Sifa Lyrics

Kitambo Bado by PaPi Clever & Dorcas cover art

PaPi Clever & Dorcas - Kitambo Bado Lyrics

Artist:
PaPi Clever & Dorcas
Album:
Pamoja Na Wewe
Official Release:
09 Apr 2024

Lyrics

Kitambo bado-vita itaisha, kitambo, na dhoruba zitapoa
Na tena nitalaza kichwa changu mbavuni mwake anayenipenda

Nitaziona raha na amani, mbinguni hazitakuwapo dhambi

Kitambo bado- roho yaumizwa, kitambo katika usiku huku
Machozi nina’toka mara nyingi sababu sijaona bado Yesu

Lakini asubuhi ya milele huko mbinguni sitalia tena

Kitambo bado ya kuchoka huku, kitambo, tena nitaona Yesu
Na huru mbali na hatari zote nitastarehe mikononi mwake

Uvuli wote utaondolewa kwa nuru huko kamilifu kweli

Mateso yangu hayadhuru tena, nitasahau yote kwa Yesu
Nikisumbuka mda duniani, mbinguni sitaona shida, kufa

Na Mungu atafuta kila chozi, ataondoa maumivu yote

Video