Usiogope Maneno Yao Lyrics - Sifaeli Mwabuka
Sifaeli Mwabuka swahili
Usiogope Maneno Yao Lyrics
Usiogope maneno yao hao ni wanadamu wewe songa
Watasema yenye kukuvunja moyo wewe songa
Ijapokuwa yanaudhi sana kaza moyo mama wewe songa
Watasema wokovu gani wewe ulio nao wewe songa
Watasema tunakujua sana tulikuwa tukilewa sote, wewe songa
Maneno ya wanadamu yasikurudishe nyuma wewe songa
Maneno ya wanadamu yasikuvunjishe moyo wewe songa .
Akusimamie songa mbele
Akusimamie songa mbele
Akusimamie songa mbele
Akusimamie songa mbele .
Yesu alikuja kutafuta aliyepotea ni mimi na wewe
Tulikuwa wasinzi kweli tulikuwa waovu kweli
Tulikuwa hatueleweki machoni pa Mungu wetu .
Alipotupata tumebalika (rudia)
Tumesamehewa dhambi zetu
Tumelipiwa deni hatudaiwi tena
Tunaitwa watoto wake Baba wetu ni mmoja .
Usiogope maneno ya wanadamu usiogope
Usiogope maneno ya wanadamu usiogope
Heshimu neno la Mungu maana ndiyo yana uzima
Heshimu maneno ya Mungu maana ndiyo msaada wako .
Akusimamie songa mbele
Akusimamie songa mbele
Akusimamie songa mbele
Akusimamie songa mbele .
Wakati mwingine wanasema ili wapate sababu utawajibu nini
Wakati mwingine wanasema ili kuharibu imani yako
Wakati mwingine wanasema ili wapate sababu ya kukushitaki kwa Mungu ...
Maneno yako ya kinya chako yanakufunga mwenyewe heri unyamaze