Sifa Lyrics

Niko Hapa Baba Niguse by Sifaeli Mwabuka cover art

Sifaeli Mwabuka - Niko Hapa Baba Niguse Lyrics

Artist:
Sifaeli Mwabuka

Lyrics

Najua Baba macho yako yanaona 


Nitazame na mimi 


Najua Baba masikio yako yanasikia 


Sikia maombi yangu 


Ni wengi wamekuona Baba ukijibu 


Jibu na mimi 


Oh ni wengi wamekuona Baba ukitenda 


Tenda kwangu na mimi 


Ni wewe Mungu wangu usiyenaupendeleo 


Niguse na mimi Baba 


Ni wewe Baba usiyenaupendeleo 


Nikumbuke na mimi 


Niko hapa, niko hapa 


Niko hapa Baba uniguse 


Niko hapa, niko hapa 


Niko hapa, Baba uniguse 


Najifunza kwa wengine walionitangulia 


Nafahamu wewe unatenda 


Najifunza kwa Yakobo 


Hakukuacha Baba uende 


Aling'ang'ana na wewe 


Akasema huwezi kwenda usiponibariki 


Yakobo na aseme 


Akasema huwezi kwenda usiponiponya 


Akashika pindo lako yule mwanamke 


Na mimi niko hapa 


Niko hapa, niko hapa 


Niko hapa Baba uniponye  


Niko hapa, niko hapa 


Niko hapa Baba uniguse  


Niko hapa, niko hapa 


Niko hapa, Baba uniguse 


Video