Lyrics
Verse 1
Wamwendea Yesu kwa kusafiwa,
na kuoshwa kwa damu ya kondoo?
je neema yake atumwagia,
tumeoshwa kwa damu ya kondoo?
Chorus (x4)
Kuoshwa, kwa damu,
itutakasayo ya kondoo;
ziwe safi nguo nyeupe mno;
umeoshwa kwa damu ya kondoo?
Verse 2
Wamwandama daima mkombozi,
na kuoshwa na damu ya kondoo?
yako kwa msulubiwa makazi,
umeoshwa kwa damu ya kondoo?
Verse 3
Atakapokuja Bwana-arusi,
Uwe safi kwa damu ya kondoo!
Yafae kwenda mbinguni mavazi,
Yafuliwe kwa damu ya kondoo.
Verse 4
Yatupwe yaliyo na takataka,
na uoshwe kwa damu ya kondoo.
Huoni kijito chatiririka,
na uoshwe kwa damu ya kondoo?
Credits & Song Information
Video
Meaning & Inspiration
Katika rekodi hii, Angela Chibalonza anaimba wimbo wa mwaliko unaouliza ikiwa msikilizaji amemwendea Yesu kwa kusafishwa. Mistari na kiitikio vinarudia picha ya kuoshwa kwa damu ya Kondoo, mavazi safi, na kujiandaa kwa kuja kwa Bwana-arusi.