MAMBO YANABADILIKA - Naona Mambo Yakibadilika Lyrics - Hellen Ken

Hellen Ken swahili

Chorus:
Naona mambo yakibadilika
Yabidilika kwa wema wako
Mambo, mambo yabadilika
#MamboYanabadilika

MAMBO YANABADILIKA - Naona Mambo Yakibadilika Video

Buy/Download Audio

MAMBO YANABADILIKA - Naona Mambo Yakibadilika Lyrics

Huu, ni mwaka wa urejesho
Mambo, mambo yabadilika

Naona mambo yakibadilika
Yabidilika kwa wema wako
Naona mambo yakibadilika
Yabidilika kwa wema wako

Mambo, mambo yabadilika
Walio chini sasa, naona wakiinuliwa
Walio nyuma sasa, naona wakiwa mbele
Wanaodharauliwa, naona heshima zao
Wanaolia sasa, machozi yanapanguzwa

Huu ni mwaka wa urejesho
Uliyepoteza ndoa, naona ikirejeshwa
Uliyepoteza watoto, naona wakirejeshwa
Uliyepoteza nyumba, naona ikirejeshwa
Uliyepoteza kazi, naona ikirejeshwa
Uliyepoteza cheo, naona kikirejeshwa
Uliyepoteza heshima, naona ikirejea
Kwani mambo yabadilika

Naona mambo yakibadilika
Yabidilika kwa wema wako
Naona mambo yakibadilika
Yabidilika kwa wema wako

Majina yaenda kubadilika
Wanaoitwa tasa, naona wakiitwa mama
Wanaodharauliwa, naona heshima zao
Wanaoitwa duni, sasa wainuliwa
Walio pekee yao, waenda pata wachumba
Kwani mambo, mambo yabadilika

Wanaolia sasa, machozi wanapanguza
Waliokataliwa, sasa wakubalika
Wasio na makao, wapata makao yao
Wasio na amani, wapata amani yao
Wasio na furaha, wapata furaha yao
Kwani mambo, mambo yabadilika

Naona mambo yakibadilika
Yabidilika kwa wema wako
Naona mambo yakibadilika
Yabidilika kwa wema wako

Jipe jina, tutakuita unapojiita sasa
Pokea jina jipya, maana majina yabadilika

Refrain: Naitwa mbarikiwa
Tukuite nani nani leo
Jipe jina, jipe jine
Na wewe waitwa nani leo
Baba yangu tukuite nani

Naona mambo yakibadilika
Yabidilika kwa wema wako
Jipe jina, jipe jina