Amani Moyoni Mwangu Tangu Siku hiyo Aliponijia Lyrics

Swahili Songs Playlist Music Videos

Amani Moyoni Mwangu Tangu Siku hiyo Aliponijia Lyrics

Mp3 Song

Tangu siku hiyo aliponijia,
Akae moyoni mwangu.
Sina giza tena, ila mwanga pia,
Kwa Yesu, Mwokozi wangu.

Amani moyoni mwangu,
Kwa Yesu, Mwokozi wangu.
Sina shaka kamwe
Kwa sababu yeye Yu nami moyoni mwangu.

Sina haja tena ya kutanga-tanga,
Ndiye Kiongozi changu.
Dhambi zangu zote zimeondolewa,
Na Yesu Mwanawe Mungu.

Amani moyoni mwangu,
Kwa Yesu, Mwokozi wangu.
Sina shaka kamwe
Kwa sababu yeye
Yu nami moyoni mwangu.

Matumaini yangu ni ya hakika,
Katika Mwokozi wangu.
Hofu zangu na hamu zimeondoka,
Kwa kuwa ninaye Yesu.

Amani moyoni mwangu,
Kwa Yesu, Mwokozi wangu.
Sina shaka kamwe
Kwa sababu yeye...
Yu nami moyoni mwangu.

Siogopi tena nikiitwa kufa,
Yu nami daima Yesu.
Mlango wa mbingu ni Yesu Mwokozi,
’Tapita humo kwa damu.

Amani moyoni mwangu,
Kwa Yesu, Mwokozi wangu.
Sina shaka kamwe
Kwa sababu yeye...
Yu nami moyoni mwangu.

Nitaketi na Yesu huko milele,
Nimsifu Mwokozi wangu.
Nina raha moyoni majira yote,
Kwa Yesu Mwanawe Mungu.

Amani moyoni mwangu,
Kwa Yesu, Mwokozi wangu.
Sina shaka kamwe
Kwa sababu yeye...
Yu nami moyoni mwangu.


Top Songs United States
Share:

Write a review/comment/correct the lyrics of Amani Moyoni Mwangu Tangu Siku Hiyo Aliponijia:

1 Comments/Reviews

  • Ekalson Julius

    God blessed.. Shalom 3 years ago