Kutoka 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kutoka 5 (Swahili) Exodus 5 (English)

Hata baadaye, Musa na Haruni wakaenda wakamwambia Farao, wakasema, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Wape watu wangu ruhusa waende, ili kunifanyia sikukuu jangwani. Kutoka 5:1

Afterward Moses and Aaron came, and said to Pharaoh, "This is what Yahweh, the God of Israel, says, 'Let my people go, that they may hold a feast to me in the wilderness.'"

Farao akasema, Bwana ni nani, hata niisikilize sauti yake, na kuwapa Israeli ruhusa waende zao? Mimi simjui Bwana, wala sitawapa Israeli ruhusa waende zao. Kutoka 5:2

Pharaoh said, "Who is Yahweh, that I should listen to his voice to let Israel go? I don't know Yahweh, and moreover I will not let Israel go."

Wakasema, Mungu wa Waebrania amekutana nasi; twakuomba, tupe ruhusa twende safari ya siku tatu jangwani, tumtolee dhabihu Bwana, Mungu wetu; asije akatupiga kwa tauni, au kwa upanga. Kutoka 5:3

They said, "The God of the Hebrews has met with us. Please let us go three days' journey into the wilderness, and sacrifice to Yahweh, our God, lest he fall on us with pestilence, or with the sword."

Mfalme wa Misri akawaambia Enyi Musa na Haruni, mbona mnawaachisha watu kazi zao? Enendeni zenu kwa mizigo yenu. Kutoka 5:4

The king of Egypt said to them, "Why do you, Moses and Aaron, take the people from their work? Get back to your burdens!"

Kisha Farao akasema, Tazameni, watu wa nchi sasa ni wengi, nanyi mnawapumzisha, wasichukue mizigo yao. Kutoka 5:5

Pharaoh said, "Behold, the people of the land are now many, and you make them rest from their burdens."

Na siku ile ile Farao akawaamuru wasimamizi wa watu, na wanyapara wao, akisema, Kutoka 5:6

The same day Pharaoh commanded the taskmasters of the people, and their officers, saying,

Msiwape watu tena majani ya kufanyia matofali, kama mlivyofanya tangu hapo; na waende wakatafute majani wenyewe. Kutoka 5:7

"You shall no longer give the people straw to make brick, as before. Let them go and gather straw for themselves.

Lakini hesabu ya matofali waliyokuwa wakifanya tokea hapo, wawekeeni iyo hiyo, msiipunguze hata kidogo, kwa maana ni wavivu hao; kwa hiyo wanapiga kelele, wakisema, Tupe ruhusa twende kumtolea Mungu wetu dhabihu. Kutoka 5:8

The number of the bricks, which they made before, you require from them. You shall not diminish anything of it, for they are idle; therefore they cry, saying, 'Let us go and sacrifice to our God.'

Wapeni watu hao kazi nzito zaidi, waitaabikie; wala wasiangalie maneno ya uongo. Kutoka 5:9

Let heavier work be laid on the men, that they may labor therein; and don't let them pay any attention to lying words."

Hao wasimamizi wa watu na wanyapara wao wakatoka, wakasema na watu, wakanena, Farao asema hivi, Mimi siwapi majani. Kutoka 5:10

The taskmasters of the people went out, and their officers, and they spoke to the people, saying, This is what Pharaoh says: "I will not give you straw.

Enendeni wenyewe, jipatieni majani hapo mtakapoyaona; kwa maana kazi yenu haitapunguzwa hata kidogo. Kutoka 5:11

Go yourselves, get straw where you can find it, for nothing of your work shall be diminished."

Basi hao watu wakatawanyika katika nchi yote ya Misri ili wapate kukusanya matakataka ya mashamba badala ya majani. Kutoka 5:12

So the people were scattered abroad throughout all the land of Egypt to gather stubble for straw.

Wasimamizi wao wakawahimiza, wakisema, Timizeni kazi zenu, shughuli zenu za kila siku, kama wakati ule majani yalipokuwapo. Kutoka 5:13

The taskmasters were urgent saying, "Fulfill your work quota daily, as when there was straw!"

Na wanyapara wa wana wa Israeli, ambao wasimamizi wa Farao wamewaweka juu yao, wakapigwa, wakiambiwa, Kwa nini hamkutimiza kazi yenu jana na leo; kwa kufanya matofali kama hapo kwanza? Kutoka 5:14

The officers of the children of Israel, whom Pharaoh's taskmasters had set over them, were beaten, and demanded, "Why haven't you fulfilled your quota both yesterday and today, in making brick as before?"

Basi wanyapara wa wana wa Israeli wakaenda, wakamlilia Farao, wakisema, Mbona umetutendea hivi, sisi watumwa wako? Kutoka 5:15

Then the officers of the children of Israel came and cried to Pharaoh, saying, "Why do you deal this way with your servants?

Watumwa wako hawapewi majani, nao wanatuambia, Fanyeni matofali; na tazama, watumwa wako wapigwa; lakini kosa hilo ni la watu wako mwenyewe. Kutoka 5:16

No straw is given to your servants, and they tell us, 'Make brick!' and, behold, your servants are beaten; but the fault is in your own people."

Akasema, Wavivu ninyi; wavivu; kwa ajili hii mwasema, Tupe ruhusa twende kumtolea Bwana dhabihu. Kutoka 5:17

But he said, "You are idle! You are idle! Therefore you say, 'Let us go and sacrifice to Yahweh.'

Basi, enendeni sasa, mkafanye kazi; kwa maana hamtapewa majani, na pamoja na hayo mtaleta hesabu ile ile ya matofali. Kutoka 5:18

Go therefore now, and work, for no straw shall be given to you, yet shall you deliver the same number of bricks!"

Basi wanyapara wa wana wa Israeli wakaona ya kwamba wa katika hali mbaya, walipoambiwa, Hamtapunguza hesabu ya matofali yenu hata kidogo; ndizo shughuli zenu za kila siku. Kutoka 5:19

The officers of the children of Israel saw that they were in trouble, when it was said, "You shall not diminish anything from your daily quota of bricks!"

Wakakutana na Musa na Haruni, waliokuwa wanasimama njiani, hapo walipotoka kwa Farao; Kutoka 5:20

They met Moses and Aaron, who stood in the way, as they came forth from Pharaoh:

wakawaambia, Bwana awaangalie na kuamua; kwa kuwa mmefanya harufu yetu kuwa chukizo mbele ya Farao, na mbele ya watumishi wake, mkatia upanga mikononi mwao, watuue. Kutoka 5:21

and they said to them, "May Yahweh look at you, and judge, because you have made us a stench to be abhorred in the eyes of Pharaoh, and in the eyes of his servants, to put a sword in their hand to kill us."

Musa akarudi kwa Bwana, akasema, Bwana, mbona umewatenda mabaya watu hawa? Kwani kunituma mimi? Kutoka 5:22

Moses returned to Yahweh, and said, "Lord, why have you brought trouble on this people? Why is it that you have sent me?

Kwa maana tangu nilipokwenda kwa Farao, kusema naye kwa jina lako, amewatenda mabaya watu hawa; wala hukuwaokoa watu wako hata kidogo.

Kutoka 5:23

For since I came to Pharaoh to speak in your name, he has brought trouble on this people; neither have you delivered your people at all."