1 Samweli 4 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Samweli 4 (Swahili) 1st Samuel 4 (English)

[Ikawa siku zile Wafilisti walikusanyika ili kupigana na Israeli,] nao Waisraeli wakatoka juu ya Wafilisti kwenda vitani;wakatua karibu na Ebenezeri ,nao Wafilisti wakatua huko Afeki. 1 Samweli 4:1

The word of Samuel came to all Israel. Now Israel went out against the Philistines to battle, and encamped beside Ebenezer: and the Philistines encamped in Aphek.

Nao Wafilisti wakajipanga juu ya Israeli; na walipopigana, Israeli wakapigwa mbele ya Wafilisti; wakauawa watu wa jeshi lao lililokuwa uwandani wapata watu elfu nne. 1 Samweli 4:2

The Philistines put themselves in array against Israel: and when they joined battle, Israel was struck before the Philistines; and they killed of the army in the field about four thousand men.

Hata watu walipofika kambini, wazee wa Israeli wakasema, Mbona Bwana ametupiga leo mbele ya Wafilisti? Twende tukalilete sanduku la agano la Bwana toka Shilo hata huku, lije kati yetu, na kutuokoa katika mikono ya adui zetu. 1 Samweli 4:3

When the people were come into the camp, the elders of Israel said, Why has Yahweh struck us today before the Philistines? Let us get the ark of the covenant of Yahweh out of Shiloh to us, that it may come among us, and save us out of the hand of our enemies.

Basi wakatuma watu kwenda Shilo, nao wakalileta toka huko sanduku la agano la Bwana wa majeshi, akaaye juu ya makerubi; na Hofni na Finehasi, wana wawili wa Eli, walikuwako huko pamoja na sanduku la agano la Mungu. 1 Samweli 4:4

So the people sent to Shiloh; and they brought from there the ark of the covenant of Yahweh of Hosts, who sits [above] the cherubim: and the two sons of Eli, Hophni and Phinehas, were there with the ark of the covenant of God.

Na sanduku la agano la Bwana lilipoingia kambini, Israeli wote wakapiga kelele kwa sauti kuu, hata nchi ikavuma. 1 Samweli 4:5

When the ark of the covenant of Yahweh came into the camp, all Israel shouted with a great shout, so that the earth rang again.

Nao Wafilisti waliposikia mshindo wa zile kelele, walisema, Maana yake nini mshindo wa kelele hizi kubwa katika kambi ya Waebrania? Wakatambua ya kuwa sanduku la Bwana limefika kambini. 1 Samweli 4:6

When the Philistines heard the noise of the shout, they said, What means the noise of this great shout in the camp of the Hebrews? They understood that the ark of Yahweh was come into the camp.

Wafilisti wakaogopa, maana walisema, Mungu ameingia kambini. Wakasema, Ole wetu! Kwani halijawa jambo kama hili tangu hapo. 1 Samweli 4:7

The Philistines were afraid, for they said, God is come into the camp. They said, Woe to us! for there has not been such a thing heretofore.

Ole wetu! Ni nani atakayetuokoa na mkono wa miungu hawa walio hodari? Hawa ndio miungu waliowapiga Wamisri kwa mapigo ya kila namna jangwani. 1 Samweli 4:8

Woe to us! who shall deliver us out of the hand of these mighty gods? these are the gods that struck the Egyptians with all manner of plagues in the wilderness.

Iweni hodari, na kufanya kiume enyi Wafilisti, msije mkawa watumwa wa Waebrania, kama wao walivyokuwa watumwa wenu; fanyeni kiume, mkapigane nao. 1 Samweli 4:9

Be strong, and behave yourselves like men, O you Philistines, that you not be servants to the Hebrews, as they have been to you: quit yourselves like men, and fight.

Wafilisti wakapigana nao, Israeli wakapigwa, wakakimbia kila mtu hemani kwake; wakauawa watu wengi sana; maana katika Israeli walianguka watu thelathini elfu wenye kwenda vitani kwa miguu. 1 Samweli 4:10

The Philistines fought, and Israel was struck, and they fled every man to his tent: and there was a very great slaughter; for there fell of Israel thirty thousand footmen.

Hilo sanduku la Mungu Likatwaliwa; na Hofni na Finehasi, wale wana wawili wa Eli, wakauawa. 1 Samweli 4:11

The ark of God was taken; and the two sons of Eli, Hophni and Phinehas, were slain.

Basi, mtu mmoja wa Benyamini akapiga mbio kutoka mle jeshini akafika Shilo siku ile ile, hali nguo zake zimeraruliwa, na mavumbi kichwani mwake. 1 Samweli 4:12

There ran a man of Benjamin out of the army, and came to Shiloh the same day, with his clothes torn, and with earth on his head.

Alipofika, tazama, Eli alikuwa ameketi kitini pake kando ya njia, akingojea; maana moyo wake ulitetemeka kwa ajili ya sanduku la Mungu. Na yule mtu alipoingia mjini, akatoa habari, mji wote ukalia. 1 Samweli 4:13

When he came, behold, Eli was sitting on his seat by the road watching; for his heart trembled for the ark of God. When the man came into the city, and told it, all the city cried out.

Naye Eli aliposikia kelele za kile kilio, akasema, Maana yake nini kelele za kishindo hiki? Yule mtu akafanya haraka, akaenda, akamwambia Eli. 1 Samweli 4:14

When Eli heard the noise of the crying, he said, What means the noise of this tumult? The man hurried, and came and told Eli.

Basi Eli umri wake umepata miaka tisini na minane; na macho yake yamepofuka hata asiweze kuona. 1 Samweli 4:15

Now Eli was ninety-eight years old; and his eyes were set, so that he could not see.

Yule mtu akamwambia Eli, Mimi ndimi niliyetoka jeshini, nami leo hivi nimekimbia toka jeshini. Naye akasema, Yalikwendaje, mwanangu? 1 Samweli 4:16

The man said to Eli, I am he who came out of the army, and I fled today out of the army. He said, How went the matter, my son?

Yeye aliyeleta habari akajibu, akasema, Israeli wamekimbia mbele ya Wafilisti, tena watu wengi sana wameuawa, hata na wana wako wawili, Hofni na Finehasi, wamekufa pia, na sanduku la Mungu limetwaliwa. 1 Samweli 4:17

He who brought the news answered, Israel is fled before the Philistines, and there has been also a great slaughter among the people, and your two sons also, Hophni and Phinehas, are dead, and the ark of God is taken.

Ikawa alipolitaja sanduku la Mungu, Eli akaanguka kitini pake kwa nyuma, kando ya mlango, shingo yake ikavunjika, akafa; maana alikuwa mzee, tena mzito. Naye alikuwa amewaamua Israeli miaka arobaini. 1 Samweli 4:18

It happened, when he made mention of the ark of God, that [Eli] fell from off his seat backward by the side of the gate; and his neck broke, and he died: for he was an old man, and heavy. He had judged Israel forty years.

Tena mkwewe, mkewe huyo Finehasi, alikuwa mja-mzito, karibu na kuzaa; basi, aliposikia habari ya kutwaliwa sanduku la Mungu, na ya kwamba mkwewe na mumewe wamekufa, akajiinamisha, akazaa; maana utungu wake ulimfikilia. 1 Samweli 4:19

His daughter-in-law, Phinehas' wife, was with child, near to be delivered: and when she heard the news that the ark of God was taken, and that her father-in-law and her husband were dead, she bowed herself and brought forth; for her pains came on her.

Hata alipokuwa katika kufa, wale wanawake waliohudhuria karibu naye wakamwambia, Usiogope; kwa maana umezaa mtoto mwanamume. Walakini hakujibu, wala hakumtazama. 1 Samweli 4:20

About the time of her death the women who stood by her said to her, Don't be afraid; for you have brought forth a son. But she didn't answer, neither did she regard it.

Akamwita mtoto, Ikabodi, akisema, Huo utukufu umeondoka katika Israeli; kwa sababu sanduku la Mungu lilikuwa limetwaliwa, na kwa sababu ya mkwewe na mumewe. 1 Samweli 4:21

She named the child Ichabod, saying, The glory is departed from Israel; because the ark of God was taken, and because of her father-in-law and her husband.

Naam, akasema, Huo utukufu umeondoka katika Israeli; maana sanduku la Mungu limetwaliwa.

1 Samweli 4:22

She said, The glory is departed from Israel; for the ark of God is taken.