1 Samweli 19 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Samweli 19 (Swahili) 1st Samuel 19 (English)

Kisha Sauli akasema na mwanawe Yonathani, tena na watumishi wake wote, kwamba wamwue Daudi. 1 Samweli 19:1

Saul spoke to Jonathan his son, and to all his servants, that they should kill David. But Jonathan, Saul's son, delighted much in David.

Lakini huyo Yonathani, mwana wake Sauli, alikuwa akipendezwa sana na Daudi. Basi Yonathani akamwambia Daudi, akasema, Sauli, baba yangu, anatafuta kukuua; basi, nakusihi, ujiangalie sana asubuhi, ukae mahali pa siri na kujificha; 1 Samweli 19:2

Jonathan told David, saying, Saul my father seeks to kill you: now therefore, please take care of yourself in the morning, and live in a secret place, and hide yourself:

na mimi nitatoka nje na kusimama kando ya babangu huko shambani ulipo wewe, nami nitazungumza na babangu habari zako; nami nikiona neno lo lote nitakuambia. 1 Samweli 19:3

and I will go out and stand beside my father in the field where you are, and I will commune with my father of you; and if I see anything, I will tell you.

Naye Yonathani akamsifu Daudi kwa Sauli, babaye akamwambia, Mfalme asikose juu ya mtumishi wake, yaani, juu ya Daudi kwa maana yeye hakukosa juu yako, tena matendo yake kwako yamekuwa mema sana. 1 Samweli 19:4

Jonathan spoke good of David to Saul his father, and said to him, Don't let the king sin against his servant, against David; because he has not sinned against you, and because his works have been very good toward you:

Kwa kuwa alitia uhai wake mkononi mwake, na kumpiga yule Mfilisti, naye Bwana akawatendea Israeli wote wokovu mkuu. Wewe mwenyewe uliona jambo hilo, ukafurahi; basi kwa nini kukosa juu ya damu isiyo na hatia, umwue huyo Daudi bure? 1 Samweli 19:5

for he put his life in his hand, and struck the Philistine, and Yahweh worked a great victory for all Israel: you saw it, and did rejoice; why then will you sin against innocent blood, to kill David without a cause?

Sauli akaisikiliza sauti ya Yonathani; naye Sauli akaapa, Aishivyo Bwana, yeye hatauawa. 1 Samweli 19:6

Saul listened to the voice of Jonathan: and Saul swore, As Yahweh lives, he shall not be put to death.

Basi Yonathani akamwita Daudi, naye Yonathani akamjulisha mambo hayo yote. Kisha Yonathani akamleta Daudi kwa Sauli, naye alikuwa akihudhuria mbele yake, kama kwanza. 1 Samweli 19:7

Jonathan called David, and Jonathan showed him all those things. Jonathan brought David to Saul, and he was in his presence, as before.

Baada ya hayo kulikuwa na vita tena; naye Daudi akatoka, naye akapigana na Wafilisti, naye akawaua kwa uuaji mkuu; nao wakakimbia mbele yake. 1 Samweli 19:8

There was war again: and David went out, and fought with the Philistines, and killed them with a great slaughter; and they fled before him.

Tena ikawa, roho mbaya kutoka kwa Bwana ilimjilia Sauli, hapo alipoketi ndani ya nyumba yake, akiwa na mkuki wake mkononi mwake; naye Daudi alikuwa akipiga kinubi kwa mkono wake. 1 Samweli 19:9

An evil spirit from Yahweh was on Saul, as he sat in his house with his spear in his hand; and David was playing with his hand.

Sauli akajaribu kumpiga Daudi hata ukutani kwa mkuki wake, ila yeye akaponyoka kutoka mbele ya Sauli, nao huo mkuki akaupiga ukutani; naye Daudi akakimbia, akaokoka usiku ule. 1 Samweli 19:10

Saul sought to strike David even to the wall with the spear; but he slipped away out of Saul's presence, and he struck the spear into the wall: and David fled, and escaped that night.

Kisha Sauli akatuma wajumbe mpaka nyumbani kwa Daudi, ili wamvizie na kumwua asubuhi; naye Mikali, mkewe Daudi, akamwambia, akasema, Wewe usipojiponya nafsi yako usiku huu, kesho utauawa. 1 Samweli 19:11

Saul sent messengers to David's house, to watch him, and to kill him in the morning: and Michal, David's wife, told him, saying, If you don't save your life tonight, tomorrow you will be slain.

Basi Mikali akamtelemsha Daudi dirishani; naye akaenda akakimbia na kuokoka. 1 Samweli 19:12

So Michal let David down through the window: and he went, and fled, and escaped.

Ndipo Mikali akakitwaa kinyago, na kukilaza kitandani, akatia na mto wa singa za mbuzi kichwani pake, na kukifunika kwa nguo. 1 Samweli 19:13

Michal took the teraphim, and laid it in the bed, and put a pillow of goats' [hair] at the head of it, and covered it with the clothes.

Naye Sauli alipotuma wajumbe ili kumkamata Daudi, yeye alisema, Hawezi. 1 Samweli 19:14

When Saul sent messengers to take David, she said, He is sick.

Basi Sauli akawatuma hao wajumbe ili wamtazame Daudi, akisema, Mleteni kwangu juu ya kitanda chake, nipate kumwua. 1 Samweli 19:15

Saul sent the messengers to see David, saying, Bring him up to me in the bed, that I may kill him.

Nao wajumbe walipoingia, kumbe! Kuna kinyago kitandani, na mto wa singa za mbuzi kichwani pake! 1 Samweli 19:16

When the messengers came in, behold, the teraphim was in the bed, with the pillow of goats' [hair] at the head of it.

Sauli akamwambia Mikali, Mbona wewe umenidanganya hivi, na kumwacha adui yangu aende, hata ameniponyoka? Naye Mikali akamjibu Sauli, Yeye aliniambia, Niache niende zangu; kwa nini nikuue? 1 Samweli 19:17

Saul said to Michal, Why have you deceived me thus, and let my enemy go, so that he is escaped? Michal answered Saul, He said to me, Let me go; why should I kill you?

Hivyo Daudi akakimbia, akajiponya, akamwendea Samweli huko Rama, akamwambia hayo yote Sauli aliyomtenda. Kisha yeye na Samweli wakaenda na kukaa katika Nayothi. 1 Samweli 19:18

Now David fled, and escaped, and came to Samuel to Ramah, and told him all that Saul had done to him. He and Samuel went and lived in Naioth.

Naye Sauli akaambiwa, kusema, Angalia, yule Daudi yuko katika Nayothi, huko Rama. 1 Samweli 19:19

It was told Saul, saying, Behold, David is at Naioth in Ramah.

Basi Sauli akatuma wajumbe ili kumkamata Daudi; nao hapo walipowaona jamaa ya manabii wakitabiri, na Samweli amesimama kama mkuu wao, roho ya Mungu ikawajilia wajumbe wa Sauli, nao pia wakatabiri. 1 Samweli 19:20

Saul sent messengers to take David: and when they saw the company of the prophets prophesying, and Samuel standing as head over them, the Spirit of God came on the messengers of Saul, and they also prophesied.

Naye Sauli alipoambiwa, alituma wajumbe wengine, wao nao wakatabiri. Naye Sauli akatuma wajumbe tena mara ya tatu, na wao pia wakatabiri. 1 Samweli 19:21

When it was told Saul, he sent other messengers, and they also prophesied. Saul sent messengers again the third time, and they also prophesied.

Kisha yeye mwenyewe akaenda Rama, akafika kunako kile kisima kikubwa kilicho huko Seku; akauliza, akasema, Je! Wako wapi Samweli na Daudi? Na mtu mmoja akajibu, Tazama, wako Nayothi, huko Rama. 1 Samweli 19:22

Then went he also to Ramah, and came to the great well that is in Secu: and he asked and said, Where are Samuel and David? One said, Behold, they are at Naioth in Ramah.

Basi akaenda Nayothi huko Rama, na roho ya Mungu ikamjilia yeye naye, akaendelea mbele, huku anatabiri, mpaka kufika Nayothi huko Rama. 1 Samweli 19:23

He went there to Naioth in Ramah: and the Spirit of God came on him also, and he went on, and prophesied, until he came to Naioth in Ramah.

Naye akavua nguo zake, akatabiri mbele ya Samweli, akalala uchi mchana kutwa na usiku kucha siku ile. Kwa hiyo watu husema, Je! Sauli pia yumo miongoni mwa manabii? 1 Samweli 19:24

He also stripped off his clothes, and he also prophesied before Samuel, and lay down naked all that day and all that night. Therefore they say, "Is Saul also among the prophets?"