1 Samweli 7 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Samweli 7 (Swahili) 1st Samuel 7 (English)

Na hao watu wa Kiriath-yearimu wakaja, wakalichukua sanduku la Bwana, wakalileta ndani ya nyumba ya Abinadabu huko kilimani, nao wakamtenga Eleazari, mwanawe, ili alilinde sanduku la Bwana. 1 Samweli 7:1

The men of Kiriath Jearim came, and fetched up the ark of Yahweh, and brought it into the house of Abinadab in the hill, and sanctified Eleazar his son to keep the ark of Yahweh.

Ikawa, tangu siku hiyo ambayo sanduku lilikaa Kiriath-yearimu wakati ulikuwa mwingi; kwa maana ulikuwa miaka ishirini; na nyumba yote ya Israeli wakamwombolezea Bwana. 1 Samweli 7:2

It happened, from the day that the ark abode in Kiriath Jearim, that the time was long; for it was twenty years: and all the house of Israel lamented after Yahweh.

Basi Samweli akawaambia nyumba yote ya Israeli, akasema, Ikiwa mnamrudia Bwana kwa mioyo yenu yote, basi, iondoleeni mbali miungu migeni, nayo Maashtorethi yatoke kwenu, mkamtengenezee Bwana mioyo yenu, mkamtumikie yeye peke yake; naye atawaokoa katika mikono ya Wafilisti. 1 Samweli 7:3

Samuel spoke to all the house of Israel, saying, If you do return to Yahweh with all your heart, then put away the foreign gods and the Ashtaroth from among you, and direct your hearts to Yahweh, and serve him only; and he will deliver you out of the hand of the Philistines.

Ndipo wana wa Israeli wakayaondoa Mabaali na Maashtorethi, wakamtumikia Bwana peke yake. 1 Samweli 7:4

Then the children of Israel did put away the Baals and the Ashtaroth, and served Yahweh only.

Samweli akasema, Wakusanyeni Israeli wote Mispa, nami nitawaombea ninyi kwa Bwana. 1 Samweli 7:5

Samuel said, Gather all Israel to Mizpah, and I will pray for you to Yahweh.

Wakakusanyika huko Mispa, wakateka maji na kuyamimina mbele za Bwana; wakafunga siku ile, wakasema huko, Tumemfanyia Bwana dhambi. Samweli akawaamua wana wa Israeli huko Mispa. 1 Samweli 7:6

They gathered together to Mizpah, and drew water, and poured it out before Yahweh, and fasted on that day, and said there, We have sinned against Yahweh. Samuel judged the children of Israel in Mizpah.

Hata Wafilisti waliposikia ya kuwa wana wa Israeli wamekusanyika huko Mispa, mashehe wa Wafilisti walipanda juu ili kupigana na Israeli. Nao wana wa Israeli waliposikia, wakawaogopa Wafilisti. 1 Samweli 7:7

When the Philistines heard that the children of Israel were gathered together at Mizpah, the lords of the Philistines went up against Israel. When the children of Israel heard it, they were afraid of the Philistines.

Wana wa Israeli wakamwambia Samweli, Usiache kumlilia Bwana, Mungu wetu, kwa ajili yetu, kwamba atuokoe na mikono ya Wafilisti. 1 Samweli 7:8

The children of Israel said to Samuel, "Don't cease to cry to Yahweh our God for us, that he will save us out of the hand of the Philistines."

Ndipo Samweli akatwaa mwana-kondoo mchanga, akamtolea Bwana sadaka ya kuteketezwa nzima; Samweli akamlilia Bwana kwa ajili ya Israeli; Bwana akamwitikia. 1 Samweli 7:9

Samuel took a sucking lamb, and offered it for a whole burnt-offering to Yahweh: and Samuel cried to Yahweh for Israel; and Yahweh answered him.

Hata Samweli alipokuwa akiitoa hiyo sadaka ya kuteketezwa, Wafilisti wakakaribia ili kupigana na Israeli; walakini Bwana akapiga ngurumo, mshindo mkubwa sana, juu ya Wafilisti siku ile, akawafadhaisha; nao wakaangamizwa mbele ya Israeli. 1 Samweli 7:10

As Samuel was offering up the burnt offering, the Philistines drew near to battle against Israel; but Yahweh thundered with a great thunder on that day on the Philistines, and confused them; and they were struck down before Israel.

Nao watu wa Israeli wakatoka Mispa, wakawafuatia Wafilisti, wakawapiga, hata walipofika chini ya Beth-kari. 1 Samweli 7:11

The men of Israel went out of Mizpah, and pursued the Philistines, and struck them, until they came under Beth Kar.

Ndipo Samweli akatwaa jiwe, na kulisimamisha kati ya Mispa na Sheni, akaliita jina lake Eben-ezeri, akisema, Hata sasa Bwana ametusaidia. 1 Samweli 7:12

Then Samuel took a stone, and set it between Mizpah and Shen, and called the name of it Ebenezer, saying, Hitherto has Yahweh helped us.

Hivyo Wafilisti walishindwa, wasiingie tena ndani ya mipaka ya Israeli; na mkono wa Bwana ulikuwa juu ya Wafilisti siku zote za Samweli. 1 Samweli 7:13

So the Philistines were subdued, and they came no more within the border of Israel: and the hand of Yahweh was against the Philistines all the days of Samuel.

Nayo miji ile Wafilisti waliyokuwa wamewapokonya Waisraeli ilirudishwa tena kwa Israeli, tokea Ekroni mpaka Gathi; na Waisraeli wakauokoa mpaka wake mikononi mwa Wafilisti. Tena kulikuwa na amani kati ya Israeli na Waamori. 1 Samweli 7:14

The cities which the Philistines had taken from Israel were restored to Israel, from Ekron even to Gath; and the border of it did Israel deliver out of the hand of the Philistines. There was peace between Israel and the Amorites.

Naye huyo Samweli akawaamua Israeli siku zote za maisha yake. 1 Samweli 7:15

Samuel judged Israel all the days of his life.

Naye huenda mwaka kwa mwaka kuzunguka mpaka Betheli, na Gilgali, na Mispa; akawaamua Israeli mahali hapo pote. 1 Samweli 7:16

He went from year to year in circuit to Bethel and Gilgal, and Mizpah; and he judged Israel in all those places.

Na kurudi kwake kulikuwa mpaka Rama; maana ndipo ilipokuwa nyumba yake; nako ndiko alikowaamua Israeli; na huko akamjengea Bwana madhabahu. 1 Samweli 7:17

His return was to Ramah, for there was his house; and there he judged Israel: and he built there an altar to Yahweh.