1 Samweli 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Samweli 3 (Swahili) 1st Samuel 3 (English)

Basi, mtoto Samweli akamtumikia Bwana mbele ya Eli. Na neno la Bwana lilikuwa adimu siku zile; hapakuwa na mafunuo dhahiri. 1 Samweli 3:1

The child Samuel ministered to Yahweh before Eli. The word of Yahweh was precious in those days; there was no frequent vision.

Ikawa wakati huo, Eli alipokuwa amelala mahali pake (tena macho yake yalikuwa yameanza kupofuka, hata asiweze kuona), 1 Samweli 3:2

It happened at that time, when Eli was laid down in his place (now his eyes had begun to grow dim, so that he could not see),

na taa ya Mungu ilikuwa haijazimika bado, na Samweli alikuwa amelala katika hekalu la Bwana, palipokuwa na sanduku la Mungu; 1 Samweli 3:3

and the lamp of God hadn't yet gone out, and Samuel had laid down [to sleep], in the temple of Yahweh, where the ark of God was;

basi, wakati huo Bwana akamwita Samweli; naye akasema, Mimi hapa. 1 Samweli 3:4

that Yahweh called Samuel; and he said, Here am I.

Akamwendea Eli kwa haraka, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akasema, Sikukuita; kalale tena. Naye akaenda, akalala tena. 1 Samweli 3:5

He ran to Eli, and said, Here am I; for you called me. He said, I didn't call; lie down again. He went and lay down.

Bwana akaita mara ya pili, Samweli! Samweli! Akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akajibu, Sikukuita, mwanangu; kalale tena. 1 Samweli 3:6

Yahweh called yet again, Samuel. Samuel arose and went to Eli, and said, Here am I; for you called me. He answered, I didn't call, my son; lie down again.

Basi Samweli alikuwa hamjui Bwana bado, na neno la Bwana lilikuwa bado halijafunuliwa kwake. 1 Samweli 3:7

Now Samuel didn't yet know Yahweh, neither was the word of Yahweh yet revealed to him.

Bwana akamwita Samweli mara ya tatu. Naye akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Ndipo Eli akatambua ya kuwa Bwana ndiye aliyemwita yule mtoto. 1 Samweli 3:8

Yahweh called Samuel again the third time. He arose and went to Eli, and said, Here am I; for you called me. Eli perceived that Yahweh had called the child.

Kwa hivyo Eli akamwambia Samweli, Enenda, kalale; itakuwa, akikuita, utasema, Nena, Bwana; kwa kuwa mtumishi wako anasikia. Basi Samweli akaenda akalala mahali pake. 1 Samweli 3:9

Therefore Eli said to Samuel, Go, lie down: and it shall be, if he call you, that you shall say, Speak, Yahweh; for your servant hears. So Samuel went and lay down in his place.

Bwana akaja, akasimama, akaita vile vile kama kwanza, Samweli! Samweli! Ndipo Samweli akasema, Nena, Bwana; kwa kuwa mtumishi wako anasikia. 1 Samweli 3:10

Yahweh came, and stood, and called as at other times, Samuel, Samuel. Then Samuel said, Speak; for your servant hears.

Bwana akamwambia Samweli, Angalia, nitatenda tendo katika Israeli, ambalo kila atakayelisikia masikio yake yatamwasha. 1 Samweli 3:11

Yahweh said to Samuel, Behold, I will do a thing in Israel, at which both the ears of everyone who hears it shall tingle.

Siku hiyo nitayatimiza maneno yale yote niliyoyasema juu ya Eli katika habari za nyumba yake, tangu mwanzo hata mwisho. 1 Samweli 3:12

In that day I will perform against Eli all that I have spoken concerning his house, from the beginning even to the end.

Kwa maana nimemwambia ya kwamba nitaihukumu nyumba yake milele, kwa ajili ya ule uovu alioujua; kwa kuwa wanawe walijiletea laana, wala yeye hakuwazuia. 1 Samweli 3:13

For I have told him that I will judge his house forever, for the iniquity which he knew, because his sons did bring a curse on themselves, and he didn't restrain them.

Na kwa hiyo nimeapa juu ya nyumba ya Eli, ya kwamba uovu wa nyumba ya Eli hautasafika kwa dhabihu wala kwa sadaka hata milele. 1 Samweli 3:14

Therefore I have sworn to the house of Eli, that the iniquity of Eli's house shall not be expiated with sacrifice nor offering forever.

Naye Samweli akalala hata asubuhi, akaifungua milango ya nyumba ya Bwana. Samweli akaogopa kumjulisha Eli maono hayo. 1 Samweli 3:15

Samuel lay until the morning, and opened the doors of the house of Yahweh. Samuel feared to show Eli the vision.

Basi Eli akamwita Samweli, akasema, Samweli, mwanangu. Naye akajibu, Mimi hapa. 1 Samweli 3:16

Then Eli called Samuel, and said, Samuel, my son. He said, Here am I.

Akamwuliza, Ni neno gani alilosema nawe? Nakusihi, usinifiche; Mungu akufanyie vivyo hivyo, na kuzidi, ukinificha lo lote katika hayo yote Bwana aliyosema nawe. 1 Samweli 3:17

He said, "What is the thing that [Yahweh] has spoken to you? Please don't hide it from me. God do so to you, and more also, if you hide anything from me of all the things that he spoke to you."

Basi Samweli akamwambia kila neno, asimfiche lo lote. Naye akasema, Ndiye Bwana; na afanye alionalo kuwa ni jema. 1 Samweli 3:18

Samuel told him every whit, and hid nothing from him. He said, It is Yahweh: let him do what seems him good.

Samweli akakua, naye Bwana alikuwa pamoja naye, wala hakuliacha neno lake lo lote lianguke chini. 1 Samweli 3:19

Samuel grew, and Yahweh was with him, and did let none of his words fall to the ground.

Nao Waisraeli wote, toka Dani mpaka Beer-sheba, walitambua ya kwamba huyo Samweli amewekwa kuwa nabii wa Bwana. 1 Samweli 3:20

All Israel from Dan even to Beersheba knew that Samuel was established to be a prophet of Yahweh.

Naye Bwana akaonekana tena huko Shilo; kwa kuwa Bwana akajifunua kwa Samweli huko Shilo, kwa neno la Bwana. Nalo neno la Samweli likawajia Israeli wote. 1 Samweli 3:21

Yahweh appeared again in Shiloh; for Yahweh revealed himself to Samuel in Shiloh by the word of Yahweh.