Kutoka 16

Exodus Chapter 16

Download Audio (Pakua)
« Orodha ya Sura
English Translation
1
Kisha wakasafiri kutoka Elimu, na mkutano wote wa wana wa Israeli wakafikilia bara ya Sini, iliyoko kati ya Elimu na Sinai, siku ya kumi na tano ya mwezi wa pili baada ya kutoka kwao nchi ya Misri.
They took their journey from Elim, and all the congregation of the children of Israel came to the wilderness of Sin, which is between Elim and Sinai, on the fifteenth day of the second month after their departing out of the land of Egypt.
2
Na mkutano mzima wa wana wa Israeli ukawanung'unikia Musa na Haruni, huko barani;
The whole congregation of the children of Israel murmured against Moses and against Aaron in the wilderness;
3
wana wa Israeli wakawaambia, Laiti tungalikufa kwa mkono wa Bwana katika nchi ya Misri, hapo tulipoketi karibu na zile sufuria za nyama, tulipokula vyakula hata kushiba; kwani mmetutoa huko na kututia katika bara hii, ili kutuua kwa njaa kusanyiko hili lote.
and the children of Israel said to them, "We wish that we had died by the hand of Yahweh in the land of Egypt, when we sat by the flesh-pots, when we ate our fill of bread, for you have brought us out into this wilderness, to kill this whole assembly with hunger."
4
Ndipo Bwana akamwambia Musa, Tazama, mimi nitawanyeshea ninyi mvua ya mkate kutoka mbinguni; na hao watu watatoka nje na kuokota kila siku sehemu ya siku; ili nipate kuwajaribu, kwamba watakwenda katika sheria yangu, ama sivyo.
Then said Yahweh to Moses, "Behold, I will rain bread from the sky for you, and the people shall go out and gather a day's portion every day, that I may test them, whether they will walk in my law, or not.
5
Kisha itakuwa siku ya sita, ya kwamba watayaandaa hayo watakayoleta ndani, nayo yatakuwa ni mara mbili kuliko wayaokotayo kila siku.
It shall come to pass on the sixth day, that they shall prepare that which they bring in, and it shall be twice as much as they gather daily."
6
Musa na Haruni wakawaambia wana wote wa Israeli, Jioni ndipo mtakapojua ya kuwa Bwana amewaleta kutoka nchi ya Misri;
Moses and Aaron said to all the children of Israel, "At evening, then you shall know that Yahweh has brought you out from the land of Egypt;
7
na asubuhi ndipo mtakapouona utukufu wa Bwana; kwa kuwa yeye asikia manung'uniko yenu mliyomnung'unikia Bwana; na sisi tu nani, hata mkatunung'unikia?
and in the morning, then you shall see the glory of Yahweh; because he hears your murmurings against Yahweh. Who are we, that you murmur against us?"
8
Musa akasema, Ndilo litakalokuwa, hapo Bwana atakapowapa nyama wakati wa jioni mle, na asubuhi mikate hata mkakinai; kwa kuwa Bwana asikia manung'uniko yenu mliyomnung'unikia yeye; na sisi tu nani? Manung'uniko yenu hayakuwa juu yetu sisi, ila juu ya Bwana.
Moses said, "Now Yahweh shall give you meat to eat in the evening, and in the morning bread to satisfy you; because Yahweh hears your murmurings which you murmur against him. And who are we? Your murmurings are not against us, but against Yahweh."
9
Musa akamwambia Haruni, Haya, sema na mkutano wote wa wana wa Israeli, Njoni karibu mbele ya Bwana; kwa kuwa yeye ameyasikia manung'uniko yenu.
Moses said to Aaron, "Tell all the congregation of the children of Israel, 'Come near before Yahweh, for he has heard your murmurings.'"
10
Ilikuwa Haruni aliponena na huo mkutano wote wa wana wa Israeli, wakaangalia upande wa bara, na tazama, utukufu wa Bwana ukaonekana katika hilo wingu.
It happened, as Aaron spoke to the whole congregation of the children of Israel, that they looked toward the wilderness, and, behold, the glory of Yahweh appeared in the cloud.
11
Bwana akasema na Musa, akinena,
Yahweh spoke to Moses, saying,
12
Nimeyasikia manung'uniko ya wana wa Israeli; haya sema nao, ukinena, Wakati wa jioni mtakula nyama, na wakati wa asubuhi mtashiba mkate; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.
"I have heard the murmurings of the children of Israel. Speak to them, saying, 'At evening you shall eat meat, and in the morning you shall be filled with bread: and you shall know that I am Yahweh your God.'"
13
Ikawa wakati wa jioni, kware wakakaribia, wakakifunikiza kituo; na wakati wa asubuhi umande ulikuwa juu ya nchi pande zote za kituo.
It happened at evening that quail came up and covered the camp; and in the morning the dew lay around the camp.
14
Na ulipoinuka ule umande uliokuwa juu ya nchi, kumbe! Juu ya uso wa bara kitu kidogo kilichoviringana, kidogo kama sakitu juu ya nchi.
When the dew that lay had gone, behold, on the surface of the wilderness was a small round thing, small as the hoar-frost on the ground.
15
Wana wa Israeli walipokiona, wakaambiana, Nini hiki? Maana hawakujua ni kitu gani. Musa akawaambia, Ndio mkate ambao Bwana amewapa ninyi, mle.
When the children of Israel saw it, they said one to another, "What is it?" For they didn't know what it was. Moses said to them, "It is the bread which Yahweh has given you to eat."
16
Neno hili ndilo aliloagiza Bwana, Okoteni ninyi kitu hicho kila mtu kama ulaji wake ulivyo; kichwa pishi,kama hesabu ya watu wenu ilivyo ;ndivyo mtakavyotwaa,kila mtu kwa ajili ya hao walioko hemani mwake.
This is the thing which Yahweh has commanded: "Gather of it everyone according to his eating; an omer a head, according to the number of your persons, shall you take it, every man for those who are in his tent."
17
Wana wa Israeli wakafanya hivyo, wakaokota wengine zaidi, wengine kupungua.
The children of Israel did so, and gathered some more, some less.
18
Nao walipoipima kwa pishi, yeye aliyekuwa ameokota kingi hakubakiwa na kitu, na yeye aliyekuwa ameokota kichache hakupungukiwa; wakaokota kila mtu kama ulaji wake ulivyokuwa.
When they measured it with an omer, he who gathered much had nothing over, and he who gathered little had no lack. They gathered every man according to his eating.
19
Musa akawaambia, Mtu awaye yote asikisaze hata asubuhi.
Moses said to them, "Let no one leave of it until the morning."
20
Lakini hawakumsikiza Musa; wengine miongoni mwao wakakisaza hata asubuhi, nacho kikaingia mabuu na kutoa uvundo; Musa akawakasirikia sana.
Notwithstanding they didn't listen to Moses, but some of them left of it until the morning, and it bred worms, and became foul: and Moses was angry with them.
21
Basi wakaokota asubuhi baada ya asubuhi, kila mtu kama ulaji wake ulivyokuwa; na hapo jua lilipokuwa ni kali, kikayeyuka.
They gathered it morning by morning, everyone according to his eating. When the sun grew hot, it melted.
22
Basi ikawa siku ya sita wakaokota kile chakula sehemu maradufu, kila mtu pishi mbili; na wazee wote wa mkutano wakaenda na kumwambia Musa.
It happened that on the sixth day they gathered twice as much bread, two omers for each one, and all the rulers of the congregation came and told Moses.
23
Akawaambia, Ndilo neno alilonena Bwana Kesho ni starehe takatifu, Sabato takatifu kwa Bwana; okeni mtakachooka, na kutokosa mtakachotokosa; na hicho kitakachowasalia jiwekeeni kilindwe hata asubuhi.
He said to them, "This is that which Yahweh has spoken, 'Tomorrow is a solemn rest, a holy Sabbath to Yahweh. Bake that which you want to bake, and boil that which you want to boil; and all that remains over lay up for yourselves to be kept until the morning."
24
Basi wakakiweka hata asubuhi, kama Musa alivyowaagiza; nacho hakikutoa uvundo wala kuingia mabuu.
They laid it up until the morning, as Moses asked, and it didn't become foul, neither was there any worm in it.
25
Musa akasema, Haya, kuleni hiki leo; kwa kuwa leo ni Sabato ya Bwana; leo hamtakiona nje barani.
Moses said, "Eat that today, for today is a Sabbath to Yahweh. Today you shall not find it in the field.
26
Siku sita mtaokota; lakini siku ya saba ni Sabato, siku hiyo hakitapatikana.
Six days you shall gather it, but on the seventh day is the Sabbath. In it there shall be none."
27
Ikawa siku ya saba wengine wakatoka kwenda kukiokota, wasikione.
It happened on the seventh day, that some of the people went out to gather, and they found none.
28
Bwana akamwambia Musa, Mtakataa kuyashika maagizo yangu na sheria zangu hata lini?
Yahweh said to Moses, "How long do you refuse to keep my commandments and my laws?
29
Angalieni, kwa kuwa Bwana amewapa ninyi hiyo Sabato, kwa sababu hii huwapa siku ya sita chakula cha siku mbili; kaeni kila mtu mahali pake, mtu awaye yote asiondoke mahali pake kwa siku ya saba.
Behold, because Yahweh has given you the Sabbath, therefore he gives you on the sixth day the bread of two days. Everyone stay in his place. Let no one go out of his place on the seventh day."
30
Basi hao watu wakapumzika kwa siku ya saba.
So the people rested on the seventh day.
31
Na nyumba ya Israeli wakakiita jina lake Mana; nacho kilikuwa mfano wa chembe za mtama, nyeupe; na tamu yake ilikuwa kama tamu ya maandazi membamba yaliyoandaliwa kwa asali.
The house of Israel called the name of it Manna,{"Mana" means "What is it?"} and it was like coriander seed, white; and its taste was like wafers with honey.
32
Musa akasema, Hili ni neno Bwana aliloliamuru, Pishi moja ya kitu hicho na kiwekwe kwa ajili ya vizazi vyenu; ili kwamba wao wapate kukiona kile chakula nilichowalisha ninyi barani, hapo nilipowaleta kutoka nchi ya Misri.
Moses said, "This is the thing which Yahweh has commanded, 'Let an omer-full of it be kept throughout your generations, that they may see the bread with which I fed you in the wilderness, when I brought you forth from the land of Egypt."
33
Basi Musa akamwambia Haruni, Twaa kopo, ukatie pishi moja ya hiyo Mana ndani yake, uiweke mbele ya Bwana, ilindwe kwa ajili ya vizazi vyenu.
Moses said to Aaron, "Take a pot, and put an omer-full of manna in it, and lay it up before Yahweh, to be kept throughout your generations."
34
Kama vile Bwana alivyomwagizia Musa ndivyo Haruni alivyoiweka hapo mbele ya Ushahidi, ili ilindwe.
As Yahweh commanded Moses, so Aaron laid it up before the Testimony, to be kept.
35
Na wana wa Israeli walikula Mana muda wa miaka arobaini, hata walipofikilia nchi iliyo na watu, wakala ile Mana, hata walipofikilia mipakani mwa nchi ya Kanaani.
The children of Israel ate the manna forty years, until they came to an inhabited land. They ate the manna until they came to the borders of the land of Canaan.
36
Hiyo omeri ni sehemu kumi ya efa. </p>
Now an omer is the tenth part of an ephah.
« 15 17 »

Chagua Sura Nyingine (Select Chapter)