Ni tabibu wa Karibu - imbeni malaika sifa kwa Yesu Bwana

Ni tabibu wa karibu; tabibu wa ajabu;
na rehema za daima; ni dawa yake njema.

Imbeni, malaika, sifa za Yesu Bwana;
pweke limetukuka jina lake Yesu.

Hatufai kuwa hai, wala hatutumai,
ila yeye kweli ndiye atupumzishaye.

Imbeni, malaika, sifa za Yesu Bwana;
pweke limetukuka jina lake Yesu.

Dhambi pia na hatia ametuchukulia;
Twenendeni na amani hata kwake mbinguni.

Huliona tamu jina, la Yesu kristo Bwana,
yuna sifa mwenye kufa asishindwe na kufa.

Kila mume asimame, sifa zake zivume;
Wanawake na washike kusifu jina lake.

Na vijana wote tena, wampendao sana,
waje kwake wawe wake kwa utumishi wake.Share:
1 Comments

Comments / Song Reviews

Maryann Wanjiku Muthoni Very blessing songs 2 months ago

Share your understanding & meaning of this song


Tenzi

@tenzi

Bio

Profile bio not available. Go to Artists Page to add bio & Links

Bible Verses for Ni tabibu wa Karibu - imbeni malaika sifa kwa Yesu Bwana

No verses added for this song, suggest a verse to be included in the comments section

Sifa Lyrics

Social Links