Kutoka 20 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kutoka 20 (Swahili) Exodus 20 (English)

Mungu akanena maneno haya yote akasema, Kutoka 20:1

God{After "God," the Hebrew has the two letters "Aleph Tav" (the first and last letters of the Hebrew alphabet), not as a word, but as a grammatical marker.} spoke all these words, saying,

Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Kutoka 20:2

"I am Yahweh your God, who brought you out of the land of Egypt, out of the house of bondage.

Usiwe na miungu mingine ila mimi. Kutoka 20:3

You shall have no other gods before me.

Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Kutoka 20:4

"You shall not make for yourselves an idol, nor any image of anything that is in the heavens above, or that is in the earth beneath, or that is in the water under the earth:

Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, Kutoka 20:5

you shall not bow yourself down to them, nor serve them, for I, Yahweh your God, am a jealous God, visiting the iniquity of the fathers on the children, on the third and on the fourth generation of those who hate me,

nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu. Kutoka 20:6

and showing loving kindness to thousands of those who love me and keep my commandments.

Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure. Kutoka 20:7

"You shall not take the name of Yahweh your God in vain, for Yahweh will not hold him guiltless who takes his name in vain.

Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Kutoka 20:8

"Remember the Sabbath day, to keep it holy.

Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; Kutoka 20:9

You shall labor six days, and do all your work,

lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Kutoka 20:10

but the seventh day is a Sabbath to Yahweh your God. You shall not do any work in it, you, nor your son, nor your daughter, your man-servant, nor your maid-servant, nor your cattle, nor your stranger who is within your gates;

Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa. Kutoka 20:11

for in six days Yahweh made heaven and earth, the sea, and all that is in them, and rested the seventh day; therefore Yahweh blessed the Sabbath day, and made it holy.

Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako. Kutoka 20:12

"Honor your father and your mother, that your days may be long in the land which Yahweh your God gives you.

Usiue. Kutoka 20:13

"You shall not murder.

Usizini. Kutoka 20:14

"You shall not commit adultery.

Usiibe. Kutoka 20:15

"You shall not steal.

Usimshuhudie jirani yako uongo. Kutoka 20:16

"You shall not give false testimony against your neighbor.

Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako. Kutoka 20:17

"You shall not covet your neighbor's house. You shall not covet your neighbor's wife, nor his man-servant, nor his maid-servant, nor his ox, nor his donkey, nor anything that is your neighbor's."

Watu wote wakaona umeme na ngurumo na sauti ya baragumu, na ule mlima kutoka moshi; na watu walipoona hayo wakatetemeka, wakasimama mbali. Kutoka 20:18

All the people perceived the thunderings, the lightnings, the sound of the trumpet, and the mountain smoking. When the people saw it, they trembled, and stayed at a distance.

Wakamwambia Musa, Sema nasi wewe, nasi tutasikia, bali Mungu asiseme nasi, tusije tukafa. Kutoka 20:19

They said to Moses, "Speak with us yourself, and we will listen; but don't let God speak with us, lest we die."

Musa akawaambia watu, Msiogope, maana Mungu amekuja ili awajaribu, na utisho wake uwe mbele yenu, ili kwamba msifanye dhambi. Kutoka 20:20

Moses said to the people, "Don't be afraid, for God has come to test you, and that his fear may be before you, that you won't sin."

Basi hao watu wakasimama mbali, naye Musa akalikaribia lile giza kuu Mungu alipokuwapo. Kutoka 20:21

The people stayed at a distance, and Moses drew near to the thick darkness where God was.

Bwana akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli hivi, Ninyi wenyewe mmeona ya kuwa nimenena nanyi kutoka mbinguni. Kutoka 20:22

Yahweh said to Moses, "This is what you shall tell the children of Israel: 'You yourselves have seen that I have talked with you from heaven.

Msifanye miungu mingine pamoja nami; miungu ya fedha, wala miungu ya dhahabu, msijifanyie. Kutoka 20:23

You shall most certainly not make alongside of me gods of silver, or gods of gold for yourselves.

Utanifanyia madhabahu ya udongo, nawe utatoa dhabihu zako juu yake; sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani, kondoo zako, na ng'ombe zako, kila mahali nitakapotia ukumbusho wa jina langu, hapo ndipo nitakapokujilia na kukubarikia. Kutoka 20:24

You shall make an altar of earth for me, and shall sacrifice on it your burnt offerings and your peace-offerings, your sheep and your oxen. In every place where I record my name I will come to you and I will bless you.

Nawe ukinifanyia madhabahu ya mawe, hutaijenga ya mawe yaliyochongwa; kwa kuwa ukiwa wewe umetumia chombo chako katika kuichonga umeitia unajisi. Kutoka 20:25

If you make me an altar of stone, you shall not build it of hewn stones; for if you lift up your tool on it, you have polluted it.

Tena hutapanda kwenda madhabahuni kwangu kwa daraja, uchi wako usidhihirike juu yake.

Kutoka 20:26

Neither shall you go up by steps to my altar, that your nakedness may not be exposed to it.'