1 Samweli 17 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Samweli 17 (Swahili) 1st Samuel 17 (English)

Wakati huo Wafilisti walikusanya majeshi yao kwa vita, nao wakakusanyika huko Soko, ulio mji wa Yuda, wakatua kati ya Soko na Azeka, katika Efes-damimu. 1 Samweli 17:1

Now the Philistines gathered together their armies to battle; and they were gathered together at Socoh, which belongs to Judah, and encamped between Socoh and Azekah, in Ephesdammim.

Naye Sauli na watu wa Israeli wakakusanyika, wakatua katika bonde la Ela, nao wakapanga vita juu ya hao Wafilisti. 1 Samweli 17:2

Saul and the men of Israel were gathered together, and encamped in the valley of Elah, and set the battle in array against the Philistines.

Wafilisti wakasimama juu ya mlima upande huu, na Waisraeli wakasimama juu ya mlima upande huu, napo palikuwa na hilo bonde katikati. 1 Samweli 17:3

The Philistines stood on the mountain on the one side, and Israel stood on the mountain on the other side: and there was a valley between them.

Ndipo akatoka shujaa katika kambi ya Wafilisti, aliyeitwa Goliathi, wa Gathi, ambaye urefu wake ulikuwa mikono sita na shibiri moja. 1 Samweli 17:4

There went out a champion out of the camp of the Philistines, named Goliath, of Gath, whose height was six cubits and a span.

Alikuwa na chapeo ya shaba kichwani, tena amevaa darii ya shaba; na uzani wake ile darii ya shaba ulikuwa shekeli elfu tano za shaba. 1 Samweli 17:5

He had a helmet of brass on his head, and he was clad with a coat of mail; and the weight of the coat was five thousand shekels of brass.

Tena amevaa mabamba ya shaba miguuni mwake, naye alikuwa na mkuki wa shaba kati ya mabega; yake. 1 Samweli 17:6

He had brass shin-armor on his legs, and a javelin of brass between his shoulders.

Na mti wa fumo lake ulikuwa kama mti wa mfumaji; na kichwa cha mkuki wake kilikuwa shekeli mia sita za chuma uzito wake; na mtu aliyemchukulia ngao yake akamtangulia. 1 Samweli 17:7

The staff of his spear was like a weaver's beam; and his spear's head [weighed] six hundred shekels of iron: and his shield-bearer went before him.

Naye akasimama, akawapigia kelele majeshi ya Israeli akawaambia, Mbona mmetoka kupanga vita? Je! Mimi si Mfilisti, na ninyi si watumishi wa Sauli? Jichagulieni mtu, akanishukie mimi. 1 Samweli 17:8

He stood and cried to the armies of Israel, and said to them, Why are you come out to set your battle in array? am I not a Philistine, and you servants to Saul? choose you a man for you, and let him come down to me.

Kama akiweza kupigana nami na kuniua, sisi tutakuwa watumwa wenu; nami nikimshinda yeye na kumwua, ninyi mtakuwa watumwa wetu, na kututumikia. 1 Samweli 17:9

If he be able to fight with me, and kill me, then will we be your servants; but if I prevail against him, and kill him, then shall you be our servants, and serve us.

Yule Mfilisti akasema, Nayatukana leo majeshi ya Israeli; nipeni mtu tupigane. 1 Samweli 17:10

The Philistine said, I defy the armies of Israel this day; give me a man, that we may fight together.

Basi Sauli na Israeli wote waliposikia maneno hayo ya Mfilisti, wakafadhaika na kuogopa sana. 1 Samweli 17:11

When Saul and all Israel heard those words of the Philistine, they were dismayed, and greatly afraid.

Basi Daudi alikuwa mwana wa yule Mwefrathi, wa Bethlehemu ya Yuda, aliyeitwa jina lake Yese; naye huyo alikuwa na wana wanane; na yeye mwenyewe alikuwa mzee siku za Sauli, na mkongwe miongoni mwa watu. 1 Samweli 17:12

Now David was the son of that Ephrathite of Bethlehem Judah, whose name was Jesse; and he had eight sons: and the man was an old man in the days of Saul, stricken [in years] among men.

Nao wale wana watatu wa Yese waliokuwa wakubwa walikuwa wamefuatana na Sauli kwenda vitani, na majina ya hao wanawe watatu waliokwenda vitani ni haya, mzaliwa wa kwanza Eliabu, na wa pili wake Abinadabu, na wa tatu Shama. 1 Samweli 17:13

The three eldest sons of Jesse had gone after Saul to the battle: and the names of his three sons who went to the battle were Eliab the firstborn, and next to him Abinadab, and the third Shammah.

Naye huyo Daudi alikuwa mdogo wa wote; na hao watatu waliokuwa wakubwa wakafuatana na Sauli. 1 Samweli 17:14

David was the youngest; and the three eldest followed Saul.

Basi Daudi alikuwa akienda kwa Sauli na kurudi ili awalishe kondoo za baba yake huko Bethlehemu. 1 Samweli 17:15

Now David went back and forth from Saul to feed his father's sheep at Bethlehem.

Naye yule Mfilisti hukaribia asubuhi na jioni, akajitokeza siku arobaini. 1 Samweli 17:16

The Philistine drew near morning and evening, and presented himself forty days.

Ndipo Yese akamwambia Daudi mwanawe, Haya! Sasa uwachukulie ndugu zako efa ya bisi, na mikate hii kumi, ipeleke upesi kambini kwa ndugu zako; 1 Samweli 17:17

Jesse said to David his son, Take now for your brothers an ephah of this parched grain, and these ten loaves, and carry [them] quickly to the camp to your brothers;

ukampelekee akida wa elfu yao jibini hizi kumi, ukawaangalie, wa hali gani, kisha uniletee jawabu yao. 1 Samweli 17:18

and bring these ten cheeses to the captain of their thousand, and look how your brothers fare, and take their pledge.

Basi Sauli, na watu wote wa Israeli, walikuwa katika bonde la Ela, wakipigana na Wafilisti. 1 Samweli 17:19

Now Saul, and they, and all the men of Israel, were in the valley of Elah, fighting with the Philistines.

Daudi akaondoka asubuhi na mapema, akawaacha kondoo pamoja na mchungaji, akavitwaa vitu vile, akaenda, kama Yese alivyomwamuru; akafika penye magari, wakati lile jeshi walipokuwa wakitoka kwenda kupigana, wakipiga kelele za vita. 1 Samweli 17:20

David rose up early in the morning, and left the sheep with a keeper, and took, and went, as Jesse had commanded him; and he came to the place of the wagons, as the host which was going forth to the fight shouted for the battle.

Nao Waisraeli na Wafilisti wakajipanga, jeshi hili likikabili jeshi hili. 1 Samweli 17:21

Israel and the Philistines put the battle in array, army against army.

Basi Daudi akaviacha vile vyombo vyake katika mkono wa mlinda vyombo, akalikimbilia jeshi, akafika, akawasalimu ndugu zake. 1 Samweli 17:22

David left his baggage in the hand of the keeper of the baggage, and ran to the army, and came and greeted his brothers.

Hata alipokuwa akisema nao, kumbe! Yule shujaa alitokea, yule Mfilisti wa Gathi, jina lake Goliathi, akitoka katika jeshi la Wafilisti, akasema maneno yale yale; naye Daudi akayasikia. 1 Samweli 17:23

As he talked with them, behold, there came up the champion, the Philistine of Gath, Goliath by name, out of the ranks of the Philistines, and spoke according to the same words: and David heard them.

Na watu wote wa Israeli walipomwona yule mtu wakakimbia, wakaogopa sana. 1 Samweli 17:24

All the men of Israel, when they saw the man, fled from him, and were sore afraid.

Watu wa Israeli wakasema, Je! Mmemwona mtu huyu aliyepanda huko? Hakika ametokea ili awatukane Israeli; basi, itakuwa, mtu yule atakayemwua, mfalme atamtajirisha kwa utajiri mwingi, naye atamwoza binti yake, na kuifanya mbari ya baba yake kuwa huru katika Israeli. 1 Samweli 17:25

The men of Israel said, Have you seen this man who is come up? surely to defy Israel is he come up: and it shall be, that the man who kills him, the king will enrich him with great riches, and will give him his daughter, and make his father's house free in Israel.

Daudi akaongea na watu waliosimama karibu, akisema, Je! Atafanyiwaje yeye atakayemwua Mfilisti huyo, na kuwaondolea Israeli aibu hii? Maana Mfilisti huyu asiyetahiriwa ni nani hata awatukane majeshi ya Mungu aliye hai? 1 Samweli 17:26

David spoke to the men who stood by him, saying, What shall be done to the man who kills this Philistine, and takes away the reproach from Israel? for who is this uncircumcised Philistine, that he should defy the armies of the living God?

Nao watu wakamjibu vivyo hivyo, wakisema, Ndivyo atakavyofanyiwa mtu yule atakayemwua. 1 Samweli 17:27

The people answered him after this manner, saying, So shall it be done to the man who kills him.

Naye Eliabu, mkubwa wake, alisikia hapo alipoongea na watu; na hasira yake Eliabu ikawaka juu ya Daudi, akasema, Mbona wewe umeshuka hapa? Na kondoo wale wachache umemwachia nani kule nyikani? Mimi nakujua kiburi chako, na ubaya wa moyo wako; maana umeshuka ili upate kuvitazama vita. 1 Samweli 17:28

Eliab his eldest brother heard when he spoke to the men; and Eliab's anger was kindled against David, and he said, Why are you come down? and with whom have you left those few sheep in the wilderness? I know your pride, and the naughtiness of your heart; for you have come down that you might see the battle.

Naye Daudi akamjibu, Je! Mimi nimekosa nini sasa? Je! Si neno kubwa hilo? 1 Samweli 17:29

David said, What have I now done? Is there not a cause?

Naye akamgeukia ili kumwelekea mtu mwingine, akasema naye jinsi ile ile; na watu wakamjibu tena jinsi ile ile kama ya kwanza. 1 Samweli 17:30

He turned away from him toward another, and spoke after the same manner: and the people answered him again after the former manner.

Na maneno hayo aliyosema Daudi yaliposikiwa, watu wakamweleza Sauli; naye akatuma mtu kwenda kumwita. 1 Samweli 17:31

When the words were heard which David spoke, they rehearsed them before Saul; and he sent for him.

Daudi akamwambia Sauli, Asizimie moyo mtu ye yote kwa ajili ya huyu; mimi mtumishi wako nitakwenda kupigana na Mfilisti huyu. 1 Samweli 17:32

David said to Saul, Let no man's heart fail because of him; your servant will go and fight with this Philistine.

Sauli akamwambia Daudi, Huwezi wewe kumwendea Mfilisti huyu upigane naye; maana wewe u kijana tu; na huyu ni mtu wa vita tangu ujana wake. 1 Samweli 17:33

Saul said to David, You are not able to go against this Philistine to fight with him; for you are but a youth, and he a man of war from his youth.

Daudi akamwambia Sauli, Mtumishi wako alikuwa akichunga kondoo za baba yake, na alipokuwa akija simba, au dubu, akamkamata mwana-kondoo wa lile kundi, 1 Samweli 17:34

David said to Saul, Your servant was keeping his father's sheep; and when there came a lion, or a bear, and took a lamb out of the flock,

mimi hutoka nikamfuata, nikampiga, nikampokonya kinywani mwake; na akinirukia, humshika ndevu zake, nikampiga, nikamwua. 1 Samweli 17:35

I went out after him, and struck him, and delivered it out of his mouth; and when he arose against me, I caught him by his beard, and struck him, and killed him.

Mtumishi wako alimwua simba na dubu pia; na huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wao, kwa sababu amewatukana majeshi ya Mungu aliye hai. 1 Samweli 17:36

Your servant struck both the lion and the bear: and this uncircumcised Philistine shall be as one of them, seeing he has defied the armies of the living God.

Daudi akasema, Bwana aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu. Sauli akamwambia Daudi, Enenda, na Bwana atakuwa pamoja nawe. 1 Samweli 17:37

David said, Yahweh who delivered me out of the paw of the lion, and out of the paw of the bear, he will deliver me out of the hand of this Philistine. Saul said to David, Go, and Yahweh shall be with you.

Ndipo Sauli akamvika Daudi mavazi yake ya vita, akamtia chapeo cha shaba kichwani, akamvika dirii. 1 Samweli 17:38

Saul clad David with his clothing, and he put a helmet of brass on his head, and he clad him with a coat of mail.

Naye Daudi akajifunga upanga juu ya mavazi yake, akajaribu kwenda; maana alikuwa hajavijaribu. Daudi akamwambia Sauli, Siwezi kwenda na vitu hivi, maana sikuvijaribu. Basi Daudi akavivua. 1 Samweli 17:39

David girded his sword on his clothing, and he tried to go; for he had not proved it. David said to Saul, I can't go with these; for I have not proved them. David put them off him.

Akaichukua fimbo yake mkononi, akajichagulia mawe laini matano katika kijito cha maji, akayatia katika mfuko wa kichungaji aliokuwa nao, maana ni mkoba wake, na kombeo lake alikuwa nalo mkononi mwake, akamkaribia yule Mfilisti. 1 Samweli 17:40

He took his staff in his hand, and chose him five smooth stones out of the brook, and put them in the shepherd's bag which he had, even in his wallet; and his sling was in his hand: and he drew near to the Philistine.

Huyo Mfilisti naye akamsogelea Daudi na kumkaribia; na mtu yule aliyemchukulia ngao yake akamtangulia. 1 Samweli 17:41

The Philistine came on and drew near to David; and the man who bore the shield went before him.

Hata Mfilisti alipotazama huku na huku, akamwona Daudi akamdharau; kwa kuwa ni kijana tu mwekundu, tena ana sura nzuri. 1 Samweli 17:42

When the Philistine looked about, and saw David, he disdained him; for he was but a youth, and ruddy, and withal of a fair face.

Mfilisti akamwambia Daudi, Je! Mimi ni mbwa hata umenijia kwa fimbo? Mfilisti akamlaani Daudi kwa miungu yake. 1 Samweli 17:43

The Philistine said to David, Am I a dog, that you come to me with sticks? The Philistine cursed David by his gods.

Mfilisti akamwambia Daudi, Njoo huku kwangu; nyama yako nitawapa ndege wa angani na wanyama wa mwituni. 1 Samweli 17:44

The Philistine said to David, Come to me, and I will give your flesh to the birds of the sky, and to the animals of the field.

Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana. 1 Samweli 17:45

Then said David to the Philistine, You come to me with a sword, and with a spear, and with a javelin: but I come to you in the name of Yahweh of hosts, the God of the armies of Israel, whom you have defied.

Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli. 1 Samweli 17:46

This day will Yahweh deliver you into my hand; and I will strike you, and take your head from off you; and I will give the dead bodies of the host of the Philistines this day to the birds of the sky, and to the wild animals of the earth; that all the earth may know that there is a God in Israel,

Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu. 1 Samweli 17:47

and that all this assembly may know that Yahweh doesn't save with sword and spear: for the battle is Yahweh's, and he will give you into our hand.

Ikawa, hapo Mfilisti alipojiinua, akaenda akamkaribia Daudi, ndipo Daudi naye akapiga mbio, akalikimbilia jeshi ili akutane na yule Mfilisti. 1 Samweli 17:48

It happened, when the Philistine arose, and came and drew near to meet David, that David hurried, and ran toward the army to meet the Philistine.

Daudi akatia mkono wake mfukoni, akatwaa humo jiwe moja, akalitupa kwa kombeo lake, akampiga Mfilisti katika kipaji cha uso; jiwe hilo likamwingilia kipajini, akaanguka chini kifudifudi. 1 Samweli 17:49

David put his hand in his bag, and took there a stone, and slang it, and struck the Philistine in his forehead; and the stone sank into his forehead, and he fell on his face to the earth.

Hivyo Daudi akamshinda yule Mfilisti kwa kombeo na jiwe, akampiga Mfilisti, akamwua; walakini Daudi hakuwa na upanga mkononi mwake. 1 Samweli 17:50

So David prevailed over the Philistine with a sling and with a stone, and struck the Philistine, and killed him; but there was no sword in the hand of David.

Ndipo Daudi akapiga mbio, akasimama juu ya Mfilisti, akautwaa upanga wake, akaufuta alani mwake, akamwua, akamkata kichwa kwa upanga huo. Nao Wafilisti walipoona ya kuwa shujaa wao amekufa, wakakimbia. 1 Samweli 17:51

Then David ran, and stood over the Philistine, and took his sword, and drew it out of the sheath of it, and killed him, and cut off his head therewith. When the Philistines saw that their champion was dead, they fled.

Nao watu wa Israeli na wa Yuda wakainuka, na kupiga kelele, nao wakawafuata Wafilisti mpaka ufikapo Gathi, na mpaka malango ya Ekroni. Nao majeruhi wa Wafilisti wakaanguka kando ya njia iendayo Shaarimu, mpaka Gathi, na mpaka Ekroni. 1 Samweli 17:52

The men of Israel and of Judah arose, and shouted, and pursued the Philistines, until you come to Gai, and to the gates of Ekron. The wounded of the Philistines fell down by the way to Shaaraim, even to Gath, and to Ekron.

Kisha wana wa Israeli wakarudi kutoka katika kuwafukuza Wafilisti, wakateka nyara marago yao. 1 Samweli 17:53

The children of Israel returned from chasing after the Philistines, and they plundered their camp.

Naye Daudi akakitwaa kichwa chake yule Mfilisti na kukileta Yerusalemu; lakini silaha zake akaziweka hemani mwake. 1 Samweli 17:54

David took the head of the Philistine, and brought it to Jerusalem; but he put his armor in his tent.

Basi Sauli, hapo alipomwona Daudi akitoka ili kumwendea yule Mfilisti, alimwambia Abneri, jemadari wa jeshi, Je! Abneri, kijana huyu ni mwana wa nani? Abneri akamjibu, Ee mfalme, kama iishivyo roho yako, mimi siwezi kusema. 1 Samweli 17:55

When Saul saw David go forth against the Philistine, he said to Abner, the captain of the host, Abner, whose son is this youth? Abner said, As your soul lives, O king, I can't tell.

Basi mfalme akasema, Uliza wewe, kijana huyu ni mwana wa nani. 1 Samweli 17:56

The king said, "Inquire whose son the young man is!"

Hata na Daudi alipokuwa yuarudi kutoka katika kumwua yule Mfilisti, Abneri alimtwaa, akamleta mbele ya Sauli, naye anacho kichwa chake yule Mfilisti mkononi mwake. 1 Samweli 17:57

As David returned from the slaughter of the Philistine, Abner took him, and brought him before Saul with the head of the Philistine in his hand.

Basi Sauli akamwuliza, Wewe, kijana, u mwana wa nani? Naye Daudi akamjibu, Mimi ni mwana wa mtumishi wako, Yese, mtu wa Bethlehemu. 1 Samweli 17:58

Saul said to him, Whose son are you, you young man? David answered, I am the son of your servant Jesse the Bethlehemite.