Sifa Lyrics

Kile Unachopanda by Reuben Kigame + Sifa Voices cover art

Reuben Kigame + Sifa Voices - Kile Unachopanda Lyrics

Artist:
Reuben Kigame + Sifa Voices

Lyrics

Watu wengi wanapanda 


Mbegu nyingi duniani 


Bila hata kuchunguza 


Ili wafahamu yakuwa 


Yale mavuno yatakayotoka 


Yote ni yao ooh kabisa x2 


Bwana Mungu Hubariki 


Wale wote humfwata 


Na kupanda mbegu nzuri 


Hao maisha yao ni mema 


Ukiwachunguza kwa makina 


Utaona aah baraka 


Kile unachopanda 


Ndicho utakachovuna X2 


Sababu Mungu wetu hadanganyiki x2 


Hata kidogo 


Kile unachopanda ndicho utakachovuna 


Mungu hadanganyiki wala hadhihakiwi 


Reuben Kigame


Ukipanda mbegu mbaya utavuna mavuno maovu


Mimi nimejifunza ninapanda mbegu za baraka yeyoo 


Sifa Voices


Kile unachopanda ndicho utakachovuna 


Mungu hadanganyiki wala hadhihakiwi 


Reuben Kigame 


Chunga chunga sana ni mbegu gani unapanda 


Kama mbegu ni mbaya utavuna mavuno maovu


Sifa Voices


Kile unachopanda ndicho utakachovuna 


Mungu hadanganyiki wala hadhihakiwi 


[Instrumental]


"Panda mbegu nzuri kaka utavuna" 


Kile unachopanda ndicho utakachovuna 


Mungu hadanganyiki wala hadhihakiwi 


(Repeat from verse)


Video