Kale nilitembea Nikilemewa dhambi
Nilikosa msaada, kuniponya mateso.
Usifiwe Msalaba! Lisifiwe kaburi!
Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!
Hata nilipofika, Mahali pa Msalaba,
Palinifaa sana, Sitasahau kamwe.
Usifiwe Msalaba! Lisifiwe kaburi!
Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!
Hicho ndicho chanzo, Cha kufurahi kwangu.
Hapo ndipo mzigo, Uliponituliwa.
Usifiwe Msalaba! Lisifiwe kaburi!
Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!
Panapo msalaba, Kinatolewa cheti,
Cha kuingia Mbinguni, Kisicho cha kanisa.
Usifiwe Msalaba Lisifiwe kaburi!
Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!
Yule Bwana mjinga, Likwenda bila cheti,
Kitumai kwingia, Kama walio nacho.
Usifiwe Msalaba Lisifiwe kaburi!
Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!
Lipofika langoni, Akaulizwa cheti,
Cha kumwonyesha Bwana, Akakutwa hanacho.
Usifiwe Msalaba Lisifiwe kaburi!
Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!
Lituhuzunishalo, Ni ninyi msio nacho,
Kuwa kama mjinga, Kwa siku ya arusi!
Usifiwe Msalaba Lisifiwe kaburi!
Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!
Ubavuni mwa Yesu, Mlitokea damu,
Chemchemi ya uzima, Itakasayo roho.
Usifiwe Msalaba Lisifiwe kaburi!
Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!
Jitahidi wingie, Damuni mwa Mwokozi,
Utafutiwa dhambi, Toka rohoni mwako.
Usifiwe Msalaba Lisifiwe kaburi!
Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!
Write a review/comment/correct the lyrics of Kale Nilitembea - Usifiwe Msalaba:
jina la bwana lihibidiwe 1 week ago
Am blessed. 5 months ago
asante kwa wimbo 1 year ago
Nimebarkiwa sanaa 1 year ago
Nakupenda bwana
1 year ago
Thanks for the Song 2 years ago
For I am not ashamed of the gospel: for it is the power of God unto salvation to every one that believeth; to the Jew first, and also to the Greek.
Galatians 6 : 14But far be it from me to glory, save in the cross of our Lord Jesus Christ, through which the world hath been crucified unto me, and I unto the world.