1 Samweli 31 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Samweli 31 (Swahili) 1st Samuel 31 (English)

Basi Wafilisti wakapigana na Israeli; nao watu wa Israeli wakakimbia mbele ya Wafilisti, wakaanguka wameuawa katika mlima wa Gilboa. 1 Samweli 31:1

Now the Philistines fought against Israel: and the men of Israel fled from before the Philistines, and fell down slain on Mount Gilboa.

Wafilisti wakamfuatia sana Sauli na wanawe, Wafilisti wakawaua Yonathani, na Abinadabu, na Malkishua, wana wa Sauli. 1 Samweli 31:2

The Philistines followed hard on Saul and on his sons; and the Philistines killed Jonathan, and Abinadab, and Malchishua, the sons of Saul.

Tena vita vilikuwa vikali sana juu ya Sauli, na wapiga upinde wakampata; hata akafadhaika sana kwa sababu ya wapiga upinde. 1 Samweli 31:3

The battle went sore against Saul, and the archers overtook him; and he was greatly distressed by reason of the archers.

Ndipo Sauli akamwambia yule mchukua silaha zake, Futa upanga wako, unichome nao; wasije watu hawa wasiotahiriwa wakanichoma, na kunisimanga. Lakini huyo mchukua silaha zake akakataa; kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli akautwaa upanga wake, akauangukia. 1 Samweli 31:4

Then said Saul to his armor bearer, Draw your sword, and thrust me through therewith, lest these uncircumcised come and thrust me through, and abuse me. But his armor bearer would not; for he was sore afraid. Therefore Saul took his sword, and fell on it.

Na mchukua silaha zake alipoona ya kuwa Sauli amekufa, yeye naye akauangukia upanga wake, akafa pamoja naye. 1 Samweli 31:5

When his armor bearer saw that Saul was dead, he likewise fell on his sword, and died with him.

Hivyo Sauli akafa, na wanawe watatu, na mchukua silaha zake, na watu wake wote pamoja siku iyo hiyo. 1 Samweli 31:6

So Saul died, and his three sons, and his armor bearer, and all his men, that same day together.

Kisha watu wa Israeli waliokuwa upande wa pili wa bonde lile, na ng'ambo ya Yordani, walipoona ya kuwa watu wa Israeli wamekimbia, na ya kuwa Sauli na wanawe wamekufa, wakaiacha miji yao, wakakimbia; nao Wafilisti wakaenda wakakaa humo. 1 Samweli 31:7

When the men of Israel who were on the other side of the valley, and those who were beyond the Jordan, saw that the men of Israel fled, and that Saul and his sons were dead, they forsook the cities, and fled; and the Philistines came and lived in them.

Hata ikawa, siku ya pili yake, Wafilisti walipokwenda kuwateka nyara waliouawa, walimwona Sauli na wanawe watatu wameanguka juu ya mlima wa Gilboa. 1 Samweli 31:8

It happened on the next day, when the Philistines came to strip the slain, that they found Saul and his three sons fallen on Mount Gilboa.

Wakamkata kichwa, wakamvua silaha zake, wakapeleka wajumbe kwenda nchi ya Wafilisti pande zote, ili kutangaza habari nyumbani mwa sanamu zao, na kwa watu. 1 Samweli 31:9

They cut off his head, and stripped off his armor, and sent into the land of the Philistines round about, to carry the news to the house of their idols, and to the people.

Wakaziweka silaha zake nyumbani mwa Maashtorethi; wakakitundika kiwiliwili chake katika ukuta wa Beth-shani. 1 Samweli 31:10

They put his armor in the house of the Ashtaroth; and they fastened his body to the wall of Beth-shan.

Na wenyeji wa Yabesh-Gileadi waliposikia habari zake, jinsi hao Wafilisti walivyomtenda Sauli, 1 Samweli 31:11

When the inhabitants of Jabesh Gilead heard concerning him that which the Philistines had done to Saul,

wakainuka mashujaa wote, wakaenda usiku kucha, wakautwaa mwili wake Sauli, na miili ya wanawe, na kuiondoa ukutani kwa Beth-shani nao wakaja Yabeshi, na kuiteketeza huko. 1 Samweli 31:12

all the valiant men arose, and went all night, and took the body of Saul and the bodies of his sons from the wall of Beth-shan; and they came to Jabesh, and burnt them there.

Kisha wakaitwaa mifupa yao, na kuizika chini ya mkwaju huko Yabeshi, nao wakafunga siku saba. 1 Samweli 31:13

They took their bones, and buried them under the tamarisk tree in Jabesh, and fasted seven days.