1 Samweli 15 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Samweli 15 (Swahili) 1st Samuel 15 (English)

Wakati huo Samweli akamwambia Sauli, Bwana alinipeleka nikutie mafuta, uwe mfalme wa watu wake Israeli; basi sasa, isikilize sauti na maneno ya Bwana. 1 Samweli 15:1

Samuel said to Saul, Yahweh sent me to anoint you to be king over his people, over Israel: now therefore listen you to the voice of the words of Yahweh.

Bwana wa majeshi asema hivi, Nimeyatia moyoni mwangu mambo hayo Amaleki waliyowatenda Israeli, jinsi walivyowapinga njiani, hapo walipopanda kutoka Misri. 1 Samweli 15:2

Thus says Yahweh of Hosts, I have marked that which Amalek did to Israel, how he set himself against him in the way, when he came up out of Egypt.

Basi sasa enda ukawapige Amaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyo navyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, mtoto naye anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda. 1 Samweli 15:3

Now go and strike Amalek, and utterly destroy all that they have, and don't spare them; but kill both man and woman, infant and suckling, ox and sheep, camel and donkey.

Ndipo Sauli akawaita watu, akawahesabu huko Telemu, askari waliopanda farasi mia mbili elfu, na watu wa Yuda kumi elfu. 1 Samweli 15:4

Saul summoned the people, and numbered them in Telaim, two hundred thousand footmen, and ten thousand men of Judah.

Sauli akaufikilia mji wa Amaleki, akauvizia bondeni. 1 Samweli 15:5

Saul came to the city of Amalek, and laid wait in the valley.

Sauli akawaambia Wakeni, Haya! Enendeni zenu, mkashuke ili kujitenga na Waamaleki, nisije nikawaangamiza ninyi pamoja nao; maana mliwatendea wana wa Israeli mema, walipopanda kutoka Misri. Basi hao Wakeni wakaondoka, wakajitenga na Waamaleki. 1 Samweli 15:6

Saul said to the Kenites, Go, depart, get you down from among the Amalekites, lest I destroy you with them; for you shown kindness to all the children of Israel, when they came up out of Egypt. So the Kenites departed from among the Amalekites.

Sauli akawapiga Waamaleki, toka Havila uendapo Shuri, unaokabili Misri. 1 Samweli 15:7

Saul struck the Amalekites, from Havilah as you go to Shur, that is before Egypt.

Akamkamata Agagi, mfalme wa Waamaleki, yu hai, akawaangamiza hao watu wote kwa upanga. 1 Samweli 15:8

He took Agag the king of the Amalekites alive, and utterly destroyed all the people with the edge of the sword.

Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng'ombe, na vinono, na wana-kondoo, na cho chote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali cho chote kilichokuwa kibaya na kibovu, ndicho walichokiangamiza kabisa. 1 Samweli 15:9

But Saul and the people spared Agag, and the best of the sheep, and of the oxen, and of the fatlings, and the lambs, and all that was good, and wouldn't utterly destroy them: but everything that was vile and refuse, that they destroyed utterly.

Ndipo neno la Bwana likamjia Samweli, kusema, 1 Samweli 15:10

Then came the word of Yahweh to Samuel, saying,

Najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma, asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia Bwana usiku kucha. 1 Samweli 15:11

It repents me that I have set up Saul to be king; for he is turned back from following me, and has not performed my commandments. Samuel was angry; and he cried to Yahweh all night.

Samweli akaondoka asubuhi na mapema ili aonane na Sauli; Samweli akaambiwa ya kwamba, Sauli alifika Karmeli, na tazama, akajisimamishia ukumbusho, akageuka, akapita, akatelemkia Gilgali. 1 Samweli 15:12

Samuel rose early to meet Saul in the morning; and it was told Samuel, saying, Saul came to Carmel, and, behold, he set him up a monument, and turned, and passed on, and went down to Gilgal.

Samweli akamwendea Sauli; naye Sauli akamwambia, Ubarikiwe na Bwana, nimeitimiza amri ya Bwana. 1 Samweli 15:13

Samuel came to Saul; and Saul said to him, Blessed are you by Yahweh: I have performed the commandment of Yahweh.

Samweli akasema, Maana yake nini, basi, hiki kilio cha kondoo masikioni mwangu, na huu mlio wa ng'ombe ninaousikia? 1 Samweli 15:14

Samuel said, What means then this bleating of the sheep in my ears, and the lowing of the oxen which I hear?

Sauli akasema, Wamewaleta kutoka kwa Waamaleki; maana watu waliwaacha hai kondoo na ng'ombe walio wazuri, ili wawatoe dhabihu kwa Bwana, Mungu wako, nao waliosalia tumewaangamiza kabisa. 1 Samweli 15:15

Saul said, They have brought them from the Amalekites: for the people spared the best of the sheep and of the oxen, to sacrifice to Yahweh your God; and the rest we have utterly destroyed.

Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Ngoja, nami nitakuambia neno aliloniambia Bwana usiku huu. Naye akamwambia, Haya, sema. 1 Samweli 15:16

Then Samuel said to Saul, Stay, and I will tell you what Yahweh has said to me this night. He said to him, Say on.

Basi Samweli akasema, Ingawa ulikuwa mdogo machoni pako mwenyewe, je! Hukufanywa kuwa kichwa cha kabila za Israeli? Naye Bwana akakutia mafuta uwe mfalme wa Israeli. 1 Samweli 15:17

Samuel said, "Though you were little in your own sight, weren't you made the head of the tribes of Israel? Yahweh anointed you king over Israel;

Kisha Bwana akakutuma safarini, akasema, Enenda ukawaangamize kabisa wale Waamaleki wenye dhambi, upigane nao hata watakapoangamia. 1 Samweli 15:18

and Yahweh sent you on a journey, and said, 'Go, and utterly destroy the sinners the Amalekites, and fight against them until they are consumed.'

Mbona, basi, hukuitii sauti ya Bwana, bali ukazirukia nyara ukafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana? 1 Samweli 15:19

Why then didn't you obey the voice of Yahweh, but flew on the spoil, and did that which was evil in the sight of Yahweh?"

Sauli akamwambia Samweli, Hakika mimi nimeitii sauti ya Bwana, nami nimemleta Agagi, mfalme wa Waamaleki, tena nimewaangamiza Waamaleki kabisa. 1 Samweli 15:20

Saul said to Samuel, Yes, I have obeyed the voice of Yahweh, and have gone the way which Yahweh sent me, and have brought Agag the king of Amalek, and have utterly destroyed the Amalekites.

Ila watu waliteka nyara, kondoo na ng'ombe walio wazuri, katika vitu vilivyowekwa wakfu, kusudi wavitoe dhabihu kwa Bwana, Mungu wako, huko Gilgali. 1 Samweli 15:21

But the people took of the spoil, sheep and oxen, the chief of the devoted things, to sacrifice to Yahweh your God in Gilgal.

Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu. 1 Samweli 15:22

Samuel said, Has Yahweh as great delight in burnt offerings and sacrifices, as in obeying the voice of Yahweh? Behold, to obey is better than sacrifice, and to listen than the fat of rams.

Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme. 1 Samweli 15:23

For rebellion is as the sin of witchcraft, and stubbornness is as idolatry and teraphim. Because you have rejected the word of Yahweh, he has also rejected you from being king.

Ndipo Sauli akamwambia Samweli, Nimefanya dhambi; maana nimeihalifu amri ya Bwana, pia na maneno yako; kwa sababu naliwaogopa wale watu, nikaitii sauti yao. 1 Samweli 15:24

Saul said to Samuel, I have sinned; for I have transgressed the commandment of Yahweh, and your words, because I feared the people, and obeyed their voice.

Basi sasa, nakuomba, unisamehe dhambi yangu; rudi pamoja nami, nipate kumwabudu Bwana. 1 Samweli 15:25

Now therefore, please pardon my sin, and turn again with me, that I may worship Yahweh.

Samweli akasema, Sitarudi pamoja nawe; kwa sababu umelikataa neno la Bwana, Bwana naye amekukataa wewe, usiwe mfalme wa Israeli. 1 Samweli 15:26

Samuel said to Saul, I will not return with you; for you have rejected the word of Yahweh, and Yahweh has rejected you from being king over Israel.

Naye Samweli alipogeuka, aende zake, Sauli akaushika upindo wa vazi lake, nalo likararuka. 1 Samweli 15:27

As Samuel turned about to go away, [Saul] laid hold on the skirt of his robe, and it tore.

Basi Samweli akamwambia, Leo Bwana amekurarulia ufalme wa Israeli, naye amempa jirani yako, aliye mwema kuliko wewe. 1 Samweli 15:28

Samuel said to him, Yahweh has torn the kingdom of Israel from you this day, and has given it to a neighbor of yours who is better than you.

Tena Yeye aliye Nguvu za Israeli hatanena uongo, wala hataona majuto; maana siye mwanadamu, hata ajute. 1 Samweli 15:29

Also the Strength of Israel will not lie nor repent; for he is not a man, that he should repent.

Akasema, Nimekosa; lakini uniheshimu sasa, nakuomba, mbele ya wazee wa watu wangu, na mbele ya Israeli, rudi pamoja nami, nimwabudu Bwana, Mungu wako. 1 Samweli 15:30

Then he said, I have sinned: yet honor me now, Please, before the elders of my people, and before Israel, and turn again with me, that I may worship Yahweh your God.

Basi Samweli akarudi na kuandamana na Sauli; naye Sauli akamwabudu Bwana. 1 Samweli 15:31

So Samuel turned again after Saul; and Saul worshiped Yahweh.

Ndipo Samweli akasema, Nileteeni hapa Agagi, mfalme wa Waamaleki. Basi Agagi akamwendea kwa utepetevu. Naye Agagi akasema, Bila shaka uchungu wa mauti umeondoka. 1 Samweli 15:32

Then said Samuel, Bring you here to me Agag the king of the Amalekites. Agag came to him cheerfully. Agag said, Surely the bitterness of death is past.

Lakini Samweli akamjibu, Kama upanga wako ulivyofanya wanawake kufiwa na watoto wao, vivyo hivyo mama yako atafiwa miongoni mwa wanawake. Basi Samweli akamkata Agagi vipande mbele za Bwana huko Gilgali. 1 Samweli 15:33

Samuel said, As your sword has made women childless, so shall your mother be childless among women. Samuel hewed Agag in pieces before Yahweh in Gilgal.

Na baada ya hayo Samweli akaenda zake kule Rama; naye Sauli akakwea kwenda nyumbani kwake huko Gibea ya Sauli. 1 Samweli 15:34

Then Samuel went to Ramah; and Saul went up to his house to Gibeah of Saul.

Wala Samweli hakuenda tena kuonana na Sauli hata siku ya kufa kwake; lakini Samweli alikuwa akimlilia Sauli; naye Bwana akaghairi ya kuwa amemtawaza Sauli awe mfalme juu ya Israeli.

1 Samweli 15:35

Samuel came no more to see Saul until the day of his death; for Samuel mourned for Saul: and Yahweh repented that he had made Saul king over Israel.