Kutoka 17 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kutoka 17 (Swahili) Exodus 17 (English)

Mkutano wote wa wana wa Israeli ukasafiri, kutoka bara ya Sini kwa safari zao, kama Bwana alivyowaagiza, wakatua Refidimu; napo hapakuwa na maji, watu wanywe. Kutoka 17:1

All the congregation of the children of Israel traveled from the wilderness of Sin, by their journeys, according to Yahweh's commandment, and encamped in Rephidim; but there was no water for the people to drink.

Kwa hiyo hao watu wakateta na Musa, wakasema, Tupe maji tunywe. Musa akawaambia, Kwani kuteta na mimi? Mbona mnamjaribu Bwana? Kutoka 17:2

Therefore the people quarreled with Moses, and said, "Give us water to drink." Moses said to them, "Why do you quarrel with me? Why do you test Yahweh?"

Watu wakawa na kiu huko; nao wakamnung'unikia Musa, wakasema, Mbona umetupandisha kutoka Misri, kutuua sisi na watoto wetu na wanyama wetu kwa kiu? Kutoka 17:3

The people were thirsty for water there; and the people murmured against Moses, and said, "Why have you brought us up out of Egypt, to kill us, our children, and our livestock with thirst?"

Musa akamlilia Bwana, akisema, Niwatendee nini watu hawa? Bado kidogo nao watanipiga kwa mawe. Kutoka 17:4

Moses cried to Yahweh, saying, "What shall I do with these people? They are almost ready to stone me."

Bwana akamwambia Musa, Pita mbele ya watu, ukawachukue baadhi ya wazee wa Israeli pamoja nawe; na ile fimbo yako ambayo uliupiga mto kwayo, uitwae mkononi mwako, ukaende. Kutoka 17:5

Yahweh said to Moses, "Walk on before the people, and take the elders of Israel with you, and take the rod in your hand with which you struck the Nile, and go.

Tazama, nitasimama mbele yako huko, juu ya lile jabali katika Horebu; nawe utalipiga jabali, na maji yatatoka, watu wapate kunywa. Musa akafanya hivyo mbele ya wazee wa Israeli. Kutoka 17:6

Behold, I will stand before you there on the rock in Horeb. You shall strike the rock, and water will come out of it, that the people may drink." Moses did so in the sight of the elders of Israel.

Akapaita mahali pale jina lake Masa, na Meriba; kwa sababu ya mateto ya wana wa Israeli, na kwa sababu walimjaribu Bwana, wakisema, Je! Bwana yu kati yetu au sivyo? Kutoka 17:7

He called the name of the place Massah,{Massah means testing.} and Meribah,{Meribah means quarreling.} because the children of Israel quarreled, and because they tested Yahweh, saying, "Is Yahweh among us, or not?"

Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu. Kutoka 17:8

Then Amalek came and fought with Israel in Rephidim.

Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, ukatoke upigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu. Kutoka 17:9

Moses said to Joshua, "Choose men for us, and go out, fight with Amalek. Tomorrow I will stand on the top of the hill with God's rod in my hand."

Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima. Kutoka 17:10

So Joshua did as Moses had told him, and fought with Amalek; and Moses, Aaron, and Hur went up to the top of the hill.

Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda. Kutoka 17:11

It happened, when Moses held up his hand, that Israel prevailed; and when he let down his hand, Amalek prevailed.

Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa. Kutoka 17:12

But Moses' hands were heavy; and they took a stone, and put it under him, and he sat on it. Aaron and Hur held up his hands, the one on the one side, and the other on the other side. His hands were steady until sunset.

Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga. Kutoka 17:13

Joshua defeated Amalek and his people with the edge of the sword.

Bwana akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu. Kutoka 17:14

Yahweh said to Moses, "Write this for a memorial in a book, and rehearse it in the ears of Joshua: that I will utterly blot out the memory of Amalek from under the sky."

Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yehova-nisi; Kutoka 17:15

Moses built an altar, and called the name of it Yahweh our Banner.{Hebrew, Yahweh Nissi}

akasema, Bwana ameapa; Bwana atakuwa na vita na Amaleki kizazi baada ya kizazi. Kutoka 17:16

He said, "Yah has sworn: 'Yahweh will have war with Amalek from generation to generation.'"