1 Samweli 8 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Samweli 8 (Swahili) 1st Samuel 8 (English)

Hata Samweli alipokuwa mzee, aliwafanya wanawe wawe waamuzi juu ya Israeli. 1 Samweli 8:1

It happened, when Samuel was old, that he made his sons judges over Israel.

Na jina la mwanawe mzaliwa wa kwanza aliitwa Yoeli; na jina la wa pili Abiya; walikuwa waamuzi katika Beer-sheba. 1 Samweli 8:2

Now the name of his firstborn was Joel; and the name of his second, Abijah: they were judges in Beersheba.

Ila wanawe hawakuenda katika njia zake, bali waliziacha, ili wapate faida; wakapokea rushwa, na kupotosha hukumu. 1 Samweli 8:3

His sons didn't walk in his ways, but turned aside after lucre, and took bribes, and perverted justice.

Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama; 1 Samweli 8:4

Then all the elders of Israel gathered themselves together, and came to Samuel to Ramah;

wakamwambia, Angalia, wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; basi, tufanyie mfalme atuamue, mfano wa mataifa yote. 1 Samweli 8:5

and they said to him, Behold, you are old, and your sons don't walk in your ways: now make us a king to judge us like all the nations.

Lakini neno hilo likawa baya machoni pa Samweli, waliposema, Tupe mfalme atuamue. Naye Samweli akamwomba Bwana. 1 Samweli 8:6

But the thing displeased Samuel, when they said, Give us a king to judge us. Samuel prayed to Yahweh.

Bwana akamwambia Samweli, Isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokuambia; kwa maana hawakukukataa wewe, bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao. 1 Samweli 8:7

Yahweh said to Samuel, Listen to the voice of the people in all that they tell you; for they have not rejected you, but they have rejected me, that I should not be king over them.

Kwa kadiri ya matendo yote waliyonitenda tokea siku ile nilipowatoa katika Misri hata leo, kwa kuniacha mimi, na kwa kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokutenda wewe. 1 Samweli 8:8

According to all the works which they have done since the day that I brought them up out of Egypt even to this day, in that they have forsaken me, and served other gods, so do they also to you.

Basi sasa, isikilize sauti yao; walakini, uwaonye sana, na kuwaonyesha desturi ya mfalme atakayewamiliki. 1 Samweli 8:9

Now therefore listen to their voice: however you shall protest solemnly to them, and shall show them the manner of the king who shall reign over them.

Naye Samweli akawaambia wale watu waliotaka mfalme maneno yote ya Bwana. 1 Samweli 8:10

Samuel told all the words of Yahweh to the people who asked of him a king.

Akasema, Mfalme atakayewamiliki ninyi atakuwa na desturi hii; atatwaa wana wenu na kuwaweka kwake, kwa magari yake, na kuwa wapanda farasi wake; nao watapiga mbio mbele ya magari yake. 1 Samweli 8:11

He said, This will be the manner of the king who shall reign over you: he will take your sons, and appoint them to him, for his chariots, and to be his horsemen; and they shall run before his chariots;

Naye atawaweka kwake kuwa maakida juu ya elfu, na maakida juu ya hamsini; na wengine atawaweka walime shamba lake, na kuvuna mavuno yake, na kufanyiza zana zake za vita, na vyombo vya magari yake. 1 Samweli 8:12

and he will appoint them to him for captains of thousands, and captains of fifties; and [he will set some] to plow his ground, and to reap his harvest, and to make his instruments of war, and the instruments of his chariots.

Na binti zenu atawatwaa kuwa wafanyaji wa marhamu, na wapishi, na waokaji. 1 Samweli 8:13

He will take your daughters to be perfumers, and to be cooks, and to be bakers.

Atatwaa makonde yenu, na mashamba yenu ya mizabibu, na ya mizeituni, yale yaliyo mazuri sana, ili awape watumishi wake. 1 Samweli 8:14

He will take your fields, and your vineyards, and your olive groves, even the best of them, and give them to his servants.

Naye atawatoza ushuru wa mbegu zenu na wa mizabibu yenu, awape maakida wake, na watumishi Wake. 1 Samweli 8:15

He will take the tenth of your seed, and of your vineyards, and give to his officers, and to his servants.

Atawatwaa watumishi wenu na wajakazi wenu, na ng'ombe zenu walio wazuri sana, na punda zenu, naye atawatia katika kazi zake mwenyewe. 1 Samweli 8:16

He will take your men-servants, and your maid-servants, and your best young men, and your donkeys, and put them to his work.

Atawatoza fungu la kumi la makundi yenu; nanyi mtakuwa watumwa wake. 1 Samweli 8:17

He will take the tenth of your flocks: and you shall be his servants.

Nanyi mtalia siku ile kwa sababu ya mfalme wenu mliyejichagulia; Bwana asiwajibu siku ile. 1 Samweli 8:18

You shall cry out in that day because of your king whom you shall have chosen you; and Yahweh will not answer you in that day.

Walakini hao watu wakakataa kuisikiliza sauti ya Samweli; wakasema, Sivyo hivyo; lakini tunataka kuwa na mfalme juu yetu; 1 Samweli 8:19

But the people refused to listen to the voice of Samuel; and they said, No: but we will have a king over us,

ili sisi nasi tufanane na mataifa yote; tena ili mfalme wetu atuamue, tena atoke mbele yetu na kutupigia vita vyetu. 1 Samweli 8:20

that we also may be like all the nations, and that our king may judge us, and go out before us, and fight our battles.

Samweli akayasikia maneno yote ya watu, akayanena masikioni mwa Bwana. 1 Samweli 8:21

Samuel heard all the words of the people, and he rehearsed them in the ears of Yahweh.

Bwana akamwambia Samweli, Isikilize sauti yao, ukawafanyie mfalme. Kisha Samweli akawaambia watu wa Israeli, Enendeni kila mtu mjini kwake. 1 Samweli 8:22

Yahweh said to Samuel, Listen to their voice, and make them a king. Samuel said to the men of Israel, Go you every man to his city.