Nyimbo Za Kristo - Twasikia Mwito Kutoka Mbali - Tumeni Injili Lyrics
Contents:
Twasikia mwito kutoka mbali
Tumeni, Tumeni;
Roho za watu na ziokoeni,
Tumeni Tumeni.
Chorus
Tumeni nuru ya Injili,
Ing'are duniani;
Tumeni nuru ya Injili,
Ing'are duniani.
Tumeitwa kueneza Injili,
Tumeni, Tumeni;
Sadaka twaziweka msalabani,
Tumeni, Tumeni.
Na tuombe neema iendeshwe,
Tumeni, Tumeni;
Na Roho wa Kristo aonekane,
Tumeni, Tumeni.
Tusichoke kazini mwa upendo,
Tumeni, Tumeni,
Taji ya uzima tupate mwisho,
Tumeni, Tumeni.