1
Yesu ameniokoa, amenipa utulivu.
(Jesus has saved me, he has given me peace)
Kwake ninaona raha, ninataka kumsifu.
(I see pleasure in him, I want to praise him)
Haleluya, haleluya! Nimefika bandarini.
(Hallelujah, hallelujah! I have arrived at the port)
Haleluya, haleluya! Jina lake ni mnara.
(Hallelujah, hallelujah! Its name is a tower)
2
Kwa furaha ninaimba wimbo mpya wa wokovu.
(With joy I sing a new song of salvation)
Nisichoke kamwe hapa kumwimbia Mkombozi.
(May I never get tired of singing to Mkombozi here)
3
Ni habari za neema zakupasha pande zote.
(It is news of grace that warmed all around)
Mhubiri, enda mbio kufikia nchi zote!
(Preacher, run to reach all countries)
4
Yesu, siku nita’kufa na maisha ni tayari,
(Jesus, the day I die and life is ready)
‘nichukue kwako juu penye raha ya milele!
(Take me up to you where there is eternal pleasure)