Sifa Lyrics

Msalabani pa Mwokozi by Daudi Petro cover art

Daudi Petro - Msalabani pa Mwokozi Lyrics

Artist:
Daudi Petro

Lyrics

Verse 1


Msalabani pa mwokozi, hapo niliomba upozi,

akaniokoa mpenzi, mwana wa Mungu.


Chorus


Mwana wa Mungu, mwokozi wangu,

akaniokoa mpenzi, mwana wa Mungu


Verse 2


Chini ya mti msumbufu, niliomba utakatifu,

alinikomboa kwa damu, mwana wa Mungu.


Verse 3


Aliniokoa dhambini, ikawa kunikaa ndani,

aliponifia mtini, mwana wa Mungu.


Verse 4


Damu ya Yesu ya thamani, huniokoa makosani,

huniendesha wokovuni, mwana wa Mungu.


Verse 5


Hicho kijito cha gharama, leo jivike kwa kuzama,

kwake uuone uzima, mwana wa Mungu.


Credits & Song Information

Writer
E. A. Hoffman
Source verified · Delight Music Centre (Bandcamp)

Add song information · Add a supporting source

Video

Meaning & Inspiration

Katika rekodi hii, Daudi Petro anaimba Tenzi za Rohoni Na. 77 kama ushuhuda wa kumwelekea Mwokozi msalabani. Mistari inaunganisha ombi la uponyaji na utakatifu na shukrani kwa ukombozi, huku kiitikio kikisisitiza kwamba tumaini la mwimbaji limo kwa Mwana wa Mungu.