1 Samweli 10 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Samweli 10 (Swahili) 1st Samuel 10 (English)

Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu, akasema, Je! Bwana hakukutia mafuta [uwe mkuu juu ya watu wake Israeli? Nawe utamiliki watu wa Bwana, na kuwaokoa na mikono ya adui zao; kisha hii itakuwa ishara kwako ya kuwa Bwana amekutia mafuta] uwe mkuu juu ya urithi wake. 1 Samweli 10:1

Then Samuel took the vial of oil, and poured it on his head, and kissed him, and said, Isn't it that Yahweh has anointed you to be prince over his inheritance?

Utakapoondoka kwangu leo, utakutana na wanaume wawili karibu na kaburi la Raheli, katika mpaka wa Benyamini huko Selsa; nao watakuambia, Punda hao uliokwenda kuwatafuta wameonekana; na tazama, baba yako ameacha kufikiri habari za punda, anafikiri habari zenu, akisema, Nifanye nini kwa ajili ya mwanangu? 1 Samweli 10:2

When you are departed from me today, then you shall find two men by Rachel's tomb, in the border of Benjamin at Zelzah; and they will tell you, The donkeys which you went to seek are found; and, behold, your father has left off caring for the donkeys, and is anxious for you, saying, What shall I do for my son?

Kisha utakwenda mbele kutoka hapo, na kufika kwa mwaloni wa Tabori, na hapo watu watatu watakutana nawe, wanaokwea kumwendea Mungu huko Betheli, mmoja anachukua wana-mbuzi watatu, na mwingine anachukua mikate mitatu, na mwingine anachukua kiriba cha divai; 1 Samweli 10:3

Then shall you go on forward from there, and you shall come to the oak of Tabor; and there shall meet you there three men going up to God to Bethel, one carrying three kids, and another carrying three loaves of bread, and another carrying a bottle of wine:

nao watakusalimu na kukupa mikate miwili; nawe utaipokea mikononi mwao. 1 Samweli 10:4

and they will greet you, and give you two loaves of bread, which you shall receive of their hand.

Baada ya hayo utafika Gibea ya Mungu, hapo palipo na ngome ya Wafilisti; kisha itakuwa, utakapofika mjini, utakutana na kundi la manabii wakishuka kutoka mahali pa juu, wenye kinanda, na tari, na kinubi, na filimbi mbele yao, nao watakuwa wakitabiri; 1 Samweli 10:5

After that you shall come to the hill of God, where is the garrison of the Philistines: and it shall happen, when you are come there to the city, that you shall meet a band of prophets coming down from the high place with a psaltery, and a tambourine, and a pipe, and a harp, before them; and they will be prophesying:

na roho ya Bwana itakujilia kwa nguvu, nawe utatabiri pamoja nao, nawe utageuzwa kuwa mtu mwingine. 1 Samweli 10:6

and the Spirit of Yahweh will come mightily on you, and you shall prophesy with them, and shall be turned into another man.

Basi, hapo ishara hizi zitakapokutukia, fanya kama uonavyo vema; kwa kuwa Mungu yu pamoja nawe. 1 Samweli 10:7

Let it be, when these signs are come to you, that you do as occasion shall serve you; for God is with you.

Nawe utatelemka mbele yangu mpaka Gilgali; nami, angalia, nitakutelemkia huko, ili kutoa sadaka za kuteketezwa, na kuchinja sadaka za amani; siku saba utangoja, hata nitakapokujia, na kukuonyesha yatakayokupasa kuyafanya. 1 Samweli 10:8

You shall go down before me to Gilgal; and, behold, I will come down to you, to offer burnt offerings, and to sacrifice sacrifices of peace-offerings: seven days shall you wait, until I come to you, and show you what you shall do.

Ikawa, alipogeuka kumwacha Samweli, Mungu akambadilisha moyo; nazo ishara zile zote zikatukia siku ile ile. 1 Samweli 10:9

It was so, that when he had turned his back to go from Samuel, God gave him another heart: and all those signs happened that day.

Basi, walipofika Gibea, tazama, kikosi cha manabii wakakutana naye; kisha roho ya Mungu ikamjilia kwa nguvu, naye akatabiri kati yao. 1 Samweli 10:10

When they came there to the hill, behold, a band of prophets met him; and the Spirit of God came mightily on him, and he prophesied among them.

Ikawa, wote waliomjua zamani walipoliona jambo hilo, kwamba, tazama, huyo anatabiri pamoja na manabii, ndipo watu wakasemezana, Ni nini hilo lililompata mwana wa Kishi? Je! Sauli pia yumo miongoni mwa manabii? 1 Samweli 10:11

It happened, when all who knew him before saw that, behold, he prophesied with the prophets, then the people said one to another, What is this that is come to the son of Kish? Is Saul also among the prophets?

Naye akajibu mtu mmoja wa mahali hapo, akasema, Na baba yao n'nani? Kwa hiyo ikawa mithali, Je! Sauli pia yumo miongoni mwa manabii? 1 Samweli 10:12

One of the same place answered, Who is their father? Therefore it became a proverb, Is Saul also among the prophets?

Naye alipokwisha kutabiri, alipafikilia mahali pale pa juu. 1 Samweli 10:13

When he had made an end of prophesying, he came to the high place.

Basi babaye mdogo akamwuliza Sauli na mtumishi wake, Je! Mlikwenda wapi? Naye akajibu, Tulikwenda ili kuwatafuta hao punda; na tulipoona ya kwamba hawakuonekana, tulimwendea Samweli. 1 Samweli 10:14

Saul's uncle said to him and to his servant, Where went you? He said, To seek the donkeys; and when we saw that they were not found, we came to Samuel.

Babaye mdogo Sauli akasema, Tafadhali uniambie, huyo Samweli aliwaambiaje? 1 Samweli 10:15

Saul's uncle said, Tell me, Please, what Samuel said to you.

Lakini Sauli akamjibu babaye mdogo, Alituambia waziwazi ya kuwa hao punda wamekwisha onekana. Lakini habari ya ufalme, ambayo Samweli alimwambia, hakuitaja habari hiyo. 1 Samweli 10:16

Saul said to his uncle, He told us plainly that the donkeys were found. But concerning the matter of the kingdom, of which Samuel spoke, he didn't tell him.

Basi Samweli akawakusanya watu mbele za Bwana huko Mispa 1 Samweli 10:17

Samuel called the people together to Yahweh to Mizpah;

akawaambia wana wa Israeli, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Naliwatoa Israeli kutoka Misri, nami naliwaokoa ninyi na mikono ya Wamisri, na ya falme zote zilizowaonea; 1 Samweli 10:18

and he said to the children of Israel, Thus says Yahweh, the God of Israel, I brought up Israel out of Egypt, and I delivered you out of the hand of the Egyptians, and out of the hand of all the kingdoms that oppressed you:

lakini leo mmemkataa Mungu wenu, naye ndiye awaponyaye katika misiba yenu yote na shida zenu; nanyi mmemwambia, Sivyo, lakini weka mfalme juu yetu. Basi, sasa, hudhurieni mbele za Bwana, kwa kabila zenu na kwa elfu zenu. 1 Samweli 10:19

but you have this day rejected your God, who himself saves you out of all your calamities and your distresses; and you have said to him, [No], but set a king over us. Now therefore present yourselves before Yahweh by your tribes, and by your thousands.

Basi Samweli akawaleta kabila zote za Israeli karibu; na kabila ya Benyamini ikatwaliwa. 1 Samweli 10:20

So Samuel brought all the tribes of Israel near, and the tribe of Benjamin was taken.

Kisha akaileta kabila ya Benyamini karibu, kwa jamaa zao; jamaa ya Wamatri ikatwaliwa. Akaileta jamaa ya Wamatri karibu, mtu baada ya mtu; kisha Sauli, mwana wa Kishi, akatwaliwa; lakini walipomtafuta hakuonekana. 1 Samweli 10:21

He brought the tribe of Benjamin near by their families; and the family of the Matrites was taken; and Saul the son of Kish was taken: but when they sought him, he could not be found.

Basi wakazidi kumwuliza Bwana, Amebaki mtu asiyekuja huku bado? Naye Bwana akajibu, Tazama, amejificha penye mizigo. 1 Samweli 10:22

Therefore they asked of Yahweh further, Is there yet a man to come here? Yahweh answered, Behold, he has hid himself among the baggage.

Basi wakaenda mbio wakamleta kutoka huko; naye aliposimama kati ya watu, alikuwa mrefu kuliko watu wote, tangu mabega yake kwenda juu. 1 Samweli 10:23

They ran and fetched him there; and when he stood among the people, he was higher than any of the people from his shoulders and upward.

Samweli akawaambia watu wote, Mnamwona mtu huyu aliyechaguliwa na Bwana, ya kuwa hakuna mtu mfano wake katika watu wote. Ndipo watu wote wakapiga kelele, wakasema, Mfalme na aishi! 1 Samweli 10:24

Samuel said to all the people, "You see him whom Yahweh has chosen, that there is none like him among all the people?" All the people shouted, and said, [Long] live the king.

Kisha Samweli aliwaambia watu madaraka ya ufalme, akayaandika katika kitabu, akakiweka mbele za Bwana. Samweli akawaruhusu watu wote, waende kila mtu nyumbani kwake. 1 Samweli 10:25

Then Samuel told the people the manner of the kingdom, and wrote it in a book, and laid it up before Yahweh. Samuel sent all the people away, every man to his house.

Sauli naye akaenda nyumbani kwake huko Gibea; na pamoja naye wakaenda kikosi cha watu, ambao Mungu alikuwa ameigusa mioyo yao. 1 Samweli 10:26

Saul also went to his house to Gibeah; and there went with him the host, whose hearts God had touched.

Walakini wengine wasiofaa kitu wakasema, Huyu je! Atatuokoaje? Nao wakamdharau, wasimletee zawadi. 1 Samweli 10:27

But certain worthless fellows said, How shall this man save us? They despised him, and brought him no present. But he held his peace.