Msalaba ndio asili ya mema Lyrics

Tenzi Songs Playlist Music Videos

Msalaba ndio asili ya mema Lyrics

Mp3 Song

Sioni haya kwa Bwana,
Kwake nitang’ara!
Mti wake sitakana,
Ni neno imara.

(Chorus)
Msalaba ndio asili ya mema,
Nikatua mzigo hapo;
Nina uzima, furaha daima,
Njoni kafurahini papo.

Kama kiti chake vivyo,
Ni yake ahadi;
Alivyowekewa navyo,
Kamwe, havirudi.

Bwana wangu, tena Mungu,
Ndilo lake jina!
Hataacha roho yangu,
Wala kunikana.

Atakiri langu jina,
Mbele za Babaye,
Anipe pahali tena,
Mbinguni nikae

# At the CrossTop Songs United States
Share:

Write a review/comment/correct the lyrics of Msalaba Ndio Asili Ya Mema:

1 Comments/Reviews

  • Gillo

    it's awesome, it has no errors
    1 year ago