Mathayo 14 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mathayo 14 (Swahili) Matthew 14 (English)

Wakati ule mfalme Herode alisikia habari za Yesu, akawaambia watumishi wake, Mathayo 14:1

At that time, Herod the tetrarch heard the report concerning Jesus,

Huyo ndiye Yohana Mbatizaji; amefufuka katika wafu; na kwa hiyo nguvu hizo zinatenda kazi ndani yake. Mathayo 14:2

and said to his servants, "This is John the Baptizer. He is risen from the dead. That is why these powers work in him."

Maana Herode alikuwa amemkamata Yohana, akamfunga, akamtia gerezani, kwa ajili ya Herodia, mke wa Filipo nduguye. Mathayo 14:3

For Herod had laid hold of John, and bound him, and put him in prison for the sake of Herodias, his brother Philip's wife.

Kwa sababu Yohana alimwambia, Si halali kwako kuwa naye. Mathayo 14:4

For John said to him, "It is not lawful for you to have her."

Naye alipotaka kumwua, aliwaogopa watu, maana walimwona Yohana kuwa nabii. Mathayo 14:5

When he would have put him to death, he feared the multitude, because they counted him as a prophet.

Hata ilipofika sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti Herodia alicheza mbele ya watu, akampendeza Herode. Mathayo 14:6

But when Herod's birthday came, the daughter of Herodias danced among them and pleased Herod.

Hata akaahidi kwa kiapo ya kwamba atampa lo lote atakaloliomba. Mathayo 14:7

Whereupon he promised with an oath to give her whatever she should ask.

Naye, huku akichochewa na mamaye, akasema, Nipe hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji. Mathayo 14:8

She, being prompted by her mother, said, "Give me here on a platter the head of John the Baptizer."

Naye mfalme akasikitika; lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya wale walioketi chakulani pamoja naye, akaamuru apewe; Mathayo 14:9

The king was grieved, but for the sake of his oaths, and of those who sat at the table with him, he commanded it to be given,

akatuma mtu, akamkata kichwa Yohana mle gerezani. Mathayo 14:10

and he sent and beheaded John in the prison.

Kichwa chake kikaletwa katika kombe, akapewa yule kijana; akakichukua kwa mamaye. Mathayo 14:11

His head was brought on a platter, and given to the young lady: and she brought it to her mother.

Wanafunzi wake wakaenda, wakamchukua yule maiti, wakamzika; kisha wakaenda wakampasha Yesu habari. Mathayo 14:12

His disciples came, and took the body, and buried it; and they went and told Jesus.

Naye Yesu aliposikia; hayo, aliondoka huko katika chombo, akaenda mahali pasipo watu, faraghani. Na makutano waliposikia, walimfuata kwa miguu kutoka mijini mwao. Mathayo 14:13

Now when Jesus heard this, he withdrew from there in a boat, to a deserted place apart. When the multitudes heard it, they followed him on foot from the cities.

Yesu akatoka, akaona mkutano mkuu, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao. Mathayo 14:14

Jesus went out, and he saw a great multitude. He had compassion on them, and healed their sick.

Hata kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na saa imekwisha pita; uwaage makutano, waende zao vijijini, wakajinunulie vyakula. Mathayo 14:15

When evening had come, his disciples came to him, saying, "This place is deserted, and the hour is already late. Send the multitudes away, that they may go into the villages, and buy themselves food."

Yesu akawaambia, Hawana haja kwenda zao, wapeni ninyi vyakula. Mathayo 14:16

But Jesus said to them, "They don't need to go away. You give them something to eat."

Wakamwambia, Hamna kitu hapa ila mikate mitano na samaki wawili. Mathayo 14:17

They told him, "We only have here five loaves and two fish."

Akasema, Nileteeni hapa. Mathayo 14:18

He said, "Bring them here to me."

Akawaagiza makutano waketi katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi, wanafunzi wakawapa makutano. Mathayo 14:19

He commanded the multitudes to sit down on the grass; and he took the five loaves and the two fish, and looking up to heaven, he blessed, broke and gave the loaves to the disciples, and the disciples gave to the multitudes.

Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate, vikapu kumi na viwili, vimejaa. Mathayo 14:20

They all ate, and were filled. They took up twelve baskets full of that which remained left over from the broken pieces.

Nao waliokula walikuwa wanaume wapata elfu tano, bila wanawake na watoto. Mathayo 14:21

Those who ate were about five thousand men, besides women and children.

Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ng'ambo, wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano. Mathayo 14:22

Immediately Jesus made the disciples get into the boat, and to go ahead of him to the other side, while he sent the multitudes away.

Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake. Mathayo 14:23

After he had sent the multitudes away, he went up into the mountain by himself to pray. When evening had come, he was there alone.

Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi; maana upepo ulikuwa wa mbisho. Mathayo 14:24

But the boat was now in the middle of the sea, distressed by the waves, for the wind was contrary.

Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari. Mathayo 14:25

In the fourth watch of the night,{The night was equally divided into four watches, so the fourth watch is approximately 3:00 A. M. to sunrise.} Jesus came to them, walking on the sea.

Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu. Mathayo 14:26

When the disciples saw him walking on the sea, they were troubled, saying, "It's a ghost!" and they cried out for fear.

Mara Yesu alinena, akawaambia, Jipeni moyo ni mimi; msiogope. Mathayo 14:27

But immediately Jesus spoke to them, saying "Cheer up! I AM!{see Exodus 3:14.} Don't be afraid."

Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji. Mathayo 14:28

Peter answered him and said, "Lord, if it is you, command me to come to you on the waters."

Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu. Mathayo 14:29

He said, "Come!" Peter stepped down from the boat, and walked on the waters to come to Jesus.

Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe. Mathayo 14:30

But when he saw that the wind was strong, he was afraid, and beginning to sink, he cried out, saying, "Lord, save me!"

Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka? Mathayo 14:31

Immediately Jesus stretched out his hand, took hold of him, and said to him, "You of little faith, why did you doubt?"

Nao walipopanda chomboni, upepo ulikoma. Mathayo 14:32

When they got up into the boat, the wind ceased.

Nao waliokuwamo ndani ya chombo wakamsujudia, wakisema, Hakika wewe u Mwana wa Mungu. Mathayo 14:33

Those who were in the boat came and worshiped him, saying, "You are truly the Son of God!"

Na walipokwisha kuvuka, walifika nchi ya Genesareti. Mathayo 14:34

When they had crossed over, they came to the land of Gennesaret.

Na watu wa mahali pale walipomtambua, walituma watu kwenda nchi zile zilizo kandokando, wakamletea wote waliokuwa hawawezi; Mathayo 14:35

When the men of that place recognized him, they sent into all that surrounding region, and brought to him all who were sick,

nao wakamsihi waguse hata pindo la vazi lake tu; na wote waliogusa wakaponywa kabisa. Mathayo 14:36

and they begged him that they might just touch the fringe of his garment. As many as touched it were made whole.