1 Samweli 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Samweli 5 (Swahili) 1st Samuel 5 (English)

Basi Wafilisti walikuwa wamelichukua sanduku la Mungu, wakaenda nalo kutoka Eben-ezeri hata Ashdodi. 1 Samweli 5:1

Now the Philistines had taken the ark of God, and they brought it from Ebenezer to Ashdod.

Wafilisti wakalichukua sanduku la Mungu, wakalitia katika nyumba ya Dagoni, wakaliweka karibu na Dagoni. 1 Samweli 5:2

The Philistines took the ark of God, and brought it into the house of Dagon, and set it by Dagon.

Na watu wa Ashdodi, walipoamka alfajiri siku ya pili, kumbe! Dagoni imeanguka chini kifudifudi, mbele ya sanduku la Bwana. Wakaitwaa Dagoni, wakaisimamisha mahali pake tena. 1 Samweli 5:3

When they of Ashdod arose early on the next day, behold, Dagon was fallen on his face to the ground before the ark of Yahweh. They took Dagon, and set him in his place again.

Hata walipoamka kesho yake asubuhi, kumbe! Dagoni ilikuwa imeanguka chini kifudifudi, mbele ya sanduku la Bwana; na kichwa chake Dagoni na vitanga vya mikono yake vyote viwili vimekatika, vipo vimelala kizingitini; Dagoni ikasalia kiwiliwili chake tu. 1 Samweli 5:4

When they arose early on the next day morning, behold, Dagon was fallen on his face to the ground before the ark of Yahweh; and the head of Dagon and both the palms of his hands [lay] cut off on the threshold; only [the stump of] Dagon was left to him.

Kwa hiyo makuhani wa Dagoni, na mtu awaye yote aingiaye nyumbani mwa Dagoni, hawakanyagi kizingiti cha nyumba ya Dagoni huko Ashdodi, hata leo. 1 Samweli 5:5

Therefore neither the priests of Dagon, nor any who come into Dagon's house, tread on the threshold of Dagon in Ashdod, to this day.

Lakini mkono wa Bwana ulikuwa mzito juu ya watu wa Ashdodi, akawaharibu, akawapiga kwa majipu, huko Ashdodi na mipakani mwake. 1 Samweli 5:6

But the hand of Yahweh was heavy on them of Ashdod, and he destroyed them, and struck them with tumors, even Ashdod and the borders of it.

Kisha hao watu wa Ashdodi, walipoona ilivyokuwa, walisema, Hilo sanduku la Mungu wa Israeli halitakaa kwetu; kwa maana mkono wake ni mzito juu yetu, na juu ya Dagoni, mungu wetu. 1 Samweli 5:7

When the men of Ashdod saw that it was so, they said, The ark of the God of Israel shall not abide with us; for his hand is sore on us, and on Dagon our god.

Basi wakatuma watu waende kuwakusanya kwao mashehe wote wa Wafilisti, wakasema, Tulifanyieje sanduku la Mungu wa Israeli? Nao wakajibu, Sanduku la Mungu wa Israeli na lihamishwe liende Gathi. Wakalihamisha sanduku la Mungu wa Israeli. 1 Samweli 5:8

They sent therefore and gathered all the lords of the Philistines to them, and said, What shall we do with the ark of the God of Israel? They answered, Let the ark of the God of Israel be carried about to Gath. They carried the ark of the God of Israel [there].

Ikawa, walipokwisha lihamisha, mkono wa Bwana ulikuwa juu ya mji huo, kwa kuwafadhaisha sana; akawapiga watu wa mjini, wadogo kwa wakubwa, wakapatwa na majipu. 1 Samweli 5:9

It was so, that after they had carried it about, the hand of Yahweh was against the city with a very great confusion: and he struck the men of the city, both small and great; and tumors broke out on them.

Basi, wakalipeleka sanduku la Mungu mpaka Ekroni. Ikawa, sanduku la Mungu lilipofika Ekroni, watu wa Ekroni walifanya kelele, wakasema, Wamelileta hilo sanduku la Mungu wa Israeli kwetu, hata kutuua sisi na watu wetu. 1 Samweli 5:10

So they sent the ark of God to Ekron. It happened, as the ark of God came to Ekron, that the Ekronites cried out, saying, They have brought about the ark of the God of Israel to us, to kill us and our people.

Kwa hiyo wakatuma watu waende kuwakusanya mashehe wote wa Wafilisti, wakasema, Liondoeni hilo sanduku la Mungu wa Israeli, liende tena mahali pake, ili lisituue sisi, wala watu wetu; kwa sababu kulikuwa na fadhaa kubwa sana mjini mwote; mkono wa Mungu ulikuwa mzito mno huko. 1 Samweli 5:11

They sent therefore and gathered together all the lords of the Philistines, and they said, Send away the ark of the God of Israel, and let it go again to its own place, that it not kill us and our people. For there was a deadly confusion throughout all the city; the hand of God was very heavy there.

Na wale wasiokufa walipigwa kwa yale majipu; na kilio cha mji kikafika mbinguni. 1 Samweli 5:12

The men who didn't die were struck with the tumors; and the cry of the city went up to heaven.