Angela Chibalonza - 29 Baba yetu aliye Mbinguni (Anipenda Mwokozi Yesu) Lyrics

29 Baba yetu aliye Mbinguni (Anipenda Mwokozi Yesu) Lyrics

Baba yetu aliye mbinguni, amenifurahisha yakini,
kuniambia mwake chuoni, ya kuwa nami Yesu pendoni.

Anipenda Mwokozi Yesu, anipenda, anipenda;
Anipenda Mwokozi Yesu, anipenda mimi.

Nimuachapo kutanga mbali, yeye yu vivyo, hupenda kweli,
hunirejeza kwake moyoni; kweli yu nami Yesu pendoni.

Anipenda! Nami nampenda; kwa wokovu alionitenda;
akanifia Msalabani, kwa kuwa nami Yesu pendoni.

Haya kujua yanipa raha; kumuamini kuna furaha;
Humfukuza mara shetani, kwona yu nami Yesu Pendoni.

Sifa ni nyingi asifiwazo, moja ni sana katika hizo,
wala siachi, hata Mbinguni, kwimba, "Yu nami Yesu pendoni".


29 Baba yetu aliye Mbinguni (Anipenda Mwokozi Yesu) Video

Angela Chibalonza Songs

Related Songs