakiziungama dhambi zao. Mathayo 3:6

They were baptized by him in the Jordan, confessing their sins.

Hata alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja? Mathayo 3:7

But when he saw many of the Pharisees and Sadducees coming for his baptism, he said to them, "You offspring of vipers, who warned you to flee from the wrath to come?

Basi zaeni matunda yapasayo toba; Mathayo 3:8

Therefore bring forth fruit worthy of repentance!

wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto. Mathayo 3:9

Don't think to yourselves, 'We have Abraham for our father,' for I tell you that God is able to raise up children to Abraham from these stones.

Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni. Mathayo 3:10

"Even now the axe lies at the root of the trees. Therefore, every tree that doesn't bring forth good fruit is cut down, and cast into the fire.

Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. Mathayo 3:11

I indeed baptize you in water for repentance, but he who comes after me is mightier than I, whose shoes I am not worthy to carry. He will baptize you in the Holy Spirit.{TR and NU add "and with fire"}

Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika. Mathayo 3:12

His winnowing fork is in his hand, and he will thoroughly cleanse his threshing floor. He will gather his wheat into the barn, but the chaff he will burn up with unquenchable fire."

Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Mathayo 3:13

Then Jesus came from Galilee to the Jordan to John, to be baptized by him.

Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Mathayo 3:14

But John would have hindered him, saying, "I need to be baptized by you, and you come to me?"

Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali. Mathayo 3:15

But Jesus, answering, said to him, "Allow it now, for this is the fitting way for us to fulfill all righteousness." Then he allowed him.

Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; Mathayo 3:16

Jesus, when he was baptized, went up directly from the water: and behold, the heavens were opened to him. He saw the Spirit of God descending as a dove, and coming on him.

na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye. Mathayo 3:17

Behold, a voice out of the heavens said, "This is my beloved Son, with whom I am well pleased."