1.Yesu kwetu ni rafiki, Huambiwa haja pia;
Tukiomba kwa Babaye Maombi asikia;
Lakini twajikosesha, Twajitweka vibaya;
Kwamba tulimwomba Mungu Dua angesikia.
2. Una dhiki na maonjo? Una mashaka pia.
Haifai kufa moyo, Dua atasikia
Hakuna mwingine mwema Wa kutuhurumia;
Atujua tu dhaifu; Maombi asikia.
3. Je, hunayo hata nguvu, Huwezi kuendelea,
Ujapodharauliwa Ujaporushwa pia, Watu wange kudharau,
Wapendao dunia, Hukwambata mikononi, Dua atasikia.