Huniongoza

Huniongoza Lyrics

Huniongoza Mwokozi,
ndipo nami hufurahi
Niendapo pote napo,
ataniongoza papo .

Huongoza hunishika, kwa mkono wa hakika
Nitaandamana naye Kristo aniongozaye .

Pengine ni mashakani,
nami pengine rahani
Ni radhi ijayo yote,
yupo nami siku zote .

Huongoza hunishika, kwa mkono wa hakika
Nitaandamana naye Kristo aniongozaye .

Mkono akinishika,
kamwe sitanung’unika
Atachoniletea,
ni tayari kupokea .

Huongoza, hunishika kwa mkono wa hakika
Nitaandamana naye Kristu aniongozaye .

Nikiishika kazi chini,
nitakwenda huko mbinguni
Nako nitamtukuza,
Kristo aliyeniongoza .

Huongoza hunishika, kwa mkono wa hakika
Nitaandamana naye Kristo aniongozaye .

Nitaandamana naye kristo aniongozaye 
Nitaandamana naye kristo aniongozaye
Nitaandamana naye kristo aniongozaye


Top Songs United States
Share:

Write a review/comment/correct the lyrics of Huniongoza :

1 Comments/Reviews

  • Shaddy

    nazipeda Sana nyimbo zako 4 months ago