Kutoka 8 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kutoka 8 (Swahili) Exodus 8 (English)

Bwana akamwambia Musa, Ingia kwa Farao, ukamwambie, Bwana asema hivi, Wape watu wangu ruhusa, ili wapate kunitumikia. Kutoka 8:1

Yahweh spoke to Moses, Go in to Pharaoh, and tell him, "This is what Yahweh says, 'Let my people go, that they may serve me.

Tena kama ukikataa kuwapa ruhusa, tazama, nitaipiga mipaka yako yote kwa kuleta vyura; Kutoka 8:2

If you refuse to let them go, behold, I will plague all your borders with frogs:

na huo mto utafurika vyura, nao watakwea juu na kuingia ndani ya nyumba yako, na ndani ya chumba chako cha kulala, na juu ya kitanda chako, na ndani ya nyumba ya watumishi wako, na juu ya watu wako, na ndani ya meko yako, na ndani ya vyombo vyako vya kukandia unga. Kutoka 8:3

and the river shall swarm with frogs, which shall go up and come into your house, and into your bedchamber, and on your bed, and into the house of your servants, and on your people, and into your ovens, and into your kneading-troughs:

Kisha hao vyura watakwea juu yako wewe, na juu ya watu wako, na juu ya watumishi wako wote. Kutoka 8:4

and the frogs shall come up both on you, and on your people, and on all your servants.'"

Bwana akamwambia Musa, Mwambie Haruni, Nyosha mkono wako na fimbo yako juu ya mito, juu ya vijito, na juu ya maziwa ya maji, ukawalete vyura waje juu ya nchi yote ya Misri. Kutoka 8:5

Yahweh said to Moses, "Tell Aaron, 'Stretch forth your hand with your rod over the rivers, over the streams, and over the pools, and cause frogs to come up on the land of Egypt.'"

Basi Haruni akaunyosha mkono wake juu ya maji yote ya Misri; na hao vyura wakakwea juu, wakaifunika nchi ya Misri. Kutoka 8:6

Aaron stretched out his hand over the waters of Egypt; and the frogs came up, and covered the land of Egypt.

Waganga nao wakafanya mfano wa hayo kwa uganga wao; na kuwaleta vyura juu ya nchi ya Misri. Kutoka 8:7

The magicians did in like manner with their enchantments, and brought up frogs on the land of Egypt.

Ndipo Farao akawaita Musa na Haruni na kuwaambia, Mwombeni Bwana, ili awaondoe vyura hawa kwangu mimi na kwa watu wangu; nami nitawapa watu ruhusa waende zao, ili wamtolee Bwana dhabihu. Kutoka 8:8

Then Pharaoh called for Moses and Aaron, and said, "Entreat Yahweh, that he take away the frogs from me, and from my people; and I will let the people go, that they may sacrifice to Yahweh."

Musa akamwambia Farao, Haya, ujitukuze juu yangu katika jambo hili; sema ni lini unapotaka nikuombee wewe, na watumishi wako, na watu wako, ili hao vyura waangamizwe watoke kwako wewe na nyumba zako, wakae ndani ya mto tu. Kutoka 8:9

Moses said to Pharaoh, "I give you the honor of setting the time that I should pray for you, and for your servants, and for your people, that the frogs be destroyed from you and your houses, and remain in the river only."

Akamwambia, Kesho, Akasema, Na yawe kama neno lako; ili upate kujua ya kwamba hapana mwingine mfano wa Bwana, Mungu wetu. Kutoka 8:10

He said, "Tomorrow." He said, "Be it according to your word, that you may know that there is none like Yahweh our God.

Hao vyura wataondoka kutoka kwako wewe na nyumba zako, na watumishi wako, na watu wako; watasalia mtoni tu. Kutoka 8:11

The frogs shall depart from you, and from your houses, and from your servants, and from your people. They shall remain in the river only."

Basi Musa na Haruni wakatoka kwa Farao; Musa akamlilia Bwana katika jambo la hao vyura aliokuwa amewaleta juu ya Farao. Kutoka 8:12

Moses and Aaron went out from Pharaoh, and Moses cried to Yahweh concerning the frogs which he had brought on Pharaoh.

Bwana akafanya sawasawa na neno la Musa; na hao vyura wakafa kutoka katika zile nyumba, na katika viwanja, na katika mashamba. Kutoka 8:13

Yahweh did according to the word of Moses, and the frogs died out of the houses, out of the courts, and out of the fields.

Wakawakusanya chungu chungu; na nchi ikatoa uvundo. Kutoka 8:14

They gathered them together in heaps, and the land stank.

Lakini Farao alipoona ya kuwa pana nafuu, akaufanya moyo wake kuwa mzito, asiwasikize; kama Bwana alivyonena. Kutoka 8:15

But when Pharaoh saw that there was a respite, he hardened his heart, and didn't listen to them, as Yahweh had spoken.

Bwana akamwambia Musa, Mwambie Haruni, Nyosha fimbo yako, ukayapige mavumbi ya nchi, ili kwamba yawe chawa katika nchi yote ya Misri. Kutoka 8:16

Yahweh said to Moses, "Tell Aaron, 'Stretch out your rod, and strike the dust of the earth, that it may become lice throughout all the land of Egypt.'"

Nao wakafanya; Haruni akaunyosha mkono wake na fimbo yake, na kuyapiga mavumbi ya nchi, nayo yakawa chawa juu ya wanadamu na juu ya wanyama; mavumbi yote ya nchi yakawa ni chawa katika nchi yote ya Misri. Kutoka 8:17

They did so; and Aaron stretched out his hand with his rod, and struck the dust of the earth, and there were lice on man, and on animal; all the dust of the earth became lice throughout all the land of Egypt.

Hao waganga nao wakafanya mfano wa hayo kwa uganga wao, ili kwamba walete chawa, lakini wasiweze; nako kulikuwa na chawa juu ya wanadamu, na juu ya wanyama. Kutoka 8:18

The magicians tried with their enchantments to bring forth lice, but they couldn't. There were lice on man, and on animal.

Ndipo wale waganga wakamwambia Farao, Jambo hili ni chanda cha Mungu; na moyo wake Farao ukawa mgumu asiwasikize; vile vile kama Bwana alivyonena. Kutoka 8:19

Then the magicians said to Pharaoh, "This is the finger of God:" and Pharaoh's heart was hardened, and he didn't listen to them; as Yahweh had spoken.

Bwana akamwambia Musa, Inuka asubuhi na mapema usimame mbele ya Farao; angalia! Atoka aende majini; kamwambie, Bwana asema, Wape watu wangu ruhusa waende zao, ili wanitumikie mimi. Kutoka 8:20

Yahweh said to Moses, "Rise up early in the morning, and stand before Pharaoh; behold, he comes forth to the water; and tell him, 'This is what Yahweh says, "Let my people go, that they may serve me.

Au kwamba huwapi ruhusa watu wangu, tazama, nitaleta wingi wa mainzi juu yako wewe, na juu ya watumishi wako, na juu ya watu wako, nao wataingia ndani ya nyumba zako; na nyumba za Wamisri zitajawa na wingi wa mainzi, na nchi nayo ambayo wa juu yake. Kutoka 8:21

Else, if you will not let my people go, behold, I will send swarms of flies on you, and on your servants, and on your people, and into your houses: and the houses of the Egyptians shall be full of swarms of flies, and also the ground whereon they are.

Nami siku hiyo nitatenga nchi ya Gosheni, watu wangu wanayokaa, ili hao mainzi wasiwe huko; ili kwamba upate kujua wewe ya kuwa mimi ndimi Bwana kati ya dunia. Kutoka 8:22

I will set apart in that day the land of Goshen, in which my people dwell, that no swarms of flies shall be there; to the end you may know that I am Yahweh in the midst of the earth.

Nami nitatia mpaka kati ya watu wangu na watu wako; ishara hiyo italetwa kesho. Kutoka 8:23

I will put a division between my people and your people: by tomorrow shall this sign be."'"

Bwana akafanya; wakaja wingi wa mainzi kwa uzito sana, wakaingia nyumbani mwa Farao, na katika nyumba za watumishi wake, tena katika nchi yote ya Misri; nayo nchi iliharibiwa kwa ajili ya wale mainzi. Kutoka 8:24

Yahweh did so; and there came grievous swarms of flies into the house of Pharaoh, and into his servants' houses: and in all the land of Egypt the land was corrupted by reason of the swarms of flies.

Farao akawaita Musa na Haruni akawaambia, Endeni mkamtolee Mungu wenu dhabihu ndani ya nchi hii. Kutoka 8:25

Pharaoh called for Moses and for Aaron, and said, "Go, sacrifice to your God in the land!"

Musa akasema, Haitupasi kufanya hivyo; kwa kuwa tutamchinjia sadaka Bwana, Mungu wetu, na hayo machukizo ya Wamisri; je! Tutachinja sadaka ya hayo machukizo ya Wamisri mbele ya macho yao, wasitupige kwa mawe? Kutoka 8:26

Moses said, "It isn't appropriate to do so; for we shall sacrifice the abomination of the Egyptians to Yahweh our God. Behold, shall we sacrifice the abomination of the Egyptians before their eyes, and won't they stone us?

La, tutakwenda safari ya siku tatu jangwani, tumchinjie dhabihu Bwana, Mungu wetu, kama atakavyotuagiza. Kutoka 8:27

We will go three days' journey into the wilderness, and sacrifice to Yahweh our God, as he shall command us."

Farao akasema, Mimi nitawapa ruhusa mwende, ili mmchinjie dhabihu Bwana, Mungu wenu, jangwani; lakini hamtakwenda mbali sana; haya niombeeni. Kutoka 8:28

Pharaoh said, "I will let you go, that you may sacrifice to Yahweh your God in the wilderness, only you shall not go very far away. Pray for me."

Musa akasema, Tazama, mimi natoka kwako, nami nitamwomba Bwana ili hao mainzi wamtoke Farao, na watumishi wake, na watu wake kesho; lakini Farao asitende kwa udanganyifu tena, kwa kutowaacha watu waende kumchinjia Bwana dhabihu. Kutoka 8:29

Moses said, "Behold, I go out from you, and I will pray to Yahweh that the swarms of flies may depart from Pharaoh, from his servants, and from his people, tomorrow; only don't let Pharaoh deal deceitfully any more in not letting the people go to sacrifice to Yahweh."

Musa akatoka kwa Farao, akamwomba Bwana. Kutoka 8:30

Moses went out from Pharaoh, and prayed to Yahweh.

Bwana akafanya kama neno la Musa, akawaondoa wale mainzi wabaya kwake Farao, na kwa watumishi wake, na watu wake; hakusalia hata mmoja. Kutoka 8:31

Yahweh did according to the word of Moses, and he removed the swarms of flies from Pharaoh, from his servants, and from his people. There remained not one.

Farao akaufanya moyo wake kuwa mzito mara hiyo nayo, wala hakuwapa ruhusa hao watu waende zao. Kutoka 8:32

Pharaoh hardened his heart this time also, and he didn't let the people go.