Kutoka 12 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kutoka 12 (Swahili) Exodus 12 (English)

Bwana akanena na Musa na Haruni katika nchi ya Misri, akawaambia, Kutoka 12:1

Yahweh spoke to Moses and Aaron in the land of Egypt, saying,

Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu. Kutoka 12:2

"This month shall be to you the beginning of months. It shall be the first month of the year to you.

Semeni na mkutano wote wa Israeli, mkawaambie, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana-kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana-kondoo kwa watu wa nyumba moja; Kutoka 12:3

Speak to all the congregation of Israel, saying, 'On the tenth day of this month, they shall take to them every man a lamb, according to their fathers' houses, a lamb for a household;

na ikiwa watu wa nyumba ni wachache kwa mwana-kondoo, basi yeye na jirani yake aliye karibu na nyumba yake na watwae mwana-kondoo mmoja, kwa kadiri ya hesabu ya watu; kwa kadiri ya ulaji wa kila mtu, ndivyo mtakavyofanya hesabu yenu kwa yule mwana-kondoo. Kutoka 12:4

and if the household be too little for a lamb, then he and his neighbor next to his house shall take one according to the number of the souls; according to what everyone can eat you shall make your count for the lamb.

Mwana-kondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi. Kutoka 12:5

Your lamb shall be without blemish, a male a year old. You shall take it from the sheep, or from the goats:

Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule; na kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioni. Kutoka 12:6

and you shall keep it until the fourteenth day of the same month; and the whole assembly of the congregation of Israel shall kill it at evening.

Nao watatwaa baadhi ya damu yake na kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu, katika zile nyumba watakazomla. Kutoka 12:7

They shall take some of the blood, and put it on the two side-posts and on the lintel, on the houses in which they shall eat it.

Watakula nyama yake usiku ule ule, imeokwa motoni, pamoja na mkate usiotiwa chachu; tena pamoja na mboga zenye uchungu. Kutoka 12:8

They shall eat the flesh in that night, roasted with fire, and unleavened bread. They shall eat it with bitter herbs.

Msiile mbichi, wala ya kutokoswa majini, bali imeokwa motoni; kichwa chake pamoja na miguu yake, na nyama zake za ndani. Kutoka 12:9

Don't eat it raw, nor boiled at all with water, but roasted with fire; with its head, its legs and its inner parts.

Wala msisaze kitu chake cho chote hata asubuhi, bali kitu kitakachosalia hata asubuhi mtakichoma kwa moto. Kutoka 12:10

You shall let nothing of it remain until the morning; but that which remains of it until the morning you shall burn with fire.

Tena mtamla hivi; mtakuwa mmefungwa viuno vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; ni pasaka ya Bwana. Kutoka 12:11

This is how you shall eat it: with your loins girded, your shoes on your feet, and your staff in your hand; and you shall eat it in haste: it is Yahweh's Passover.

Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi Bwana. Kutoka 12:12

For I will go through the land of Egypt in that night, and will strike all the firstborn in the land of Egypt, both man and animal. Against all the gods of Egypt I will execute judgments: I am Yahweh.

Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri. Kutoka 12:13

The blood shall be to you for a token on the houses where you are: and when I see the blood, I will pass over you, and there shall no plague be on you to destroy you, when I strike the land of Egypt.

Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa Bwana; mtaifanya iwe sikukuu katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele Kutoka 12:14

This day shall be to you for a memorial, and you shall keep it a feast to Yahweh: throughout your generations you shall keep it a feast by an ordinance forever.

Mtakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba; siku hiyo ya kwanza mtaondoa chachu yote isiwe katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu ye yote atakayekula mkate uliochachwa tangu siku hiyo ya kwanza hata siku ya saba, nafsi hiyo atakatiliwa mbali na Israeli. Kutoka 12:15

Seven days shall you eat unleavened bread; even the first day you shall put away yeast out of your houses, for whoever eats leavened bread from the first day until the seventh day, that soul shall be cut off from Israel.

Siku ya kwanza kutakuwa kwenu na kusanyiko takatifu, na siku ya saba kutakuwa kusanyiko takatifu; haitafanywa kazi yo yote katika siku hizo, isipokuwa kwa hiyo ambayo kila mtu hana budi kula, hiyo tu ifanyike kwenu. Kutoka 12:16

In the first day there shall be to you a holy convocation, and in the seventh day a holy convocation; no manner of work shall be done in them, except that which every man must eat, that only may be done by you.

Nanyi mtaitunza ile sikukuu ya mikate isiyochachwa; kwa kuwa katika siku iyo hiyo mimi nimeyatoa majeshi yenu katika nchi ya Misri; kwa hiyo mtaitunza siku hiyo katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele. Kutoka 12:17

You shall observe the feast of unleavened bread; for in this same day have I brought your hosts out of the land of Egypt: therefore shall you observe this day throughout your generations by an ordinance forever.

Mwezi wa kwanza, siku ya mwezi kumi na nne, wakati wa jioni, mtakula mikate isiyochachwa, hata siku ya mwezi ishirini na moja jioni. Kutoka 12:18

In the first month, on the fourteenth day of the month at evening, you shall eat unleavened bread, until the twenty first day of the month at evening.

Muda wa siku saba isionekane chachu katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu ye yote atakayekula hiyo iliyotiwa chachu, nafsi hiyo atakatiliwa mbali na mkutano wa Israeli, akiwa mwenye kukaa hali ya ugeni, au akiwa mtu aliyezaliwa katika nchi. Kutoka 12:19

Seven days shall there be no yeast found in your houses, for whoever eats that which is leavened, that soul shall be cut off from the congregation of Israel, whether he be a foreigner, or one who is born in the land.

Msile kitu chochote kilichochachwa; mtakula mikate isiyochachwa katika makao yenu yote. Kutoka 12:20

You shall eat nothing leavened. In all your habitations you shall eat unleavened bread.'"

Hapo ndipo Musa akawaita wazee wa Israeli, na kuwaambia, Nendeni, mkajitwalie wana-kondoo kama jamaa zenu zilivyo mkamchinje pasaka. Kutoka 12:21

Then Moses called for all the elders of Israel, and said to them, "Draw out, and take lambs according to your families, and kill the Passover.

Nanyi twaeni tawi la hisopu, mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu ye yote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi. Kutoka 12:22

You shall take a bunch of hyssop, and dip it in the blood that is in the basin, and strike the lintel and the two side-posts with the blood that is in the basin; and none of you shall go out of the door of his house until the morning.

Kwa kuwa Bwana atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, Bwana atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi. Kutoka 12:23

For Yahweh will pass through to strike the Egyptians; and when he sees the blood on the lintel, and on the two side-posts, Yahweh will pass over the door, and will not allow the destroyer to come in to your houses to strike you.

Nanyi mtalitunza jambo hili kuwa ni amri kwako na kwa wanao milele. Kutoka 12:24

You shall observe this thing for an ordinance to you and to your sons forever.

Itakuwa hapo mtakapoifikilia hiyo nchi, Bwana atakayowapa, kama alivyoahidi, ndipo mtakapoushika utumishi huu. Kutoka 12:25

It shall happen when you have come to the land which Yahweh will give you, according as he has promised, that you shall keep this service.

Kisha itakuwa, hapo watoto wenu watakapowauliza, N'nini maana yake utumishi huu kwenu? Kutoka 12:26

It will happen, when your children ask you, 'What do you mean by this service?'

Ndipo mtawaambia, Ni dhabihu ya pasaka ya Bwana, kwa kuwa alipita juu ya nyumba za wana wa Israeli huko Misri, hapo alipowapiga Wamisri, akaziokoa nyumba zetu. Hao watu wakainama vichwa na kusujudia. Kutoka 12:27

that you shall say, 'It is the sacrifice of Yahweh's Passover, who passed over the houses of the children of Israel in Egypt, when he struck the Egyptians, and spared our houses.'" The people bowed their heads and worshiped.

Basi wana wa Israeli wakaenda na kufanya mambo hayo; vile vile kama Bwana alivyowaamuru Musa na Haruni, ndivyo walivyofanya. Kutoka 12:28

The children of Israel went and did so; as Yahweh had commanded Moses and Aaron, so they did.

Hata ikawa, usiku wa manane Bwana akawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, tangu mzaliwa wa kwanza wa Farao aliyeketi katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa mtu aliyefungwa katika nyumba ya wafungwa; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama. Kutoka 12:29

It happened at midnight, that Yahweh struck all the firstborn in the land of Egypt, from the firstborn of Pharaoh who sat on his throne to the firstborn of the captive who was in the dungeon; and all the firstborn of cattle.

Farao akaondoka usiku, yeye na watumishi wake wote, na Wamisri wote; pakawa na kilio kikuu katika Misri; maana hapakuwa na nyumba hata moja asimokufa mtu. Kutoka 12:30

Pharaoh rose up in the night, he, and all his servants, and all the Egyptians; and there was a great cry in Egypt, for there was not a house where there was not one dead.

Akawaita Musa na Haruni usiku, akasema, Ondokeni tokeni katika watu wangu, ninyi na wana wa Israeli; enendeni, kamtumikieni Bwana kama mlivyosema. Kutoka 12:31

He called for Moses and Aaron by night, and said, "Rise up, get out from among my people, both you and the children of Israel; and go, serve Yahweh, as you have said!

Twaeni kondoo zenu na ng'ombe zenu kama mlivyosema, enendeni zenu, mkanibariki mimi pia. Kutoka 12:32

Take both your flocks and your herds, as you have said, and be gone; and bless me also!"

Wamisri nao wakawahimiza watu, kuwatoa katika nchi kwa haraka, maana walisema, Tumekwisha kufa sote. Kutoka 12:33

The Egyptians were urgent with the people, to send them out of the land in haste, for they said, "We are all dead men."

Watu wakauchukua unga wa mikate yao kabla haijatiwa chachu, na vyombo vyao vya kukandia wakavitia ndani ya nguo zao mabegani. Kutoka 12:34

The people took their dough before it was leavened, their kneading-troughs being bound up in their clothes on their shoulders.

Wana wa Israeli wakafanya kama neno lile la Musa; wakataka kwa Wamisri vyombo vya fedha na vyombo vya dhahabu, na mavazi. Kutoka 12:35

The children of Israel did according to the word of Moses; and they asked of the Egyptians jewels of silver, and jewels of gold, and clothing.

Bwana akawajalia kupendelewa na Wamisri hata wakawapa kila walichokitaka. Nao wakawateka Wamisri nyara. Kutoka 12:36

Yahweh gave the people favor in the sight of the Egyptians, so that they let them have what they asked. They despoiled the Egyptians.

Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi mpaka Sukothi, walipata hesabu yao kama watu sita mia elfu watu waume waliokwenda kwa miguu, bila kuhesabu watoto. Kutoka 12:37

The children of Israel traveled from Rameses to Succoth, about six hundred thousand on foot who were men, besides children.

Na kundi kubwa la watu waliochangamana mno wakakwea pamoja nao; na kondoo na ng'ombe, wanyama wengi sana. Kutoka 12:38

A mixed multitude went up also with them, with flocks, herds, and even very much cattle.

Nao wakaoka mikate isiyochachwa ya ule unga waliouchukua walipotoka Misri, maana, haukutiwa chachu, kwa sababu walitolewa watoke Misri, wasiweze kukawia, nao walikuwa hawajajifanyia tayari chakula. Kutoka 12:39

They baked unleavened cakes of the dough which they brought forth out of Egypt; for it wasn't leavened, because they were thrust out of Egypt, and couldn't wait, neither had they prepared for themselves any food.

Basi wana wa Israeli kukaa kwao, maana, muda waliokaa ndani ya Misri, ulikuwa ni miaka mia nne na thelathini. Kutoka 12:40

Now the time that the children of Israel lived in Egypt was four hundred thirty years.

Ilikuwa mwisho wa miaka hiyo mia nne na thelathini, ilikuwa siku ile ile, ya kwamba majeshi yote ya Bwana yalitoka nchi ya Misri. Kutoka 12:41

It happened at the end of four hundred thirty years, even the same day it happened, that all the hosts of Yahweh went out from the land of Egypt.

Ni usiku wa kuangaliwa sana mbele za Bwana kwa sababu ya kuwatoa katika nchi ya Misri; huu ndio usiku wa Bwana, ambao wapasa kuangaliwa sana na wana wa Israeli wote katika vizazi vyao. Kutoka 12:42

It is a night to be much observed to Yahweh for bringing them out from the land of Egypt. This is that night of Yahweh, to be much observed of all the children of Israel throughout their generations.

Bwana akawaambia Musa na Haruni, Amri ya pasaka ni hii; mtu mgeni asimle; Kutoka 12:43

Yahweh said to Moses and Aaron, "This is the ordinance of the Passover. There shall no foreigner eat of it,

lakini mtumishi wa mtu awaye yote aliyenunuliwa kwa fedha, ukiisha kumtahiri, ndipo hapo atamla pasaka. Kutoka 12:44

but every man's servant who is bought for money, when you have circumcised him, then shall he eat of it.

Akaaye kwenu hali ya ugeni, na mtumishi aliyeajiriwa, wasimle pasaka. Kutoka 12:45

A foreigner and a hired servant shall not eat of it.

Na aliwe ndani ya nyumba moja; usiichukue nje ya nyumba nyama yake yo yote; wala msivunje mfupa wake uwao wote. Kutoka 12:46

In one house shall it be eaten; you shall not carry forth anything of the flesh abroad out of the house; neither shall you break a bone of it.

Na wafanye jambo hili mkutano wa Israeli wote. Kutoka 12:47

All the congregation of Israel shall keep it.

Na mgeni atakapoketi pamoja nawe, na kupenda kumfanyia Bwana pasaka, waume wake wote na watahiriwe, ndipo hapo akaribie na kufanya pasaka; naye atakuwa mfano mmoja na mtu aliyezaliwa katika nchi; lakini mtu ye yote asiyetahiriwa asimle. Kutoka 12:48

When a stranger shall live as a foreigner with you, and will keep the Passover to Yahweh, let all his males be circumcised, and then let him come near and keep it; and he shall be as one who is born in the land: but no uncircumcised person shall eat of it.

Sheria ni hiyo moja kwa mtu aliyezaliwa kwenu, na kwa mgeni akaaye kati yenu ugenini. Kutoka 12:49

One law shall be to him who is born at home, and to the stranger who lives as a foreigner among you."

Ndivyo walivyofanya wana wa Israeli wote; kama Bwana alivyowaagiza Musa na Haruni, ndivyo walivyofanya. Kutoka 12:50

Thus did all the children of Israel. As Yahweh commanded Moses and Aaron, so they did.

Ilikuwa siku ile ile moja, Bwana akawatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri kwa majeshi yao.

Kutoka 12:51

It happened the same day, that Yahweh brought the children of Israel out of the land of Egypt by their hosts.