1 Samweli 21 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Samweli 21 (Swahili) 1st Samuel 21 (English)

Basi Daudi akaenda Nobu kwa Ahimeleki, kuhani. Ahimeleki akaenda kumlaki Daudi, akitetemeka, akamwambia, Kwani wewe kuwa peke yako, wala hapana mtu pamoja nawe? 1 Samweli 21:1

Then came David to Nob to Ahimelech the priest: and Ahimelech came to meet David trembling, and said to him, Why are you alone, and no man with you?

Daudi akamwambia Ahimeleki, kuhani, Mfalme ameniagiza shughuli, akaniambia, Asijue mtu awaye yote habari ya shughuli hii ninayokutuma, wala ya neno hili ninalokuamuru; nami nimewaagiza vijana waende mahali fulani. 1 Samweli 21:2

David said to Ahimelech the priest, The king has commanded me a business, and has said to me, Let no man know anything of the business about which I send you, and what I have commanded you: and I have appointed the young men to such and such a place.

Kuna nini basi, chini ya mkono wako? Nipe mkononi mwangu mikate mitano, au cho chote ulicho nacho hapa. 1 Samweli 21:3

Now therefore what is under your hand? give me five loaves of bread in my hand, or whatever there is present.

Yule kuhani akamjibu Daudi, akasema, Hapana mikate ya sikuzote chini ya mkono wangu, ila mikate mitakatifu; ikiwa wale vijana wamejitenga na wanawake. 1 Samweli 21:4

The priest answered David, and said, There is no common bread under my hand, but there is holy bread; if only the young men have kept themselves from women.

Naye Daudi akamjibu kuhani, akamwambia, Hakika tumejitenga na wanawake siku hizi tatu; napo nilipotoka, vyombo vya vijana hawa vilikuwa vitakatifu, ingawa ilikuwa safari ya sikuzote; basi leo je! Vyombo vyetu havitakuwa vitakatifu zaidi? 1 Samweli 21:5

David answered the priest, and said to him, Of a truth women have been kept from us about these three days; when I came out, the vessels of the young men were holy, though it was but a common journey; how much more then today shall their vessels be holy?

Ndipo kuhani akampa ile mikate mitakatifu; kwa maana hapakuwa na mikate ila ile ya Wonyesho, nayo imekwisha kuondolewa mbele za Bwana, ili itiwe mikate ya moto siku ile ilipoondolewa. 1 Samweli 21:6

So the priest gave him holy [bread]; for there was no bread there but the show bread, that was taken from before Yahweh, to put hot bread in the day when it was taken away.

Basi siku ile palikuwapo na mtu mmoja wa watumishi wa Sauli, amezuiwa hapo mbele za Bwana jina lake akiitwa Doegi, Mwedomi, mkubwa wa wachungaji wa Sauli. 1 Samweli 21:7

Now a certain man of the servants of Saul was there that day, detained before Yahweh; and his name was Doeg the Edomite, the best of the herdsmen who belonged to Saul.

Tena Daudi akamwambia Ahimeleki, Na hapa chini ya mkono wako, je! Hapana mkuki, au upanga? Kwa maana sikuleta upanga, wala silaha zangu, kwa sababu ile shughuli ya mfalme ilitaka haraka. 1 Samweli 21:8

David said to Ahimelech, Isn't there here under your hand spear or sword? for I have neither brought my sword nor my weapons with me, because the king's business required haste.

Yule kuhani akasema, upanga wa Goliathi, yule Mfilisti, uliyemwua katika bonde la Ela, tazama, upo hapa, umefungwa ndani ya nguo nyuma ya naivera; ukipenda kuuchukua, haya! Uchukue, maana hapa hapana mwingine ila huo tu. Daudi akasema, Hapana mwingine kama ule; haya! Nipe. 1 Samweli 21:9

The priest said, The sword of Goliath the Philistine, whom you killed in the valley of Elah, behold, it is here wrapped in a cloth behind the ephod: if you will take that, take it; for there is no other except that here. David said, There is none like that; give it me.

Basi Daudi akaondoka, akakimbia siku ile, kwa hofu ya Sauli, akamwendea Akishi, mfalme wa Gathi. 1 Samweli 21:10

David arose, and fled that day for fear of Saul, and went to Achish the king of Gath.

Nao watumishi wa Akishi wakamwambia, Je! Huyu siye yule Daudi, mfalme wa nchi? Je! Hawakuimbiana habari zake katika ngoma zao, kusema,Sauli amewaua elfu zake,Na Daudi makumi elfu yake. 1 Samweli 21:11

The servants of Achish said to him, "Isn't this David the king of the land? Didn't they sing one to another about him in dances, saying, 'Saul has slain his thousands, David his ten thousands?'"

Naye Daudi akayatia maneno hayo moyoni mwake, akamwogopa sana Akishi, mfalme wa Gathi. 1 Samweli 21:12

David laid up these words in his heart, and was very afraid of Achish the king of Gath.

Akaubadilisha mwenendo wake mbele yao, akajifanya mwenye wazimu mikononi mwao, akakuna-kuna katika mbao za mlango, na kuyaacha mate yake kuanguka juu ya ndevu zake. 1 Samweli 21:13

He changed his behavior before them, and feigned himself mad in their hands, and scrabbled on the doors of the gate, and let his spittle fall down on his beard.

Ndipo huyo Akishi akawaambia watumishi wake, Angalieni, mwaona ya kuwa mtu huyu ana wazimu; basi, maana yake nini kumleta kwangu? 1 Samweli 21:14

Then said Achish to his servants, Look, you see the man is mad; why then have you brought him to me?

Je! Mimi nina haja ya watu wenye wazimu, hata mmemleta kiumbe hiki ili aonyeshe wazimu wake machoni pangu? Je! Huyu ataingia nyumbani mwangu? 1 Samweli 21:15

Do I lack madmen, that you have brought this fellow to play the madman in my presence? shall this fellow come into my house?