1 Samweli 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Samweli 1 (Swahili) 1st Samuel 1 (English)

Palikuwa na mtu mmoja wa Rama, Msufi, wa nchi ya milima milima ya Efraimu, jina lake akiitwa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu, mwana wa Sufu, Mwefraimu 1 Samweli 1:1

Now there was a certain man of Ramathaim Zophim, of the hill-country of Ephraim, and his name was Elkanah, the son of Jeroham, the son of Elihu, the son of Tohu, the son of Zuph, an Ephraimite:

naye alikuwa na wake wawili; jina lake mmoja akiitwa Hana, na jina lake wa pili aliitwa Penina; naye huyo Penina alikuwa na watoto, lakini Hana hakuwa na watoto. 1 Samweli 1:2

and he had two wives; the name of the one was Hannah, and the name of other Peninnah: and Peninnah had children, but Hannah had no children.

Na mtu huyo alikuwa akikwea kutoka mjini kwake mwaka kwa mwaka, ili kuabudu, na kumtolea Bwana wa majeshi dhabihu katika Shilo. Na wale wana wawili wa Eli, Hofni na Finehasi, makuhani wa Bwana, walikuwako huko. 1 Samweli 1:3

This man went up out of his city from year to year to worship and to sacrifice to Yahweh of Hosts in Shiloh. The two sons of Eli, Hophni and Phinehas, priests to Yahweh, were there.

Hata siku ile ilipofika Elkana alipotoa dhabihu, kumpa mkewe Penina sehemu, akawapa na watoto wake wote, waume kwa wake, sehemu zao; 1 Samweli 1:4

When the day came that Elkanah sacrificed, he gave to Peninnah his wife, and to all her sons and her daughters, portions:

lakini Hana humpa sehemu mara mbili; maana alimpenda Hana, ingawa Bwana alikuwa amemfunga tumbo. 1 Samweli 1:5

but to Hannah he gave a double portion; for he loved Hannah, but Yahweh had shut up her womb.

Ila mwenzake humchokoza sana, hata kumsikitisha, kwa sababu Bwana alikuwa amemfunga tumbo. 1 Samweli 1:6

Her rival provoked her sore, to make her fret, because Yahweh had shut up her womb.

Tena mumewe akafanya hivyo mwaka kwa mwaka, hapo yule mwanamke alipokwea kwenda nyumbani kwa Bwana, ndivyo yule alivyomchokoza; basi, kwa hiyo, yeye akalia, asile chakula. 1 Samweli 1:7

[as] he did so year by year, when she went up to the house of Yahweh, so she provoked her; therefore she wept, and did not eat.

Elkana mumewe akamwambia, Hana, unalilia nini? Kwani huli chakula? Kwa nini moyo wako una huzuni? Je! Mimi si bora kwako kuliko watoto kumi? 1 Samweli 1:8

Elkanah her husband said to her, Hannah, why weep you? and why don't you eat? and why is your heart grieved? am I not better to you than ten sons?

Ndipo Hana akainuka, walipokwisha kula na kunywa huko Shilo. Naye Eli, kuhani, alikuwa akiketi kitini pake penye mwimo wa hekalu la Bwana. 1 Samweli 1:9

So Hannah rose up after they had eaten in Shiloh, and after they had drunk. Now Eli the priest was sitting on his seat by the door-post of the temple of Yahweh.

Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba Bwana akalia sana. 1 Samweli 1:10

She was in bitterness of soul, and prayed to Yahweh, and wept sore.

Akaweka nadhiri, akasema, Ee Bwana wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo mimi nitakapompa Bwana huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikilia kichwani kamwe. 1 Samweli 1:11

She vowed a vow, and said, Yahweh of hosts, if you will indeed look on the affliction of your handmaid, and remember me, and not forget your handmaid, but will give to your handmaid a man-child, then I will give him to Yahweh all the days of his life, and there shall no razor come on his head.

Ikawa, hapo alipodumu kuomba mbele za Bwana, Eli akamwangalia kinywa chake. 1 Samweli 1:12

It happened, as she continued praying before Yahweh, that Eli marked her mouth.

Basi Hana alikuwa akinena moyoni mwake; midomo yake tu ilionekana kama anena, sauti yake isisikiwe; kwa hiyo huyo Eli alimdhania kuwa amelewa. 1 Samweli 1:13

Now Hannah, she spoke in her heart; only her lips moved, but her voice was not heard: therefore Eli thought she had been drunken.

Ndipo Eli akamwambia, Je! Utakuwa mlevi hata lini? Achilia mbali divai yako. 1 Samweli 1:14

Eli said to her, How long will you be drunken? put away your wine from you.

Hana akajibu, akasema, Hasha! Bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni, mimi sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina roho yangu mbele za Bwana. 1 Samweli 1:15

Hannah answered, No, my lord, I am a woman of a sorrowful spirit: I have drunk neither wine nor strong drink, but I poured out my soul before Yahweh.

Usimdhanie mjakazi wako kuwa ni mwanamke asiyefaa kitu; kwa kuwa katika wingi wa kuugua kwangu na kusikitika kwangu ndivyo nilivyonena hata sasa. 1 Samweli 1:16

Don't count your handmaid for a wicked woman; for out of the abundance of my complaint and my provocation have I spoken hitherto.

Ndipo Eli akajibu, akasema, Enenda kwa amani; na Mungu wa Israeli akujalie haja yako uliyomwomba. 1 Samweli 1:17

Then Eli answered, Go in peace; and the God of Israel grant your petition that you have asked of him.

Naye akasema, Mjakazi wako na aone kibali machoni pako. Basi huyo mwanamke akaenda zake, naye akala chakula, wala uso wake haukukunjamana tena. 1 Samweli 1:18

She said, Let your handmaid find favor in your sight. So the woman went her way, and ate; and her facial expression wasn't sad any more.

Wakaondoka asubuhi na mapema, wakasali mbele za Bwana, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye Bwana akamkumbuka. 1 Samweli 1:19

They rose up in the morning early, and worshiped before Yahweh, and returned, and came to their house to Ramah: and Elkanah knew Hannah his wife; and Yahweh remembered her.

Ikawa, wakati ulipowadia, Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; akamwita jina lake Samweli, akisema, Kwa kuwa nimemwomba kwa Bwana. 1 Samweli 1:20

It happened, when the time was come about, that Hannah conceived, and bore a son; and she named him Samuel, [saying], Because I have asked him of Yahweh.

Kisha yule mtu, Elkana, na watu wote wa nyumbani mwake, wakakwea kwenda kumtolea Bwana dhabihu ya mwaka, na nadhiri yake. 1 Samweli 1:21

The man Elkanah, and all his house, went up to offer to Yahweh the yearly sacrifice, and his vow.

Bali Hana hakukwea; maana alimwambia mumewe, Sitakwea mimi hata mtoto wangu atakapoachishwa maziwa, hapo ndipo nitakapomleta, ili ahudhurie mbele za Bwana, akae huko daima. 1 Samweli 1:22

But Hannah didn't go up; for she said to her husband, [I will not go up] until the child be weaned; and then I will bring him, that he may appear before Yahweh, and there abide forever.

Elkana, mumewe, akamwambia, Haya, fanya uonavyo vema; ngoja hata utakapomwachisha maziwa; Bwana na alithibitishe neno lake tu. Basi yule mwanamke akangoja, akamnyonyesha mtoto wake, hata akamwachisha maziwa. 1 Samweli 1:23

Elkanah her husband said to her, Do what seems you good; wait until you have weaned him; only Yahweh establish his word. So the woman waited and nursed her son, until she weaned him.

Naye alipokuwa amekwisha kumwachisha maziwa, akamchukua pamoja naye, na ng'ombe watatu, na efa moja ya unga,na chupa ya divai,akamleta nyumbani kwa BWANA,huko Shilo ;na Yule mtoto alikuwa mtoto mdogo. 1 Samweli 1:24

When she had weaned him, she took him up with her, with three bulls, and one ephah of meal, and a bottle of wine, and brought him to the house of Yahweh in Shiloh: and the child was young.

Nao wakamchinja huyo ng'ombe, wakamleta mtoto kwa Eli. 1 Samweli 1:25

They killed the bull, and brought the child to Eli.

Akasema, Ee bwana wangu, kama iishivyo roho yako, bwana wangu, mimi ndimi yule mwanamke aliyesimama karibu nawe hapa, nikimwomba Bwana. 1 Samweli 1:26

She said, Oh, my lord, as your soul lives, my lord, I am the woman who stood by you here, praying to Yahweh.

Naliomba nipewe mtoto huyu; Bwana akanipa dua yangu niliyomwomba; 1 Samweli 1:27

For this child I prayed; and Yahweh has given me my petition which I asked of him:

kwa sababu hiyo mimi nami nimempa Bwana mtoto huyu; wakati wote atakaokuwa hai amepewa Bwana. Naye akamwabudu Bwana huko. 1 Samweli 1:28

therefore also I have granted him to Yahweh; as long as he lives he is granted to Yahweh. He worshiped Yahweh there.