Mwokozi Umeokoa - Utukufu Halleluya (Tukutendereza Yesu in Luganda)

Nimekuwa wako wewe
Damu imenisafisha;
Sifa kwa mwana kondoo. .

Utukufu halleluya
Sifa kwa mwana Kondoo
Damu imenisafisha,
Utukufu kwa yesu .

Nilijitahidi sana
Ila sikupata raha;
Bali kwa kumtugemea
Nilipata Baraka. .

Utukufu halleluya
Sifa kwa mwana Kondoo
Damu imenisafisha,
Utukufu kwa yesu .

Diama Namwegemea,
Damu ikifanya kazi,
Nikioga kwa chemchemi
Itokayo Mwokozi. .

Utukufu halleluya
Sifa kwa mwana Kondoo
Damu imenisafisha,
Utukufu kwa yesu .

Sasa nimewekwa wakfu;
Nitaishi kwako wewe;
Fahari nashuhudia
Ya wokovu wa bure. .

Utukufu halleluya
Sifa kwa mwana Kondoo
Damu imenisafisha,
Utukufu kwa yesu .

Nasimama kwake Yesu,
Ameponya roho yangu;
Ameniondoa dhambi,
Anifanye mzima. .

Utukufu halleluya
Sifa kwa mwana Kondoo
Damu imenisafisha,
Utukufu kwa yesu .

Nalikuwa kifungoni,
Niliteswa na dhambi,
Nilifungwa minyororo,
Yesu akanifungua. .

Utukufu halleluya
Sifa kwa mwana Kondoo
Damu imenisafisha,
Utukufu kwa yesu .

Sifa ameninunua
Sifa nguvu za wokovu
Sifa Bwana huhifadhi
Sifa zake milele. .

Utukufu halleluya
Sifa kwa mwana Kondoo
Damu imenisafisha,
Utukufu kwa yesu!


Share:

Write a review of Mwokozi Umeokoa - Utukufu Halleluya (tukutendereza Yesu In Luganda):

0 Comments/Reviews


Sifa Music

@sifa-music

Bio

View all songs, albums & biography of Sifa Music

View Profile

Bible Verses for Mwokozi Umeokoa - Utukufu Halleluya (Tukutendereza Yesu in Luganda)

No verses added for this song, suggest a verse to be included in the comments section

Mp3 Songs & Download from iTunes

  • listen on Itunes Music