Kutoka 15 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kutoka 15 (Swahili) Exodus 15 (English)

Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia Bwana wimbo huu wakanena, na kusema, Nitamwimbia Bwana, kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini. Kutoka 15:1

Then Moses and the children of Israel sang this song to Yahweh, and said, "I will sing to Yahweh, for he has triumphed gloriously: The horse and his rider he has thrown into the sea.

Bwana ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza. Kutoka 15:2

Yah is my strength and song, He has become my salvation: This is my God, and I will praise him; My father's God, and I will exalt him.

Bwana ni mtu wa vita, Bwana ndilo jina lake. Kutoka 15:3

Yahweh is a man of war. Yahweh is his name.

Magari ya Farao na jeshi lake amewatupa baharini, Maakida yake wateule wamezama katika bahari ya Shamu. Kutoka 15:4

Pharaoh's chariots and his host has he cast into the sea; His chosen captains are sunk in the Red Sea.

Vilindi vimewafunikiza, Walizama vilindini kama jiwe. Kutoka 15:5

The deeps cover them. They went down into the depths like a stone.

Bwana, mkono wako wa kuume umepata fahari ya uwezo, Bwana, mkono wako wa kuume wawaseta-seta adui. Kutoka 15:6

Your right hand, Yahweh, is glorious in power, Your right hand, Yahweh, dashes the enemy in pieces.

Kwa wingi wa ukuu wako wawaangusha chini wanaokuondokea, Wapeleka hasira yako, nayo huwateketeza kama mabua makavu. Kutoka 15:7

In the greatness of your excellency, you overthrow those who rise up against you: You send forth your wrath. It consumes them as stubble.

Kwa upepo wa mianzi ya pua yako maji yalipandishwa, Mawimbi yakasimama juu wima mfano wa chungu, Vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari. Kutoka 15:8

With the blast of your nostrils the waters were piled up. The floods stood upright as a heap. The deeps were congealed in the heart of the sea.

Adui akasema, Nitafuatia, nitapata, nitagawanya nyara, Nafsi yangu itashibishwa na wao; Nitaufuta upanga wangu, mkono wangu utawaangamiza. Kutoka 15:9

The enemy said, 'I will pursue, I will overtake, I will divide the spoil. My desire shall be satisfied on them. I will draw my sword, my hand shall destroy them.'

Ulivuma kwa upepo wako, bahari ikawafunikiza; Wakazama kama risasi ndani ya maji makuu. Kutoka 15:10

You blew with your wind. The sea covered them. They sank like lead in the mighty waters.

Ee Bwana, katika miungu ni nani aliye kama wewe? Ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu, Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu? Kutoka 15:11

Who is like you, Yahweh, among the gods? Who is like you, glorious in holiness, Fearful in praises, doing wonders?

Ulinyosha mkono wako wa kuume, Nchi ikawameza. Kutoka 15:12

You stretched out your right hand. The earth swallowed them.

Wewe kwa rehema zako umewaongoza watu uliowakomboa, Kwa uweza wako uliwaelekeza hata makao yako matakatifu. Kutoka 15:13

"You, in your loving kindness, have led the people that you have redeemed. You have guided them in your strength to your holy habitation.

Kabila za watu wamesikia, wanatetemeka, Wakaao Ufilisti utungu umewashika. Kutoka 15:14

The peoples have heard. They tremble. Pangs have taken hold on the inhabitants of Philistia.

Ndipo majumbe wa Edomu wakashangaa, Watu wa Moabu wenye nguvu tetemeko limewapata, Watu wote wakaao Kanaani wameyeyuka. Kutoka 15:15

Then the chiefs of Edom were dismayed. Trembling takes hold of the mighty men of Moab. All the inhabitants of Canaan are melted away.

Hofu na woga umewaangukia; Kwa uweza wa mkono wako wanakaa kimya kama jiwe; Hata watakapovuka watu wako, Ee Bwana, Hata watakapovuka watu wako uliowanunua. Kutoka 15:16

Terror and dread falls on them. By the greatness of your arm they are as still as a stone; Until your people pass over, Yahweh, Until the people pass over who you have purchased.

Utawaingiza, na kuwapanda katika mlima wa urithi wako, Mahali pale ulipojifanyia, Ee Bwana, ili upakae, Pale patakatifu ulipopaweka imara, Bwana, kwa mikono yako. Kutoka 15:17

You shall bring them in, and plant them in the mountain of your inheritance, The place, Yahweh, which you have made for yourself to dwell in; The sanctuary, Lord, which your hands have established.

Bwana atatawala milele na milele. Kutoka 15:18

Yahweh shall reign forever and ever."

Kwa maana farasi za Farao na magari yake na wapanda farasi wake waliingia ndani ya bahari, Bwana akayarudisha maji ya bahari juu yao; bali wana wa Israeli walikwenda katika nchi kavu katikati ya bahari. Kutoka 15:19

For the horses of Pharaoh went in with his chariots and with his horsemen into the sea, and Yahweh brought back the waters of the sea on them; but the children of Israel walked on dry land in the midst of the sea.

Na Miriamu, nabii mke, ndugu yake Haruni, akatwaa tari mkononi mwake; wanawake wakatoka wote wakaenda nyuma yake, wenye matari na kucheza. Kutoka 15:20

Miriam the prophetess, the sister of Aaron, took a tambourine in her hand; and all the women went out after her with tambourines and with dances.

Miriamu akawaitikia,Mwimbieni Bwana ,kwa maana ametukuka sana;Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini. Kutoka 15:21

Miriam answered them, "Sing to Yahweh, for he has triumphed gloriously: The horse and his rider he has thrown into the sea."

Musa akawaongoza Israeli waende mbele kutoka Bahari ya Shamu, nao wakatokea kwa jangwa la Shuri; wakaenda safari ya siku tatu jangwani wasione maji. Kutoka 15:22

Moses led Israel onward from the Red Sea, and they went out into the wilderness of Shur; and they went three days in the wilderness, and found no water.

Walipofika mahali palipoitwa Mara hawakupata kuyanywa yale maji ya Mara, kwa kuwa yalikuwa machungu; kwa ajili ya hayo jina lake likaitwa Mara. Kutoka 15:23

When they came to Marah, they couldn't drink from the waters of Marah, for they were bitter. Therefore the name of it was called Marah.{Marah means bitter.}

Ndipo watu wakamnung'unikia Musa, wakisema, Tunywe nini? Kutoka 15:24

The people murmured against Moses, saying, "What shall we drink?"

Naye akamlilia Bwana; Bwana akamwonyesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, akawaonja huko; Kutoka 15:25

Then he cried to Yahweh. Yahweh shown him a tree, and he threw it into the waters, and the waters were made sweet. There he made a statute and an ordinance for them, and there he tested them;

akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi Bwana nikuponyaye. Kutoka 15:26

and he said, "If you will diligently listen to the voice of Yahweh your God, and will do that which is right in his eyes, and will pay attention to his commandments, and keep all his statutes, I will put none of the diseases on you, which I have put on the Egyptians; for I am Yahweh who heals you."

Wakafikilia Elimu, palipokuwa na chemchemi kumi na mbili, na mitende sabini; wakapanga hapo, karibu na maji.

Kutoka 15:27

They came to Elim, where there were twelve springs of water, and seventy palm trees: and they encamped there by the waters.