Hope Samwel - 27 Mungu ni pendo Lyrics

27 Mungu ni pendo Lyrics

Mungu ni pendo apenda watu,
Mungu ni pendo anipenda

Sikilizeni furaha yangu,
Mungu ni pendo, anipenda

Nilipotea katika dhambi,
nikawa mtumwa wa shetani

Sikilizeni furaha yangu,
Mungu ni pendo, anipenda

Akaja Yesu kuniokoa,
yeye kanipa kuwa huru
Sikilizeni furaha yangu,
Mungu ni pendo, anipenda

Sababu hii namtumikia,
namsifu yeye siku zote.
Sikilizeni furaha yangu,
Mungu ni pendo, anipenda



27 Mungu ni pendo Video

Hope Samwel Songs

Related Songs