Sifa Lyrics

46 Twae Wangu Uzima by Sifa Music cover art

Sifa Music - 46 Twae Wangu Uzima Lyrics

Artist:
Sifa Music

Lyrics

Twae wangu uzima,


Sadaka ya daima;


Twae saa na siku,


Zikutukuze huku.


Twae mikono nayo


Ifanye upendavyo,


Twae yangu miguu


Kwa wongozi wako tu.


Twae sauti yangu,


Niimbe kwa Mungu tu;


Itwae na midomo,


Ijae neno lako.


Twae dhanabu pia,


Na yote ya dunia;


Twae yangu hekima,


Upendavyo tumia.


Nia itwae, Mungu,


Haitakuwa yangu;


Twae moyo; ni wako,


Uwe makazi yako.


Twae mapenzi yangu,


Sifa za moyo wangu;


Twae kabisa nafsi


Nniwe wako halisi.


Video