Kutoka 38 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kutoka 38 (Swahili) Exodus 38 (English)

Kisha akafanya hiyo madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, ya mti wa mshita urefu wake ulikuwa dhiraa tano, na upana wake ulikuwa dhiraa tano, ilikuwa mraba; na kwenda juu kwake kulikuwa dhiraa tatu. Kutoka 38:1

He made the altar of burnt offering of acacia wood. It was square. Its length was five cubits, its breadth was five cubits, and its height was three cubits.

Naye akazifanya pembe zake katika ncha zake nne; hizo pembe zilikuwa za kitu kimoja nayo; naye akaifunika shaba. Kutoka 38:2

He made its horns on its four corners. Its horns were of one piece with it, and he overlaid it with brass.

Kisha akafanya vyombo vyote vya madhabahu, yaani sufuria zake, na majembe yake, na mabakuli yake, na uma zake, na meko yake; vyombo vyake vyote akavifanya vya shaba. Kutoka 38:3

He made all the vessels of the altar, the pots, the shovels, the basins, the flesh-hooks, and the fire pans. He made all its vessels of brass.

Naye akaifanyia madhabahu wavu wa shaba, akautia chini ya ukingo kuizunguka pande zote, ukawa katikati ya hiyo madhabahu. Kutoka 38:4

He made for the altar a grating of a network of brass, under the ledge around it beneath, reaching halfway up.

Naye akasubu vikuku vinne kwa kutiwa katika pembe nne za huo wavu wa shaba, viwe mahali pa kutia ile miti ya kuichukulia. Kutoka 38:5

He cast four rings for the four ends of brass grating, to be places for the poles.

Naye akaifanya hiyo miti kwa mti wa mshita na kuifunika shaba. Kutoka 38:6

He made the poles of acacia wood, and overlaid them with brass.

Naye akaitia ile miti katika vile vikuku vilivyokuwa katika mbavu za hiyo madhabahu, ili kuichukua; akaifanya yenye mvungu ndani, kwa zile mbao. Kutoka 38:7

He put the poles into the rings on the sides of the altar, with which to carry it. He made it hollow with planks.

Kisha akafanya hilo birika la shaba, na tako lake la shaba; shaba hiyo ilikuwa ni ya vioo vya wanawake wenye kutumika, waliokuwa wakitumika mlangoni mwa hema ya kukutania. Kutoka 38:8

He made the basin of brass, and its base of brass, out of the mirrors of the ministering women who ministered at the door of the tent of meeting.

Naye akafanya ule ua; upande wa kusini kwa kuelekea kusini, chandarua ya ua ilikuwa ya nguo ya kitani nzuri ya kusokotwa, kiasi cha dhiraa mia; Kutoka 38:9

He made the court: for the south side southward the hangings of the court were of fine twined linen, one hundred cubits;

nguzo zake zilikuwa ishirini, na matako yake yalikuwa ishirini, yalikuwa ya shaba; kulabu za nguzo na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha. Kutoka 38:10

their pillars were twenty, and their sockets twenty, of brass; the hooks of the pillars and their fillets were of silver.

Upande wa kaskazini ulikuwa ni dhiraa mia vivyo, nguzo zake ishirini na matako yake ishirini, yalikuwa ni ya shaba; kulabu za nguzo na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha. Kutoka 38:11

For the north side one hundred cubits, their pillars twenty, and their sockets twenty, of brass; the hooks of the pillars, and their fillets, of silver.

Upande wa magharibi mlikuwa na chandarua ya dhiraa hamsini, nguzo zake zilikuwa ni kumi, na matako yake kumi; kulabu za hizo nguzo na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha. Kutoka 38:12

For the west side were hangings of fifty cubits, their pillars ten, and their sockets ten; the hooks of the pillars, and their fillets, of silver.

Upande wa mashariki kuelekea mashariki dhiraa hamsini. Kutoka 38:13

For the east side eastward fifty cubits.

Chandarua ya upande mmoja wa lango ilikuwa dhiraa kumi na tano urefu wake; na nguzo zake tatu, na matako yake matatu; Kutoka 38:14

The hangings for the one side were fifteen cubits; their pillars three, and their sockets three;

ni vivyo upande wa pili; upande huu na huu langoni mwa ua mlikuwa na chandarua ya dhiraa kumi na tano urefu wake; nguzo zake zilikuwa ni tatu, na matako yake matatu. Kutoka 38:15

and so for the other side: on this hand and that hand by the gate of the court were hangings of fifteen cubits; their pillars three, and their sockets three.

Chandarua za nguo zote za ule ua zilizouzunguka pande zote zilikuwa za nguo ya kitani nzuri iliyosokotwa. Kutoka 38:16

All the hangings around the court were of fine twined linen.

Na matako ya zile nguzo yalikuwa ya shaba; kulabu za hizo nguzo na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha; na vichwa vya zile nguzo vilikuwa ni vya fedha; na nguzo zote za huo ua ziliungwa kwa vitanzi vya fedha. Kutoka 38:17

The sockets for the pillars were of brass. The hooks of the pillars and their fillets were of silver; and the overlaying of their capitals, of silver; and all the pillars of the court were filleted with silver.

Na hilo pazia la lango la ua, lilikuwa ni kazi ya mwenye kutia taraza, lilikuwa la nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri ya kusokotwa; lilikuwa na urefu wake dhiraa ishirini, na kutukuka kwake katika huo upana wake kulikuwa dhiraa tano, kupatana na ile chandarua ya ua. Kutoka 38:18

The screen for the gate of the court was the work of the embroiderer, of blue, purple, scarlet, and fine twined linen. Twenty cubits was the length, and the height in the breadth was five cubits, like to the hangings of the court.

Na nguzo zake zilikuwa nne, na matako yake manne, yalikuwa ya shaba; kulabu zake zilikuwa za fedha, na vichwa vyake na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha. Kutoka 38:19

Their pillars were four, and their sockets four, of brass; their hooks of silver, and the overlaying of their capitals, and their fillets, of silver.

Na vigungi vyote vya maskani, na vya ua ulioizunguka pande zote vilikuwa vya shaba. Kutoka 38:20

All the pins of the tent, and around the court, were of brass.

Jumla ya vile vyombo vilivyofanywa kwa ajili ya hiyo maskani, hiyo maskani ya ushuhuda ni hii, kama vilivyohesabiwa, kama maagizo ya Musa yalivyokuwa, kwa ajili ya utumishi wa Walawi kwa mkono wa Ithamari, mwana wa Haruni, kuhani. Kutoka 38:21

This is the amount of material used for the tent, even the Tent of the Testimony, as they were counted, according to the commandment of Moses, for the service of the Levites, by the hand of Ithamar, the son of Aaron the priest.

Na Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda, akafanya yote Bwana aliyomwagiza Musa. Kutoka 38:22

Bezalel the son of Uri, the son of Hur, of the tribe of Judah, made all that Yahweh commanded Moses.

Na pamoja naye alikuwa na Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani, aliyekuwa fundi wa kuchora nakshi, mfanyaji wa kazi mwerevu, naye alikuwa mwenye kutia taraza za nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri. Kutoka 38:23

With him was Oholiab, the son of Ahisamach, of the tribe of Dan, an engraver, and a skillful workman, and an embroiderer in blue, in purple, in scarlet, and in fine linen.

Dhahabu yote iliyotumiwa kwa ajili ya hiyo kazi, katika kazi hiyo yote ya mahali patakatifu, hiyo dhahabu ya matoleo, ilikuwa ni talanta ishirini na kenda, na shekeli mia saba na thelathini, kwa kadiri ya shekeli ya mahali patakatifu. Kutoka 38:24

All the gold that was used for the work in all the work of the sanctuary, even the gold of the offering, was twenty-nine talents, and seven hundred thirty shekels, after the shekel of the sanctuary.

Na fedha ya hao waliohesabiwa, watu wa huo mkutano ilikuwa talanta mia, na shekeli elfu moja na mia saba na sabini na tano kwa kadiri ya shekeli ya mahali patakatifu; Kutoka 38:25

The silver of those who were numbered of the congregation was one hundred talents, and one thousand seven hundred seventy-five shekels, after the shekel of the sanctuary:

kichwa beka, maana, nusu shekeli, kwa kadiri ya shekeli ya mahali patakatifu, kwa ajili ya kila mtu aliyepita kwa wale waliohesabiwa, aliyekuwa wa umri wa miaka ishirini au zaidi, kwa ajili ya watu waume sita mia na tatu elfu, na mia tano na hamsini (603,550). Kutoka 38:26

a beka a head, that is, half a shekel, after the shekel of the sanctuary, for everyone who passed over to those who were numbered, from twenty years old and upward, for six hundred three thousand five hundred fifty men.

Na hizo talanta mia za fedha zilikuwa kwa kusubu yale matako ya mahali patakatifu na matako ya hilo pazia; matako mia kwa hizo talanta mia, talanta moja tako moja. Kutoka 38:27

The one hundred talents of silver were for casting the sockets of the sanctuary, and the sockets of the veil; one hundred sockets for the one hundred talents, a talent for a socket.

Na kwa hizo shekeli elfu moja na mia saba, na sabini na tano, akafanya vifungo vya hizo nguzo, na kuvifunika fedha vile vichwa vyake, na kufanya vitanzi vyake. Kutoka 38:28

Of the one thousand seven hundred seventy-five shekels he made hooks for the pillars, overlaid their capitals, and made fillets for them.

Na hiyo shaba iliyoletwa ilikuwa ni talanta sabini, na shekeli elfu mbili na mia nne. Kutoka 38:29

The brass of the offering was seventy talents, and two thousand four hundred shekels.

Naye akafanya ya hiyo shaba matako kwa ajili ya lango la hema ya kukutania, na hiyo madhabahu ya shaba, na ule wavu wa shaba kwa ajili yake na vyombo vyote vya hiyo madhabahu, Kutoka 38:30

With this he made the sockets to the door of the tent of meeting, the brazen altar, the brazen grating for it, all the vessels of the altar,

na matako ya ua kuuzunguka pande zote, na matako ya lango la huo ua, na vigingi vyote vya maskani, na vigingi vyote vya huo ua uliozunguka pande zote.

Kutoka 38:31

the sockets around the court, the sockets of the gate of the court, all the pins of the tent, and all the pins around the court.