Sifa Lyrics

Mungu Yuko Pamoja Nasi by Sifaeli Mwabuka cover art

Sifaeli Mwabuka - Mungu Yuko Pamoja Nasi Lyrics

Artist:
Sifaeli Mwabuka

Lyrics

Nisikilize acha nikwambie
Habari za Danieli
Alimwabudu Mungu, Mungu wa mbinguni
Jehovah Rafa


Nisikilize acha nikwambie
Habari za Danieli
Alimwabudu Mungu, Mungu wa mbinguni
Jehovah Nissi


Lakini adui zake waliweka mitego mingi
Ili wamnase Danieli
Wakatunga sheria kwenda kwa mfalme
Ili wamnase Danieli


Lakini adui zake waliweka mitego mingi
Ili wamnase Danieli
Wakatunga sheria kwenda kwa mfalme
Ili wamnase Danieli


Danieli aliwauliza, nimwabudu nani?
Ooh Danieli akawauliza tena nimsifu nani?
Nisipomwabudu Mungu nimwabudu nani? Aliuliza Danieli
Nisipomwomba Mungu wangu, nimwombe nani? Jamani nauliza
Nisipomlilia Mungu wangu nimlilie nani? Aliwauliza adui wake
Nisipomwimbia baba, nimwimbie nani? Jamani niambieni


Danieli alijua yupo Mungu mtetezi wake
Adui zetu wasimame kuleta vitisho
Bado Mungu yuko na sisi


--


Video