1 Samweli 20 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Samweli 20 (Swahili) 1st Samuel 20 (English)

Kisha Daudi akatoka Nayothi huko Rama, akakimbia, akaenda kwa Yonathani, akasema mbele yake, Nimefanya nini? Uovu wangu ni nini? Dhambi yangu mbele ya baba yako ni nini, hata akaitaka roho yangu? 1 Samweli 20:1

David fled from Naioth in Ramah, and came and said before Jonathan, "What have I done? What is my iniquity?" and "What is my sin before your father, that he seeks my life?"

Naye akamwambia, Hasha! Hutakufa; angalia, baba yangu hatendi neno kubwa wala dogo bila kuifunulia mimi, na baba yangu ana sababu gani ya kunificha jambo hili? Sivyo usemavyo. 1 Samweli 20:2

He said to him, "Far from it; you shall not die: behold, my father does nothing either great or small, but that he discloses it to me; and why should my father hide this thing from me? It is not so."

Daudi akaapa, akasema, Baba yako anajua sana ya kuwa nimeona kibali machoni pako, naye asema, Yonathani asilijue neno hili, asije akahuzunika; lakini ni kweli, aishivyo Bwana, na iishivyo roho yako, iko hatua moja tu kati ya mimi na mauti. 1 Samweli 20:3

David swore moreover, and said, Your father knows well that I have found favor in your eyes; and he says, Don't let Jonathan know this, lest he be grieved: but truly as Yahweh lives, and as your soul lives, there is but a step between me and death.

Ndipo Yonathani akamwambia Daudi, Kadiri roho yako itakavyo, nitakutendea. 1 Samweli 20:4

Then said Jonathan to David, Whatever your soul desires, I will even do it for you.

Naye Daudi akamwambia Yonathani, Tazama, kesho ni mwandamo wa mwezi, nami hainipasi kukosa kuketi chakulani pamoja na mfalme; lakini niache nijifiche bondeni hata siku ya tatu jioni. 1 Samweli 20:5

David said to Jonathan, Behold, tomorrow is the new moon, and I should not fail to sit with the king at meat: but let me go, that I may hide myself in the field to the third day at evening.

Baba yako akiona ya kuwa sipo basi sema, Daudi alitaka sana nimpe ruhusa, aende upesi Bethlehemu, mji wake, kwa maana iko huko dhabihu ya mwaka kwa ajili ya jamaa yake yote. 1 Samweli 20:6

If your father miss me at all, then say, David earnestly asked leave of me that he might run to Bethlehem his city; for it is the yearly sacrifice there for all the family.

Basi, akisema, Ni vema, mimi mtumishi wako nitakuwa na amani; bali akikasirika, ujue ya kuwa amekusudia kutenda jambo baya. 1 Samweli 20:7

If he says, 'It is well;' your servant shall have peace: but if he be angry, then know that evil is determined by him.

Basi, unitendee mema mimi mtumishi wako; kwa sababu umenitia mimi mtumishi wako katika agano la Bwana pamoja nawe, lakini ikiwa mna uovu moyoni mwangu, uniue wewe mwenyewe; kwa nini kunileta kwa baba yako? 1 Samweli 20:8

Therefore deal kindly with your servant; for you have brought your servant into a covenant of Yahweh with you: but if there be in me iniquity, kill me yourself; for why should you bring me to your father?

Naye Yonathani akasema, Haya na yawe mbali nawe, kwa maana kama ningejua ya kuwa baba yangu amekusudia kukutenda neno baya, je! Singekuambia? 1 Samweli 20:9

Jonathan said, Far be it from you; for if I should at all know that evil were determined by my father to come on you, then wouldn't I tell you that?

Basi Daudi akamwambia Yonathani, Ni nani atakayeniambia, ikiwa baba yako amekujibu maneno makali? 1 Samweli 20:10

Then said David to Jonathan, Who shall tell me if perchance your father answer you roughly?

Yonathani akamwambia Daudi, Twende zetu nje mashambani. Wakatoka wote wawili, wakaenda mashambani. 1 Samweli 20:11

Jonathan said to David, Come, and let us go out into the field. They went out both of them into the field.

Naye Yonathani akamwambia Daudi, Bwana, Mungu wa Israeli, na awe shahidi; nitakapokuwa nimekwisha kumwuliza baba yangu, kama wakati huu kesho, au siku ya tatu, angalia, kama liko neno jema la kumfaa Daudi, je! Nisikupelekee habari na kukufunulia neno hili? 1 Samweli 20:12

Jonathan said to David, Yahweh, the God of Israel, [be witness]: when I have sounded my father about this time tomorrow, [or] the third day, behold, if there be good toward David, shall I not then send to you, and disclose it to you?

Bwana anitende mimi, Yonathani, hivyo, na kuzidi, ikiwa yampendeza babangu kukutenda mabaya, nisipokufunulia haya, na kukupeleka uende zako kwa amani; na Bwana awe pamoja nawe, kama alivyokuwa pamoja na baba yangu. 1 Samweli 20:13

Yahweh do so to Jonathan, and more also, should it please my father to do you evil, if I don't disclose it to you, and send you away, that you may go in peace: and Yahweh be with you, as he has been with my father.

Nawe utanionyesha fadhili za Bwana, ili nisife, si wakati huu tu maadamu mimi ni hai; 1 Samweli 20:14

You shall not only while yet I live show me the loving kindness of Yahweh, that I not die;

lakini pamoja na hayo, hata jamaa yangu pia hutawaondolea kabisa fadhili zako; la, hata wakati ule Bwana atakapokuwa amewaondoa kabisa adui za Daudi wote pia katika uso wa nchi. 1 Samweli 20:15

but also you shall not cut off your kindness from my house forever; no, not when Yahweh has cut off the enemies of David everyone from the surface of the earth.

Basi Yonathani akafanya agano na jamaa yake Daudi, akisema, Bwana naye atayataka mkononi mwa adui zake Daudi. 1 Samweli 20:16

So Jonathan made a covenant with the house of David, [saying], Yahweh will require it at the hand of David's enemies.

Naye Yonathani akamwapisha Daudi mara ya pili, kwa ajili ya upendo aliokuwa nao kwake; kwa maana alimpenda kama alivyoipenda roho yake mwenyewe. 1 Samweli 20:17

Jonathan caused David to swear again, for the love that he had to him; for he loved him as he loved his own soul.

Kisha Yonathani akamwambia, Kesho ni mwandamo wa mwezi, nawe utakosekana, kwa sababu kiti chako kitakuwa hakina mtu. 1 Samweli 20:18

Then Jonathan said to him, Tomorrow is the new moon: and you will be missed, because your seat will be empty.

Nawe ukiisha kungoja siku tatu, shuka upesi ufike kuko huko ulikojificha, siku ya shughuli ile; nawe kaa karibu na kile kichuguu kule. 1 Samweli 20:19

When you have stayed three days, you shall go down quickly, and come to the place where you did hide yourself when the business was in hand, and shall remain by the stone Ezel.

Nami nitapiga mishale mitatu kando-kando yake, kana kwamba ninapiga shabaha. 1 Samweli 20:20

I will shoot three arrows on the side of it, as though I shot at a mark.

Kisha, angalia, nitamtuma mtoto na kumwambia, Nenda ukaitafute mishale. Hapo nikimwambia yule mtoto, Tazama, mishale iko upande wako huu, itwae; basi uje, maana iko amani kwako, wala hapana hatari, Bwana aishivyo. 1 Samweli 20:21

Behold, I will send the boy, [saying], Go, find the arrows. If I tell the boy, Behold, the arrows are on this side of you; take them, and come; for there is peace to you and no hurt, as Yahweh lives.

Bali nikimwambia yule mtoto, Tazama, mishale iko huko mbele yako; basi enenda zako, kwa maana Bwana amekuamuru uende zako. 1 Samweli 20:22

But if I say thus to the boy, Behold, the arrows are beyond you; go your way; for Yahweh has sent you away.

Na kwa habari ya neno lile tulilonena, wewe na mimi, angalia Bwana yu kati ya wewe na mimi milele. 1 Samweli 20:23

As touching the matter which you and I have spoken of, behold, Yahweh is between you and me forever.

Basi Daudi akajificha shambani; na mwezi ulipoandama, mfalme aliketi kula chakula. 1 Samweli 20:24

So David hid himself in the field: and when the new moon was come, the king sat him down to eat food.

Mfalme aliketi kitini mwake kama sikuzote, katika kiti kilichokuwa karibu na ukuta; Yonathani alikuwa mbele yake; Abneri naye akaketi karibu na Sauli; lakini mahali pake Daudi palikuwa hapana mtu. 1 Samweli 20:25

The king sat on his seat, as at other times, even on the seat by the wall; and Jonathan stood up, and Abner sat by Saul's side: but David's place was empty.

Lakini Sauli hakusema neno siku ile; maana alidhani ya kuwa, Amepatikana na neno, hakutakata; hakosi yeye hakutakata. 1 Samweli 20:26

Nevertheless Saul didn't say anything that day: for he thought, Something has happened to him. He is not clean. Surely he is not clean.

Hata siku ya pili baada ya mwandamo wa mwezi, mahali pake palikuwa hapana mtu; basi Sauli akamwambia Yonathani mwanawe, Mbona mwana wa Yese haji kula chakula, jana wala leo? 1 Samweli 20:27

It happened on the next day after the new moon, [which was] the second [day], that David's place was empty: and Saul said to Jonathan his son, Why doesn't the son of Jesse come to meat, neither yesterday, nor today?

Naye Yonathani akamjibu Sauli, Daudi alitaka sana nimpe ruhusa aende Bethlehemu; 1 Samweli 20:28

Jonathan answered Saul, David earnestly asked leave of me to go to Bethlehem:

akasema, Tafadhali nipe ruhusa niende; kwa maana jamaa yetu wana dhabihu mjini mwetu; na ndugu yangu ameniamuru niende; basi sasa, kama nimeona kibali machoni pako, nakuomba, niondoke; nikawatazame ndugu zangu. Ndiyo sababu hakuja mezani pa mfalme. 1 Samweli 20:29

and he said, Please let me go, for our family has a sacrifice in the city; and my brother, he has commanded me [to be there]: and now, if I have found favor in your eyes, let me get away, I pray you, and see my brothers. Therefore he is not come to the king's table.

Basi hasira yake Sauli ikawaka juu ya Yonathani, akamwambia, Wewe, mwana wa mke mkaidi, asi, je! Mimi sijui ya kuwa umemchagua huyo mwana wa Yese, kwa aibu yako mwenyewe, na kwa aibu ya uchi wa mama yako. 1 Samweli 20:30

Then Saul's anger was kindled against Jonathan, and he said to him, You son of a perverse rebellious woman, don't I know that you have chosen the son of Jesse to your own shame, and to the shame of your mother's nakedness?

Maana wakati mwana wa Yese akiwa hai juu ya nchi, wewe hutafanikiwa, wala ufalme wako. Basi, sasa peleka, ukamlete kwangu, maana hakika yake atakufa huyu. 1 Samweli 20:31

For as long as the son of Jesse lives on the earth, you shall not be established, nor your kingdom. Therefore now send and bring him to me, for he shall surely die.

Yonathani akamjibu Sauli, baba yake, akamwambia, Auawe kwa sababu gani? Amefanya nini? 1 Samweli 20:32

Jonathan answered Saul his father, and said to him, "Why should he be put to death? What has he done?"

Sauli akamtupia mkuki wake ili kumpiga; basi Yonathani akajua ya kuwa baba yake ameazimu kumwua Daudi. 1 Samweli 20:33

Saul cast his spear at him to strike him. By this Jonathan knew that his father was determined to put David to death.

Basi Yonathani akaondoka pale mezani, mwenye hasira kali, wala hakula chakula siku ya pili ya mwezi, kwa sababu alimhuzunikia Daudi sana, na kwa sababu baba yake amemwaibisha. 1 Samweli 20:34

So Jonathan arose from the table in fierce anger, and ate no food the second day of the month; for he was grieved for David, because his father had done him shame.

Hata asubuhi Yonathani akatoka kwenda shambani wakati ule alioagana na Daudi, na mtoto mdogo alikuwa pamoja naye. 1 Samweli 20:35

It happened in the morning, that Jonathan went out into the field at the time appointed with David, and a little boy with him.

Akamwambia mtoto wake, Piga mbio, ukaitafute mishale niipigayo. Na yule mtoto alipokuwa akipiga mbio, akapiga mshale, ukapita juu yake. 1 Samweli 20:36

He said to his boy, Run, find now the arrows which I shoot. As the boy ran, he shot an arrow beyond him.

Na mtoto alipofika penye ule mshale alioupiga Yonathani, Yonathani akampigia mtoto kelele, akasema, Je! Mshale si huko mbele yako? 1 Samweli 20:37

When the boy was come to the place of the arrow which Jonathan had shot, Jonathan cried after the boy, and said, Isn't the arrow beyond you?

Yonathani akampigia mtoto kelele, Haya! Hima! Usikawie. Mtoto wa Yonathani akaikusanya mishale, akaenda kwa bwana wake. 1 Samweli 20:38

Jonathan cried after the boy, Go fast! Hurry! Don't delay! Jonathan's boy gathered up the arrows, and came to his master.

Lakini yule mtoto hakujua lo lote. Yonathani na Daudi ndio walioijua habari yenyewe. 1 Samweli 20:39

But the boy didn't know anything: only Jonathan and David knew the matter.

Naye Yonathani akampa mtoto silaha zake, akamwambia, Nenda, ukazichukue mjini. 1 Samweli 20:40

Jonathan gave his weapons to his boy, and said to him, Go, carry them to the city.

Basi mara alipokuwa amekwisha ondoka yule mtoto, mara Daudi akatoka mahali pale karibu na kile kichuguu, akaanguka kifudifudi, akajiinama mara tatu; nao wakabusiana, wakaliliana, hata Daudi akazidi. 1 Samweli 20:41

As soon as the boy was gone, David arose out of [a place] toward the South, and fell on his face to the ground, and bowed himself three times: and they kissed one another, and wept one with another, until David exceeded.

Naye Yonathani akamwambia Daudi, Enenda kwa amani; kwa maana sisi sote wawili tumeapiana kwa jina la Bwana ya kwamba, Bwana atakuwa kati ya mimi na wewe, na kati ya uzao wangu na uzao wako milele. Daudi akaondoka, akaenda zake; Yonathani naye akaenda zake mjini. 1 Samweli 20:42

Jonathan said to David, Go in peace, because we have sworn both of us in the name of Yahweh, saying, Yahweh shall be between me and you, and between my seed and your seed, forever. He arose and departed: and Jonathan went into the city.